CHADEMA wasitisha safari kuelekea Katesh-Hanang kuwafariji wahanga wa mafuriko kutokana na vikwazo walivyowekewa
Hili swali kwa machawa wote mbona kila mara mkilala mki amka mkikaa midomoni mwenu chadema chadema mbona vyama vipo vingi kwanini chadema halafu mnatangazia watu chadema imekufa lakini kila siku midomoni mwenu humuishi kuitaja chadema mara hawaendi kuwafarijii wahanga wakienda mnawazuia eti rais anakwenda kwani kuna sheria ipi inayosema rais akienda sehemu fulani mwengine haruhusiwi kwenda ooh wanatafuta kiki wanatafuta kiki kwa nani wakati mnasema wananchi wamekususa kwanini chadema vp act tlp chauma cuf n,k mnasema chadema imekufa lakini mnaiogopa nyinyi wa ajabu sana
 
Nyinyi askofu Ina MAANA hamjui kwamba Leo mh. Rais alikuwa yupo huko Hanang?? Ni kwanini hao CHADEMA wapange ziara Leo kama kweli Wana lengo zuri na sio show off... Wasubiri amiri jeshi mkuu aondoke kwanza halafu nao wataingia wakae Hadi mavuno walitaka.. nyinyi askofu tendeni haki na muwe mnafikiria sawasawa sio Kila saa tu lawama

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
Rais ni nani kiasi kwamba watu wengine wabaguliwe kwa sababu ya Rais.Hivi hayo maridhiano na mapicha makubwa ya kushikana mikono ni nini?Elimu yetu isitupeleke shimoni Tanzania ni moja bila kubagua nani anafaa zaidi ya mwenzie.Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya 1977 Ibara 12 na 13.
 
UBAGUZI KATIKA MAAFA YA MANYARA NI AIBU KWA TAIFA!
View attachment 2835774
Ndugu Watanzania!

Kuna taarifa kuwa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Manyara limemzuia Mhe. Freeman Mbowe kufika eneo la maafa likisingizia kuwa limepata maagizo ya kutoka juu. Sisi Askofu tunaamini kuwa hakuna maagizo yeyote kutoka zaidi ya hofu za wanasiasa wa Manyara. Sisi hatuamini kama Rais Samia au Waziri Mkuu Majaliwa na wao wanaweza kutoa amri hizo.

Sisi Askofu tunatoa wito kwa Waziri mwenye dhamana kutoka kueleza umma nini kimetokea hadi Jeshi la Polisi likazuia Mhe Mbowe kufika Manyara. Mbona jana alikuwepo msibani kwa Askofu Kweka? Je, kwa nini Mbowe azuiwe kuwatembelea hao wahanga wakati wengine ni wafuasi wake? Je, Jeshi la Polisi halijui kama Mbowe ni kiongozi wa kitaifa katika nchi hii? Askofu au Sheikh akitaka kutembelea Manyara atazuiwa? Je, UN wakitaka kwenda huko pia watazuiwa? Taharuki ya nini kwenye maafa?

Hivi ni taifa gani hili ambalo watu hubaguana hata katika maafa kama hayo? Je, serikali iko tayari kupokea misaada ya kutoka nje ya nchi wakati inakataa misaada kutoka kwa wananchi wake wengine kama viongozi wa upinzani?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Dar es Salaam, 7 Desemba 2023; 9:30 alasiri
Ichi hii inaongozwa na wahuni wasiojiamini. Eti Makonda ndiye mshauri wa Samia!
 
Kwa hili nadhani opposition wakiri walipotoka kidogo.

Kiukweli kama wangeenda jana sidhani kama wangezuiwa. Mngeahirisha vyoooote mkafika pale ingewezekana hata Makamu wa Mwenyekiti angefika jana kumuwakilisha Mwenyekiti ( pole Mwenyekiti na misiba Mungu akufariji)

Mkuu wa nchi ni SSH so kuna sehemu tuzingatie security na mengineyo sio kila kitu ni show. Ilitangazwa Mkulu anaenda Dec 7 kwanza then ninyi mkaja na tarehe hiyo hiyo hamuoni kama mmekuwa wachokozi zaidi?

Kuna maudhi kero mapungufu mengi kwa watalawa hayaelezeki. Hata kwenye hili mapungufu meeeengi yamejionyesha but msiegemee kuprove ninyi ni bora kuliko wao..

Tunazungumzia janga kuu tuanzie hapo. Aim ilikuwa ni kwenda kuwasaidia wahanga au kushow off? Hii ni both sides inawahusu..

Mwenyekiti ameelewa na ndio maana ametulia.

Opposition, Hawakupashwa kugeuza janga kama hili iwe mtaji. Mwenyekiti angeenda kesho pia kusingekuwa na shida. Kinana alienda kwani yeye yupo ndani ya utawala so msifananishe kiviiiile. What if alienda kuset security na mengineyo.

Tuache hizi petty petty things..

Tulisema kukosolewa ni pande zote so kama chama mkubali mliteleza kidogo. Don’t dwell kwa hii issue maisha yaendelee.. sio kila jambo ni vita
Kwani kama Rais angetoa pole na kumwita au kumwalika Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania naye atoe pole kwa wahanga tatizo lingekua nini?
 
Siasa zisiingizwe katika majanga makubwa kama haya....

Yawezekena janga kama hili... Likatumika kama mtaji wa kisiasa! Kuelekea 2024/25...(hasa kwa ukanda huo!... Atakako huyo mkuu wa hicho chama).

.... kutafuta sympathy ya wananchi kuwa chadema wanaonewa ... Kumbe wamekiuka itifaki kwa makusudi kabisa!!!
Hivi msiba au majanga vinakuwaga na kadi????
 
Kama ni hivyo Rais anayejua kuwa ni Rais wa Watanzania wote angejua kuwa huu ni msiba wa kitaifa na angekuwa wa kwanza kuwashirikisha upinzani wote kuonesha ni msiba wa Taifa siyo wa CCM! Kwani nchi yetu ingeingia vitani angefanyeje? Watu hawafikiri sana. Mnaingia kwenye siasa kama mahala pa itifaki na mbwembwe tu. Nashangaa. Poleni wananchi.
Pointi hii,hongera sana mkuu.
 
Si ndio wangejupendekeza kwa wananchi kwenye matatizo ili waonekane Bora zaidi kwa kuwahi kutoka watu? Sasa kwenye Kampeni wanaokula Bata hewani na helcopter kwenye maafa hatuzioni si ubinafsi huo?
Uoga utawaponza.
 
UBAGUZI KATIKA MAAFA YA MANYARA NI AIBU KWA TAIFA!
View attachment 2835774
Ndugu Watanzania!

Kuna taarifa kuwa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Manyara limemzuia Mhe. Freeman Mbowe kufika eneo la maafa likisingizia kuwa limepata maagizo ya kutoka juu. Sisi Askofu tunaamini kuwa hakuna maagizo yeyote kutoka zaidi ya hofu za wanasiasa wa Manyara. Sisi hatuamini kama Rais Samia au Waziri Mkuu Majaliwa na wao wanaweza kutoa amri hizo.

Sisi Askofu tunatoa wito kwa Waziri mwenye dhamana kutoka kueleza umma nini kimetokea hadi Jeshi la Polisi likazuia Mhe Mbowe kufika Manyara. Mbona jana alikuwepo msibani kwa Askofu Kweka? Je, kwa nini Mbowe azuiwe kuwatembelea hao wahanga wakati wengine ni wafuasi wake? Je, Jeshi la Polisi halijui kama Mbowe ni kiongozi wa kitaifa katika nchi hii? Askofu au Sheikh akitaka kutembelea Manyara atazuiwa? Je, UN wakitaka kwenda huko pia watazuiwa? Taharuki ya nini kwenye maafa?

Hivi ni taifa gani hili ambalo watu hubaguana hata katika maafa kama hayo? Je, serikali iko tayari kupokea misaada ya kutoka nje ya nchi wakati inakataa misaada kutoka kwa wananchi wake wengine kama viongozi wa upinzani?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Dar es Salaam, 7 Desemba 2023; 9:30 alasiri
Chadema ni upumbavu mtupu kutumia Political kicks za maafa!

Je!
tangu Majanga yametokea huko Hanang ni kwa nini hamkwenda mpaka mumsubiri siku mheshimiwa Rais akiwa anakwenda huko?

Je!
Ilikuwa ni lazima nyinyi Chadema kwenda huko sambamba na ziara ya Rais?
Je!
Viongozi wa Chadema hawana Busara za kufanya maamuzi sahihi?
Mfano....kwani mngeacha kwenda Hanamg leo na mkaenda huko kesho mngekuta hao wagonjwa wameondoka wodini wote?

Chadema mnazidi kupoteza umakini na sifa ya chama mbadala kwa siasa za nchi hii.
JamiiForums-1775739402.jpg
 
Nasikia mwenyekiti wa kudumu wa chadema alilia kwa uchungu mkuu usiovumilika alipozuiwa kuwapa salamu za pole ndugu zetu wa Manyara

CC Erythrocyte
 
Back
Top Bottom