JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na machapisho mbalimbali yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwa na jumbe zinazodaiwa kutolewa na baadhi ya viongozi, hususan wa nchi za Afrika Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya machapisho hayo linadai kuwa aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alisema:"If you want to stop youths from alcohol or playing Aviator, just tell them that it's owned by William Ruto." Chapisho lingine linadai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisema: "Mimi naomba Rais ndugu yangu William Ruto anipe mamlaka niongoze Kenya kwa wiki mbili tu, nimalize huo mchakato wa hao viumbe wa ajabu wanaojiita Gen Z. Ninyooshe nchi ya Kenya." moja ya machapisho yamechapishwa hapa Je...
Inadaiwa kuwa Kalonzo Musyoka amefanya kikao cha siri leo na Rais William Ruto mjini Narok, ambapo walifikia makubaliano ya kushirikiana kabla ya uchaguzi. Haya yanajiri huku kukiwa na uvumi kwamba upinzani unampendelea Edwin Sifuna kuwa mgombea wao wa urais, akisaidiwa na mgombea mwenza kutoka Mlima Kenya, ambaye inadaiwa ni Kiharu MP Ndindi Nyoro. Kwa mujibu wa madai hayo, Kalonzo hayuko tayari kuwa mgombea mwenza na badala yake anapendelea kumuunga mkono Ruto, ambaye inadaiwa tayari alimuahidi kumuunga mkono mwaka 2032. Kabla ya hapo, baada ya uchaguzi wa 2027, Kalonzo anadaiwa kuahidiwa nafasi ya kupendekeza Mawaziri (CSs) watano na Makatibu Wakuu (PSs) 13. Madai hayo pia yanasema kuwa Kalonzo ameagizwa kuendelea kujionyesha kama...
Katika siku za hivi karibuni, baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, kuzungumzia suala la Katiba Mpya, kumekuwa na usambazaji wa picha zenye maandishi (graphics) kwenye mitandao ya kijamii zikimdai Benson Bagonza amesema: "Nchimbi ni CCM anaongelea akiwa mbele ya sufuria ya nyama, kwamba tupambanie chakula. Jiuzulu tukuamini." Ufuatiliaji wa taarifa hii umebaini kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa Askofu Dkt. Benson Bagonza aliwahi kutoa kauli hiyo katika mahojiano yoyote ya hivi karibuni au kupitia majukwaa yake rasmi. Badala yake, mahojiano yake ya karibu zaidi yalifanyika kupitia Radio Sauti FM, ambapo alijadili kauli ya Makamu wa Rais kuhusu Katiba Mpya. Katika mahojiano hayo, Bagonza...
The International Monetary Fund (IMF) has retracted a previous statement claiming that Special Drawing Rights (SDRs) amounting to $443.9 million had been allocated to Tanzania. The communication, originally said to be dated July 10, was officially withdrawn by the IMF. Officials confirmed there are currently no plans for an alternative announcement regarding this disbursement or any new allocation for Tanzania. This development comes amid global scrutiny over financial disbursements to developing nations, as the IMF aims to maintain transparency and accountability in its fiscal operations. Source: Devdiscourse For Swahili viewers. IMF yaondoa taarifa kuhusu mkopo wa dola milioni 443.9 kwa Tanzania. Shirika la Fedha la Kimataifa...
Kumekuwepo na graphic inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, alisema:"Usitegemee katiba mpya sasa hivi. Watanzania tunatakiwa tujikite katika kujenga nchi yetu." Katika ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni, ikiwemo hotuba, mahojiano na taarifa rasmi zinazopatikana hadharani, hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa Jakaya Kikwete aliwahi kutoa kauli hiyo. Sambamba na hilo graphic hiyo potoshi imeambatana na ujumbe ufuato kikwete ukiona mtu anazungumzia katiba mpya chunguza akili zake haziko sawa Tanzania nchi ya amani Aidha, hakuna taarifa rasmi, rekodi za vyombo vya habari, wala hotuba zinazomnukuu Kikwete akisema maneno...
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la usambazaji wa nukuu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zinazodaiwa kutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Mojawapo ya nukuu hizo, iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, inamdai Rais Samia amesema: "Natamani muda wangu uishe." Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kupitia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni umebaini kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Rais Samia aliwahi kutoa kauli hiyo, iwe katika hotuba, mahojiano, taarifa rasmi au kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Aidha, ukaguzi wa hotuba na taarifa rasmi zinazochapishwa kupitia kurasa za mawasiliano za Ikulu ya Tanzania haukubaini sehemu yoyote ambayo Rais Samia amesema...
SANAMU YA DHAHABU YA RAIS TRUMP KUWEKWA IRAN KWA HESHIMA YAKE! . Wafuasi sugu wa rais trump wanapendekeza sanamu ya dhahabu ya Trump iwekwe mjini Tehran siku chache baada ya "kulikomboa" taifa hilo kutoka kwa utawala wa Kiislamu, ikiwa ni ishara ya amani mpya kati ya Washington na Iran. #MAGA HARDLINERS propose a GOLDEN STATUE of Trump be placed in Tehran days after “liberating” the country from the Islamic regime, as a symbol of renewed peace between Washington and Iran.
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, hususan Facebook, zikidai kuwa Ridhiwani Jakaya Kikwete ametangaza kuwa atagombea uraisi na kuwatumikia watanzanai mwaka 2030. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya taarifa, umebaini kuwa madai hayo ni ya kupotosha. Hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa Ridhiwani Kikwete amewahi kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2030 au kusema kuwa atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi nchini Tanzania, uchaguzi mkuu ulifanyika Oktoba 2025, na uchaguzi mkuu unaofuata unatarajiwa kufanyika mwaka 2030. Hata hivyo, mchakato rasmi wa kuwapata viongozi wanaogombea nyadhifa mbalimbali hutangazwa na INEC...
Ikiwa ni siku chache tangu chombo cha habari cha kimataifa cha BBC News kuchapisha makala iliyomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, zimeendelea kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa kauli ya kutaka BBC Swahili ifungiwe kufanya kazi nchini Tanzania. Chapisho hilo, ambalo limesambazwa kupitia Facebook, linaambatana na nukuu isemayo: "Baada ya BBC Swahili kuchapisha video yenye habari ya Tundu Lissu kuhoji demokrasia ya Tanzania, Kikwete atoa tamko kuu kwa TCRA kuifungia BBC Swahili." Hata hivyo, uchunguzi wa taarifa mbalimbali za umma, ikiwemo hotuba, mahojiano na taarifa rasmi zilizochapishwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, haukubaini...
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na machapisho mbalimbali yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mojawapo ya machapisho hayo yanadai kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema, amesema kuwa kwa sasa anaonekana kama msaliti ndani ya chama. Chapisho hilo, lililosambazwa kupitia Facebook, limenukuu kauli inayosema:"Asante Lema, usikubali kuchafuka kizembe wakati ukweli wa jambo unao wewe mwenyewe! Sema ukweli wote wa ufisadi wa Makamu Mwenyekiti Heche bila kuogopa, umma uko pamoja na wewe." je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo ambalo limeonekana kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku klikiwa na graphic ya chombo cha habari cha Jambo Tv ?
Back
Top Bottom