JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kumekuwepo na picha kadhaa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, zikionyesha hali ya viwanja vya michezo vilivyotumika katika mashindano ya AFCON nchini Gabon mwaka 2017 vikiwa katika hali mbaya ya uharibifu na kutelekezwa. Katika baadhi ya picha zinazoonekana kwenye picha hizo, miti imeota ndani ya viwanja hivyo, jambo linaloashiria kuwa havitumiki kwa muda mrefu na havifanyiwi matengenezo ya mara kwa mara. je taarifa hizo zina usahihi kiasi gani ?
Katika jamii ya Kitanzania, baadhi ya mifugo kama vile mbuzi na ng’ombe hufariki wanapokula maganda ya mihogo mibichi. Hali hii huwastaajabisha wafugaji wengi, kwa kuwa mihogo hiyo huwa salama na hata tamu kwa matumizi ya binadamu, lakini inapoliwa na baadhi ya mifugo husababisha madhara makubwa, ikiwemo kifo. ufuatiliaji ambao umefanywa umebainisha kuwa Mihogo ina kemikali zinazoitwa cyanogenic glycosides (hasa linamarin na lotaustralin). Kemikali hizi zikivunjika ndani ya mwili au wakati mihogo inapokatwa/kupondwa, hutengeneza hydrogen cyanide (HCN) ambayo ni sumu kali ndani ya mwili wa mnyama Utafiti ambao umefanywa Tweyongyere,R. & Katongole (2002)umeeleza kuwa sehemu ya nje ya muhogo mara nyingi ina kiwango kikubwa cha cyanide...
Back
Top Bottom