Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Maadhimisho ya jana yalikuwa na sura ya kitaifa iliyozoeleka. Pongezi kwa serikali ya awamu ya tano kwahili
 
Kwa maneno machache tu Mbowe speech yake ndiyo kila mtu anaiongelea kwenye kila mtandao, groups na hata vijiweni.

Mbowe pamoja na mapungufu ana kipaji cha kuongea kuliko wanasiasa wengine.

Lakini vilevile amekuwa presidential na ana heshimika na Watanzania huwezi kuzuia talent.

Tujiulize kama nchi kwanini watu wamevutiwa na speech yake kiasi hiki
 
Nyie kila analoongea Mbowe lazima mpige vigelegele, wanaitwaga nyumbuuuu. Anaongelea demokrasia huku ndani ya chama chake ikiwa haimo, anaongelea maridhiano huku ndani ya chama chake yakiwa hamna. Na huo ndo mjadala unaoongelewa jinsi gani alivyomnafiki. Hujawahi kujiuliza kuwa kwa nn mabaya ya mtu yanavuma sana kuliko mazuri yake? Hutakaaa uelewe, endelea kushangalia kufunika
 
Kwa maneno machache tu Mbowe speech yake ndiyo kila mtu anaiongelea kwenye kila mtandao, groups na hata vijiweni. Mbowe pamoja na mapungufu ana kipaji cha kuongea kuliko wanasiasa wengine. Lakini vilevile amekuwa presidential na ana heshimika na Watanzania huwezi kuzuia talent. Tujiulize kama nchi kwanini watu wamevutiwa na speech yake kiasi hiki
Haya ni mahaba yako
 
Sihitaji kutukanana na wewe wala mtu yeyote for that matter. Nimeandika nachoamini na nina haki ya kufanya hivyo. Halafu kuandamana sio political strategy pekee na kwa kweli mimi sijazungumzia strategies, nimetaja strategists.

Sijawahi kumfatilia huyo Mange, simdharau lakini sio mtu wa mimi kumfatilia! Ni nani? Ni mtu wa caliber gani? Napenda kufuatilia wanasiasa makini, local and international sio Mange, whoever he or she is! Mange? Seriously!
Humu ndani hatulazimiki kuandika vitu vinavyofanana. Hili ni jukwaa huru na nitaandika kile ninachoamini bila kujali nitaitwa ' keyboard hero' or 'keyboard warrior'. Sheesh!!!
Umeandika vema sana
 
Wachawi pekee hawapendi maridhiano, Mbowe amefanya kitu cha maana kwa upande wangu, raisi atajua yeye akubali au akatae. Hata afanye maendeleo kiasi gani akiminya demokrasia na kuonea walio na itikadi tofauti itamsumbua mpaka mauti, na historia itamhukumu.
Umeandika vema sana
 
Hotuba fupi yenye ujumbe mhimu sana.

Natumaini walioisikia wataichukulia kwa uzito iliyoubeba.

Mwenye kupuuza haya, hakika halitakii taifa hili mema.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Maridhiano ni lazima na muhimu. Chama changu cha CCM, kikigomea usuluhisho, tutapata pigo kubwa kisiasa na tutakosa sifa.

Inajulikana kuwa CDM wanahitaji kujikosha na makosa yao ya kisiasa, wanahitaji wakati wa kupumua na kujitafakari.

Wapewe hiyo nafasi ni haki yao, upinzani madhubuti na wenye muelekeo ni tija kwa chama tawala.
Wenzako hawalioni.
 
Mbowe leo nimetangaza rasmi kutokukukejeli haijalishi ulifanya maovu gani huko nyuma lakini kwa ujasiri uliouonyesha leo nimejisikia amani sana ubarikiwe sana Mwenyekiti.

Binadamu tunabadilika hatuko static tuko dynamic, binafsi nilikuwa miongoni mwa watu waliokuchukia sana natangaza kuanzia leo nitakuheshimu daima umeonyesha uungwana kutii mamlaka zilizowekwa na Mungu umetumia maneno ya hekima na busara sana.

Keep it up.
MAAMUZI YAKE SIO YA MKUTANO MKUU WA CHADEMA.MKUTANO MKUU WA CHADEMA NDIO WENYE MAMLAKA MAKUU KWENYE MAMBO MAZITO YA CHAMA
 
Ujumbe mzito sana wanajitangaza wacha MUNGU kutwa kucha kudhulumu haki za watu.
Uongo ni uovu kutwa kucha pesa za mkopo wanazibatiza ati pesa zilizo tayari zimetoka kwa Wananchi.
Nguvu inayotumika kukandamiza chadema ni kubwa mno. Mbowe alitakiwa atoe maneno makali kidogo
 
Watu wanaotaka kukaa pamoja kujenga nchi yao wanakukera nini we mrundi!!!? Tanzania tumezoea kuzungumza pale tunapohitilafiana kama umetumwa kafie mbele huko kwenu,,,ina maana huoni ufa wa kisiasa uliopo???
Nadhani naweza ku'guess' ni nani unamwelekezea ujumbe huu, hata kama hukumtaja, wala mum'quote' kwenye bandiko lako.

Basi ngoja nikwambie jambo: Jamaa anatafuta/lazimisha 'attention' iwe kwake. Wewe huoni anavuta kila mtu amwangalie yeye?

Kuna watu wa aina hiyo, na huyo, ni 'typical' ya watu hao. Wewe tafuta humu JF michango anayohusika yeye.
Anatafuta awe 'center' ya 'attention', badala ya mjadala uliowekwa ujadiliwe.

Watu wa namna hiyo mimi sina muda nao.
Natumaini utanielewa niliyoandika hapa. Kama nimekosea uliyemlenga kwa bandiko lako hili, naomba kumradhi.
 
Kwa maneno machache tu Mbowe speech yake ndiyo kila mtu anaiongelea kwenye kila mtandao, groups na hata vijiweni.

Mbowe pamoja na mapungufu ana kipaji cha kuongea kuliko wanasiasa wengine.

Lakini vilevile amekuwa presidential na ana heshimika na Watanzania huwezi kuzuia talent.

Tujiulize kama nchi kwanini watu wamevutiwa na speech yake kiasi hiki
Wanaompinga hutumia chuki za kutokukubalika kwao ila Mbowe level ya juu kuliko wanaompinga hata wao nafsi zao zinawashuhudia. Speech yake fupi imekuwa na mvuto sana kwa wengi. Hata humu toka Jana sijaona Uzi unaomhusu kiongozi mwingine aliyekuwepo Mwanza utadhani Jana ni mbowe pekee ndo alihutubia. Big up Chairman.
 
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.

CHADEMA hakuna kitu
kinacho nishangaza Mbowe kaongea kwa dakika moja lakini mitandao yote inaongea kuhusu Mbowe na chadema hakuna hata anaye sema kuhusu hatuba za wanasiasa wengine akiwemo Magufuli. utafikiri Mbowe ndiye raisi.
 
Back
Top Bottom