Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Hawa CHADEMA wasitupoteze muda wao waendeleze kususa sisi tule
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani

Bila shaka kuna mwaliko rasmi wa kwenda ku-kickstart reconciliation. Kile kitabu kilichozinduliwa majuzi kimewasilisha kwa wale wenye uwezo wa kusoma between the lines mengi waliyonayo wazee wa nchi hii. Hali siyo shwari tena na baada ya kile kilichotokea uchaitwa uchaguzi wa serikali za mitaa haiwezekani kuendelea kutazama tu huku nchi ikisambaratika.
 
Kuna wakati niliona Mheshimiwa dr Bashiru akimtajia namba ya simu Mheshimiwa mwenyekiti wa Chadema.
Nilibaki najiuliza ni kweli hawa watu walikuwa hawana mawasiliano baina yao au naona vibaya?
Naamini kuwa, kuwa vyama tofauti siyo uadui sasa iweje watu hawa wawili ambao kwa namna moja au nyingine taifa linawategemea wakose kuwa na mawasiliano baina yao kwa muda wote huu waliokaa kwenye uandamizi wa siasa?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] operation Entebbe
Iddi Amin alipokubaliana na watekaji wandege ya air France 1976, ilitumika njia ya majadiliano ya kumlghai ili ajione anaweza kumbe makanda wa IDF walikuwa kwenye rehearsal kwaajili ya kufanya uokozi.

Asomaye na afahamu.
 
Naamini akina Mbowe wameshauriwa kufanya hivyo na mtu mkubwa sana ndani ya chama tawala,na kama ndivyo basi siku si nyingi ombi la wapinzani litatekelezwa.
 
sijaona kama kuna watanzania wame athiriwa au kuumizwa kwa namna yoyote ile hadi kuleta maridhiano, sijaona sababu ya pointi ya maridhiano kwenye taifa lenye umoja na mshikamano kama TZ, chaguzi zote huru na za wazi.hakuna umwagaji wa damu ktk taifa letu.
 
1575901158212.png


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amempongeza Rais John Magufuli kutokana na juhudi mbalimbali anazozifanya katika kuliongoza taifa.

Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mbowe amesema kuna ulazima wa kuwepo maridhiano na mshikamano ili taifa lizidi kusonga mbele.

“Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya uhuru kama udhibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano katika taifa letu, ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia ili tujenge taifa lenye upendo na mshikamano.

“Mheshimiwa rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika na kuumia basi utumie nafasi hii kuliweka taifa katika nafasi ya utengamano,” amesema Mbowe.

Mbali na Mbowe, viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika uwanja huo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ambapo amesema kuna haja ya serikali kuimarisha demokrasia hata wakati tukijiandaa kulekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

"Ninampongeza Rais (Dkt Magufuli) kwa kazi aliyofanya, lakini ninamuomba ajue ana jumuku la kujenga demokrasia katika nchi yetu, hasa tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2020."Amesema Lipumba
 
suala la demokrasia ni jambo la mazungumzo na sio maridhiano
 
Kazi kwenu wafia vyama hawa ndiyo wanasiasa
 
Leo mnamtambua kuwa magufuli ni raisi? Ila kwenye kuapishwa kwake mligomea
Unafikiri nafasi ya Mbowe kuhutubia haikuandaliwa,na Kama iliandaliwa waandaaji hawajui kama wapinzani waligoma kwenda wakati wa kuapishwa Rais Magufuli na hawamtambui? Unafikiri Rais Magufuli hakuwa na taarifa yoyote kuhusu uwepo wa wapinzani wake ?
 
Vipi Mzee Sumayee yeye kasema nini au nae kasema CCM oyee kama Lowassa?
 
Akili kubwa sana... Sherehe zimemezwa na CDM
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
 
.... Mbowe kaongea maneno machache mno lakini upande wa pili utadhani hazina gani sijui imevumbuliwa. Mbona alichoongea Mbowe ndio umekuwa ujumbe wake kila mara? Au kwa kuwa kaonekana jukwaa kuu? Sijasikia tusi wala mpasho ukitoka kinywani mwake kama wale wengine; au ndio sababu ya "furaha kuu"? "Sema neno moja tu ..."
 
kitendo cha viongozi wa vyama mbalimbali kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Taifa letu hicho tu ni kielelezo dhahiri za Umoja na mshikamano kwa Taifa letu.
Hongera nyingi kwa Rais wetu kwa kuwaleta pamoja wapinzani wako.
HAPPY BIRTH DAY TANZANIA.58 YRS
 
Back
Top Bottom