Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Nyani Ngabu,

Yaani kwa mawazo yako mpaka tufike kwenye Rwanda au Kenya unachosema hapa ni mpaka watu wengi wafe kwanza👆. Kitu ambacho haki make sense je unajua ni vitu vingapi hao wapinzani viongozi wamezuia. Vilevile kuna tatizo gani kufanya?
 
Nimemsikiliza Mh.Mbowe kwa makini sana leo wakati aliporibishwa na Rais Magufuli kutoa salamu za uhuru

Nilimsikiliza zaidi Mbowe Kwasababu chama anachoongoza kimekuwa kikilamikia kuwa demekrosia haikidhi viwango

Kwa kauli yake Mh.Mbowe amemwomba Rais Magufuli Kuitisha MARIDHIANO ya kitaifa

Nilishtuka sana Mh Mbowe alipotamka hili neno
Kwa tafsri ni kwamba Mh.Mbowe alitaka kuaminisha Umma kwamba Taifa letu limegawanyika Mimi binafsi sikupenda kwa kweli ile kauli

Tanzania haijawahi kufikia kiwango cha kuitisha maridhiano ya kitaifa

Nadhani Mbowe alikuwa anamaanisha maridhiano ya wanasiasa,
Wanasiasa wao inawezekana kuna vitu walizoea kupata ila sasa hawapati angesema hivyo tungemuelewa

Ila Tanzania hatupo kwenye mstari wa kuhitaji maridhiano ya kitaifa Kwani Tanzania Amani imetawala

Ila nimeangalia kauli ya Mbowe kuhusu maridhiano kama njia ya kutaka kutengenezea Watu ulaji

Mbowe ni mfanyabiashara ana jicho kali la kibiashara anajua ikiundwa Tume ya maridhiano chama chake kitaingiza pesa ya kutosha

Miaka 58 ya Uhuru Tanzania ni shwari kabisa
 
Wewe lazima usielewe hata sikushangai, mleta mada anataka mpaka yatokee majanga zaidi ndio tutafute maridhiano, sasa hivi hizi kesi wanazobambikiwa wapinzani na kuharibiwa mali zao ( Mbowe) kwake ni vitu vidogo tu, hajui kama vinachochea chuki kati ya kundi moja na jingine kwenye jamii, yeye anataka tuendelee kuwakumbusha tu huku mkizidi kuumiza wengine kila kukicha!
Unaelewa maana ya maridhiano lakini?!
 
Nyani Ngabu

Unakosea!

Wewe umeleta hoja, ni mtazamo wako, kwa maana ndivyo unavyoona...

Achana na kujibu hoja kwa jazba. Kwa kujibu kwa mtindo huu, unaonesha hata ulichokiandika hapa ni umbea tu....

Kama unaona hoja ya mchangiaji fulani ni ya kipuuzi na ina kejeli, ignore it kwa sababu kwenye baraza lolote huwezi kukosa watu wa aina hii...

Jibu wachangiaji wanaopinga hoja yako kwa hoja, wasiokuwa na hoja ignore them....

Binafsi sikubaliani na wewe, RECONCILIATION ni muhimu. Huna haja ya kusubiri mpaka tufikie hatua kama ya Rwanda ama Kenya ama SA ndiyo tuamke ndo tuone kuna ulazima wa kukaa chini na kuyazungumza....

Kinga ni bora kuliko Tiba!!
 
Yaani kwa mawazo yako mpaka tufike kwenye Rwanda au Kenya unachosema hapa ni mpaka watu wengi wafe kwanza👆. Kitu ambacho haki make sense je unajua ni vitu vingapi hao wapinzani viongozi wamezuia. Vilevile kuna tatizo gani kufanya?

Hatuhitaji maridhiano kwa sababu hatuna sababu ya kufanya hivyo.

Tunachokihitaji ili kuboresha hali iliyopo nimekielezea.

Soma ukielewe. Ukisoma na kuona huelewi, niulize. Nitakufafanulia.
 
Mimi Nadhani M.Mh.Mbowe aliwasilisha salamu akiwa na jazba mno akasahau hata kufikisha ujumbe aliokusudia
 
Mbowe atimue washauri wote Ninachoona wao Ndio wanamshauri vibaya
 
Hata kama tunampenda Mbowe lkn ukweli usemwe
Taifa halijafikia kwenye hatua ya Kufanyika Maridhiano ya Kitaifa
Jiandae kuoga matusi maana umemgusa mwenyekiti wetu
Mwamba tuvushe
Tano tena.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anachomaanisha Mbowe ni maridhiano ya Kidemokrasia, Demokrasia yetu iko mahututi.

Watu kupita bila kupigwa na wengine kuondolewa kwa vigezo vya kipumbavu sio uhai wa Taifa.

Wenyeviti wengi sana huku mitaani wanazidi kukataliwa.
 
Wewe lazima usielewe hata sikushangai, mleta mada anataka mpaka yatokee majanga zaidi ndio tutafute maridhiano, sasa hivi hizi kesi wanazobambikiwa wapinzani na kuharibiwa mali zao ( Mbowe) kwake ni vitu vidogo tu, hajui kama vinachochea chuki kati ya kundi moja na jingine kwenye jamii, yeye anataka tuendelee kuwakumbusha tu huku mkizidi kuumiza wengine kila kukicha!
Kweli umenena tujikumbushe Mzee Karume kilicho muondoa ni chuki zidi ya mtu mmoja aliye umizwa na alicho tendewa Mzazi wake tusiende keze chuki binafsi mtu kwenda kuharibu mali ya mtu kisa siasa
 
Unakosea!

Wewe umeleta hoja, ni mtazamo wako, kwa maana ndivyo unavyoona...

Achana na kujibu hoja kwa jazba. Kwa kujibu kwa mtindo huu, unaonesha hata ulichokiandika hapa ni umbea tu....

Kama unaona hoja ya mchangiaji fulani ni ya kipuuzi na ina kejeli, ignore it kwa sababu kwenye baraza lolote huwezi kukosa watu wa aina hii...

Jibu wachangiaji wanaopinga hoja yako kwa hoja, wasiokuwa na hoja ignore them....

Binafsi sikubaliani na wewe, RECONCILIATION ni muhimu. Huna haja ya kusubiri mpaka tufikie hatua kama ya Rwanda ama Kenya ama SA ndiyo tuamke ndo tuone kuna ulazima wa kukaa chini na kuyazungumza....

Kinga ni bora kuliko Tiba!!
Kwa kweli hapa neno 'maridhiano' halijatendewa haki. Mbowe labda aseme amekosa neno sahihi...
 
Nyani Ngabu unataka kila mtu akubali mawazo yako sio?!, kuita wengine wanyama coz wanakupinga sio ustaarabu, you are selfish arrogant!
 
Back
Top Bottom