JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kumekuwepo Picha inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ikimuonesha raia wa Afrika Kusini akichoma mahindi imezua mjadala mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mitandao hiyo. Katika machapisho mbalimbali yanayosambazwa mtandaoni, inadaiwa kuwa raia huyo wa Afrika Kusini amechukua kazi ambayo hapo awali ilikuwa ikifanywa na raia wa Zimbabwe. Hata hivyo, je, madai hayo yana ukweli wowote? Uhalisia wa picha hiyo inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ni upi? Picha hiyo imechapishwa hapa, hapa hapa,
BREAKING NEWS: WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN, ABBAS ARAGHCHI YADAIWA AMEUAWA KWENYE SHAMBULIO LA USIKU HUU LA JESHI LA MAREKANI IRAN - Hata hivyo taarifa hizi bado hazijakuwa na uthibitisho US STRIKES IRAN; REPORTS OF FOREIGN MINISTER'S DEATH Severe tension in the Middle East. According to reports, Iranian Foreign Minister Abbas Araghchi was killed instantly in a massive US military strike. This incident occurred just hours after Araghchi issued a direct threat to the US.
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kufanya ziara ya takribani siku tatu nchini Urusi, kumeendelea kusambaa taarifa zinazoeleza kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sasa linashika nafasi ya 15 au 20 barani Afrika na kwamba halipo miongoni mwa majeshi 100 bora duniani kwa mujibu wa viwango mbalimbali vya tathmini ya kijeshi. JWTZ linatajwa kuwa na uwezo thabiti wa kiulinzi na nidhamu ya hali ya juu. Aidha, jeshi hilo linajulikana kwa mchango wake katika operesheni za kulinda amani katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na uwezo wake wa kukabiliana na vitisho vya kiusalama vya ndani na vya mipakani. katika kile ambacho kipo chapisho hilo...
Picha ambayo baadhi ya watu wanadai kuwa inamuonyesha raisi wa Urusi Vladimir Putin akitoa mafunzo kwa wapigania uhuru kusini mwa Afrika ilisambaa na kutumiwa na baadhi ya watu kuhalalisha kuwa nchi za kiafrika zinapaswa kuunga mkono Urusi katika vita vya Ukraine. Picha hiyo ilisambazwa sana mtandaoni baada ya kuchapiswa katika blogu za Zibwabwe mwishoni mwa mwaka 2018, machapisho hayo yalidai yanamuonyesha Putin katika mafunzo ya kijeshi ya Tanzania kwaajili ya harakati za kupigania uhuru katika nchi za Afrika mwaka 1973.
SINEMA INAENDELEA : Mwanaharakati Maria Sarungi, Hilda Newtown na Twaha, walivyokutwa kwenye kikao cha siri huko Nairobi cha kutengeneza sinema ya kupotea kwa kijana msaidizi wa Tundu Lissu ambaye hafahamiki hata na familia ya Tundu Lissu. CHADEMA wala waje na kitu kingine ila hili la kujiteka, ni sinema kama sinema nyingine na Watanzania washazishtukia.
Serikali ya Cambodia imetoa tangazo linalowaagiza raia wote wa Afrika, wakiwemo kutoka Kenya, Ghana, Cameroon na Uganda kuondoka nchini humo kabla ya Mei 31, 2026, la sivyo watakamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za uhamiaji. Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Idara Kuu ya Uhamiaji, mamlaka zilisema kuwa msamaha uliokuwa umetolewa awali kwa Waafrika utaisha rasmi mwishoni mwa Mei. Taarifa hiyo imeeleza kuwa wageni wote walioathirika ambao wamemaliza kulipa faini zao za uhamiaji wanapaswa kuondoka Cambodia kabla au ifikapo Mei 31, 2026. “ Juni 1, 2026, raia yeyote wa kigeni atakayekutwa akiwa nchini Cambodia atakamatwa iwe uwanja wa ndege au eneo lolote,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo. Kwa mujibu wa agizo hilo...
Kumekuwepo na chapisho ambalo linasambazwa kwenye mtandao wa Instagram likidai kuwaonyesha baadhi ya raia wa Kenya wakiwapokea wageni wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Katika chapisho hilo imeomekana kuwa na jumbe ufuatao” Marekani itaipatia Kenya USD milioni 13.5 [TZS bilioni 35.5] kwa ajili ya kujenga karantini ya kuwaweka raia wa Marekani wanaoshukiwa kuwa na maambuzi ya virusi vya Ebola. Marekani imesema kipaumbele chao ni kulinda afya na usalama wa raia wake, kwa kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini humo. Je ?ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ?
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook likidai kuwa aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama, amekamatwa baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kutoa amri hiyo kufuatia kile kinachoendelea Mashariki ya Kati. Katika chapisho hilo linalosambaa, maneno yafuatayo yameonekana kuandikwa:“Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Marekani, wakati Trump anaandika ujumbe huo tayari Obama alikuwa ameshakamatwa. Inaelezwa kuwa baada ya Donald Trump kufanya ziara nchini China, alirejea Marekani akiwa tofauti kabisa. Msemaji mkuu wa Trump amesema kuwa rais huyo alikwenda China kujua msimamo wa taifa hilo kuhusu usalama wa dunia na mustakabali wa amani duniani. Uhalisia Hata...
Kumekuwepo na chapisho linasambazwa mitandaoni huku likiambatana na picha ambayo inamuonesha paul makonda likinukuu kuwa vyama vya siasa vitabaki kama vilivyo, hakuna chama kitakachofutwa. Lakini ni vyema kutambua kuwa chama kinachoongoza nchi ndicho kinachoamua kupanga utaratibu wa mifumo yote ya taifa ili kutimiza ahadi zake kwa wananchi. katika chapisho hilo limedai kuwa mpango wa serikali ya chama tawala ni kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na kadi ya CCM ifikapo mwaka 2030, ili aweze kupata huduma za msingi za serikali. Bila kadi hiyo, mtu hawezi kupata leseni, cheti, barua ya mwenyekiti, hata pasipoti. vilevile katika chapisho ambalo linasamabzwa na watumiaji wa facebook lina jumbe ufuato "Hakuna chama cha siasa, kitakacho futwa...
Na Dr. Zack, Geita Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mhe. Heche John, amepongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kufungua njia ya maridhiano ya kitaifa na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa taifa. Mhe. Heche alitoa kauli hiyo leo Mei 16, 2026 wakati wa uzinduzi wa Operesheni #KatibaMpya #FreeLissu uliofanyika katika Mji Mdogo wa Katoro, Mkoa wa Geita. Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo, alisema kuwa juhudi za Rais Samia katika kuhimiza maridhiano na mazungumzo ya kitaifa ni hatua muhimu inayopaswa kuungwa mkono na Watanzania wote kwa manufaa ya taifa. “Tunatambua juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia...
Back
Top Bottom