Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Huwezi kutaka maridhiano na mtu anaye kuchukulia poa,anaye kuzidi nguvu na kila kitu na anajua hamna kitu utamfanya.

Wanaridhiana watu wanaokaribiana nguvu,kwamba usiporidhia nna uwezo wa kuzingua lkn mtu anajua hamna kitu CDM itafanya unadhani amesikiliza chochote.
Tatizo wanadharau upinzani kwa kuwa hakuna dalili za Shari kutokea na Watanzania siyo watu wa Shari.

Binafsi naamini kuwa Wapinzani Wana Wafuasi wengi tu wa kutosha ila tu bado hawajawa stretched to the breaking point ndiyo maana CCM wanapata kiburi mpaka akina Kabudi wanakwenda kupreach nchi jirani Amani wakiamini hapa ni shwari na itakuwa hivyo milele.

Prevention is better than cure. Why wait mpaka hali imekuwa mbaya ndiyo ukae kwenye round table? Hizo chaguzi zinazoibiwa na kina Jafo na Jecha kuna siku watu hawatakubali.

Kwa mtizamo wangu kwa sasa anayependwa ni Magufuli tu na siyo CCM kama wanavyotaka watu waamini.
 
Ndugu zangu, kama kuna mwanasiasa anajaribu kupinga maridhiano aliyoomba Mbowe, atangulie msituni ili tumpuuze Mbowe.
 
Uzuri wa Mbowe anajua sana kujieleza ila hayakuwa mambo makubwa sana yanayokuzwa na mitandao ya kijamii.
 
Katika wanasiasa wote tulionao Tanzania sikutegemea watatu hawa kujitoa ufahamu kwa kiwango hiki.

Kiukweli vyama vya upinzani nchini ndivyo vilivyokosa demokrasia kabisa na vinapaswa kuiiga CCM. Hebu waangalie Mbowe, Prof Lipumba, Cheyo, Mbatia, Mrema, Rungwe na hata Dovutwa aliyetumbuliwa juzikati hawa jamaa wako uongozini kidemokrasia kweli?

Muangalie Sugu na wafuasi wake pale Mbeya wanavyomsumbua Ph.D Tulia asigombee ubunge kana kwamba hilo jimbo ni mali binafsi ya Mbilinyi!

Wapinzani tekelezeni demokrasia ili wananchi wawapime katika mizani sawa na CCM acheni kulialia.....unailalamikia CCM wakati wewe chama chako hata kufanya uchaguzi tu mnataka kutoana roho?

Maendeleo hayana vyama!
 
Chumia tumbo utamjua tu, yaani unaishi kwa kutegemea umbea
Hizi zingine ni mbwembwe tu dogo.

Ukweli ni kuwa kishindo cha awamu ya tano maji yake hamuwezi kuogelea kamwe.

Viva Magufuli
 
Hakika mkuu ingawa kuna watu wanafaidi sana hali hii ya mtafaruku kati ya ccm na vyama vya upinzani.

Wao wanapata mkate wao wa kila siku kwa kutumia migogoro ya vyama vya siasa.
Safi, tuanze na hivi vikesi kesi vya kisiasa tuvifutilite mbali.

Hata kuundwaji wa Serikali ya umoja wa kitaifa yawezekana come 2020, Katiba ni mali yetu na si biblia ama msahafu...it can be edited, kama kweli tuna nia ya dhati why not.

Tanzania ni mali ya watanzania wote, si mali ya chama cha siasa chochote.
 
Kudadadeeeki sasa vijakazi wa lumumba mtakufa kwa njaa maana mlikuwa mnatumia migogoro ya vyama vya siasa na CCM kujipatia ridhiki
 
Kesi yao imekaa vibaya,kuna kufungwa,ooh!,wameenda kumuangukia
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
 
wengine walidhani asingepewa hata nafasi ya kuzungumza pale!
 
Mpaka sasa zitto kwenye kudai demokrasia kafanya lipi la maana. Je wakisusia uchaguzi kipi kinafwata.
 
Mbowe yuko vizuri sana, yale maneno machache aliyoongea unaweza ombea mkopo world bank.

The guy is very convicive, talented and gifted leader. Most of all he is very very strong, inahitaji kuwa mwanaume kamili kuongea maneno yale mbele ya Raisi.

The guy is extremely confident.
 
Ujumbe wake ulikuwa wa kichungaji/mahubiri ya kusisitiza amani. "Nawapeni amani yangu..."
Neno amani japo la kawaida lina ujumbe mzito.
Tuache chuki binafsi na ushabiki tuangalie ujumbe na sio mti.
 
Ndugu zangu, kama kuna mwanasiasa anajaribu kupinga maridhiano aliyoomba Mbowe, atangulie msituni ili tumpuuze Mbowe.

hivi wanaosema nchi hii haihitaji MARIDHIANO YA KITAIFA wanaakili kweli?
Juzi tumeona mwanzo mbaya sana was kushindwa kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji wao wanaona ni jambo jema hilo kwa nchi?

Hawaoni tayari huko vijijini tayari mifarakano imeanza kutokea kwa waliopachikwa kurudisha vyeo hivyo kwa vile wameshindwa kifanya kazi? Nchi zingine kususia uchaguzi ni ishara ya vita ya ndani kwa ndani inanyemelea Ila kwa sababu hapa tunadanganywa "kuna amani" basi nasi tunadanganyika.

Maridhiano ni lazima na ni sasa sio wakati mwingine tena.
 
Wanaompinga hutumia chuki za kutokukubalika kwao ila Mbowe level ya juu kuliko wanaompinga hata wao nafsi zao zinawashuhudia. Speech yake fupi imekuwa na mvuto sana kwa wengi. Hata humu toka Jana sijaona Uzi unaomhusu kiongozi mwingine aliyekuwepo Mwanza utadhani Jana ni mbowe pekee ndo alihutubia. Big up Chairman.
Nami nashangaa, hotuba ya dakika 1.06 ndiyo imekuwa hotuba ya maadhimisho ya 58 ya Uhuru maana ndio inayojadiliwa nchi nzima.
Watu wamesahau hadi msamaha mkubwa wa wafungwa?
Basi kumkebehi Mbowe ni dalili za kumshindwa. Kweli Mbowe ni jabali la siasa kwa nyakati hizi
 
Back
Top Bottom