Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Moshi vijijini Kuna Ester Mmassy na Victor Tesha ambao watachuana vikali. Wengine hawana nguvu.

Ubungo yupo Emmanuel Maluli huyu ni Katibu wa Hamasa kata ya Makuburi.

Mwingine ni Cypirian Mrema ambaye Ni mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ubungo.

Pia yupo Kitila Mkumbo. Wengine siwajui
Moshi vijijini,ida mushi wa itv vipi?
 
Haya kumeshakucha tena La mgambo likilia ujue kuna jambo.


Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, leo na kesho ni siku ya Mikutano Mikuu ya CCM ya Majimbo/Wilaya kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge na ujumbe wa baraza la wawakilishi

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Magufuli waliochukua kugombea nafasi za Ubunge na uwakilishi ni 10,367. Waliokamilisha kujaza fomu na kurejesha ni 10,321.

Watanzania wataelekeza zaidi macho na masikio yao maeneo yenye upinzani mkali kama Kigamboni, Arusha mjini, Simanjiro, Kyela, Mbeya mjini, Mwibara, Misungwi, Same Mashariki, Tunduma, Tarime Vijijini na Ubungo ni baadhi ya maeneo yanayoangaliwa kwa jicho la tatu.

Ngoja tuone.

Up dates:

Jimbo la kinondoni jumla ya waliochukuwa fomu ni 81 na waliorejesha ni 79 ambao wanaendelea kujieleza .

Jimbo la Ubungo waliochukuwa fomu ni 113 na waliorejesha ni 111 na wanaendelea kujieleza, Mbarouk Masoud ambaye ni Katibu mwenezi anasema zege halilali.

Arusha mjini kuna watia nia 91 wanaoendelea kujieleza.

Jimbo la Lupembe mkoani Njombe watia nia 19 wanajieleza.

Abas Tarimba anaongoza kwa wingi wa kura za maoni Kinondoni akifuatiwa kwa ukaribu na IDD AZAN kura bado zinaendelea kuhesabiwa mubashara.
Mtulia akuze maembe[emoji16][emoji16]
 
Iramba kura zilizopangwa na Uongozi wa CCM Wilaya

1. Eng. CC Mkali - 4
2. Dr. Mwigulu Nchemba - 27
3. Monica Yongolo --8
4. Lyanga Martin 3
5. Dr Timoth Lyanga - 13
6. Paulo Mkoma 2
7. Abdala Matanga - 3
8. Robert Jackson Makala - 5
9. Vicent Shomela - 3
10. Eng. Jumbe Katala 11
12. Mwl Noel Kingu - 4
13. Matahyo Samson - 9
14. Elia Mpesa 1
15.Elibariki Ndau 1
16. Paulina Makamba - 2
17. Adv. John W. Jacob - 16
18. Sadath Nkuku - 1
19. Herijema Nalaila - 6
20. Babu Khamis Bulali - 3
21. Amani Irunde 1

Dk. Mwigulu Chemba [emoji3581]
Kumbe Nchemba hakubaliki hivyo
 
Temeke vipi wakuu?
Kule Jimbo la Moshi mjini pia ccm imenunuliwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro kumuuzia Jimbo mfanyabiashara ya mabasi ibra line. Kule singida nako chama kinauzwa kwa wafanyabiashara.Hali ni tete
 
kuna utofauti mkubwa ukiangalia idadi ya kura wanazopata wenzake kwenye majimbo mengine.... yaani jimbo lake kura zimetawanyika sana...
Ukiangalia idadi ya wapiga kura ni ndogo
Angalia washindani wake wengi wanapata kura 2 3 mpaka 8 basi
 
Back
Top Bottom