Viongozi wa dini wamekutana na Rais wakatoa ushauri ila TEC kwa utashi wao wakakosa subira wakafanya maamuzi ya kibinafsi yanayotaka kuleta udini na kuligawa taifa.

Nioneshe ni lini viongozi wa dini walikutana na rais kuzungumzia mkataba
 
Kwa kuwa Viongozi wa dini kuu Kwa umoja wao walienda kumuona mh.Rais na wakatoa maoni Yao ,hii ya TEC inatoka wapi? Je Kuna mahala mh.Rais amekataa maoni ya watu?
Mbona mnapenda sana kupotosha? Kwa nini hamtaki kuyaweka kwa usahihi yale ambayo mkuu huyu wa KKKT kayasema mbele ya rais kwenye hiyo sherehe ya kanisa lao? Wapi hata kwenye hiyo video clip Askofu Shoo kasema anaunga mkono mkataba wa uwekezaji wa DP World?

Kwani kwenye hili sakata la bandari zetu ni kwamba wananchi wanapinga uwekezaji? Kinachopingwa ni huo mkataba wa ovyo sana kuliko mikataba ya ovyo yote ambayo nchi yetu ilishawahi kuingia. Askofu Shayo kasema kuwa viongozi wawakilishi wa dini zote nchini (TEC, KKKT, BAKWATA, CCT nk) walienda Ikulu miezi 2 iliyopita, wakaonana na rais kupinga mkataba huo kwa mdomo na maandishi wakitoa maoni yao na mapendekezo ya kipi kifanyike. Askofu Shoo kasema kwamba hadi sasa kwa busara zake rais kakaa kimya. Askofu anaamini yatafanyiwa kazi lakini Askofu kaonya kwamba KKKT itakapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo, haitasita kuikemea serikali. Ikifika hapo serikali isijesema dini zinafanya siasa.

Hivyo ndivyo waraka wa TEC ulivyosema, kwamba maoni na mapendekezo ya viongozi hao wa dini zote yaliyowakilishwa kwa rais miezi 2 iliyopita yamepuuzwa. Hivyo wameamua kusambaza huo waraka kwa wananchi kupitia kwenye ibada za kila jumapili kwa wiki sita. Hii ni sawa na ile hatua ya kuikemea serikali aliyoisema mkuu huyo wa KKKT. Hivyo TEC imepiga hatua moja mbele, tutegemee KKKT muda si mrefu itafanya hivyo hivyo au zaidi yake. CCT na BAKWATA nao wanaweza kufanya hivyo hivyo kama mkataba huo hautaondolewa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Lengo ni kuishinikiza serikali iondoe huo mkataba au ufanyiwe marekebisho makubwa sana.


View: https://youtu.be/qJvAMuLCH3Y
 
😁😁😁 acha mi ncheke kwanza maana hii Nchi bhana unaumia na kufurahi at the same time 🙌
 
Anasubiri mtu ajitokeze kufanya haya aliyosema hapa?

Hajui kwamba hii ni kazi endelevu inayofanyika taratibu kwa kumong'onyoa vipande kidogo kidogo kwa muda mrefu?

Yeye anadhani huo umoja na amani aliyoikuta ilianguka tu yote mara moja toka mahali fulani bila ya kujengewa mazingira ya kuiwezesha kuwepo?

Yeye hajui kwamba katika mambo anayoyafanya leo hii yanabomoa taratibu, na wala hajengi taratibu kuimarisha umoja na amani iliyokuwepo?
 
Limeonya au limekubaliana?
 
Jamani askofu kasema anaunga mkono uwekezaji.

Hajasema uwekezaji gani ila watu mnamlisha maneno.

Pia mapendekezo yao bado hayajafanyiwa kazi.yasipofanyiwa kazi lazima waraka utoke
Wanajitoa akili makusudi hao jamaa.
 
Punguzeni porojo
Hawajaunga mkono mkataba mbovu
Mnadanganya ili iweje
Amesema wanaunga mkono uwekezaji ulio na faida kwa Taifa sio huu uliopo sasa
Wakatoliki wamenyoosha maelezo KKKT wamefunga mjadala. Ujumbe ni ule ule acheni kupotosha
Kwanini makanisa mengine wakialikwa ikulu kunywa chai TEC wananuna?
 
Askofu Shoo ujumbe umemfikia
Asante mtumishi wa Mungu

Eti hakuna mwenye ubavu wa kuligawa Taifa kwani haoni limegawanyika tayari...
Hakuna mwenye msuli wa kuligawa taifa .amiri jeshi mkuu wa majeshi ameshaongea kama unachukia sana kunywa sumu huyo ndio rais mpaka 2030.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…