Haji Manara popote ulipo au ukisaidiwa na Yanga SC Wenzako mkinijibu haya Maswali yangu Muhimu nitashukuru

Haji Manara popote ulipo au ukisaidiwa na Yanga SC Wenzako mkinijibu haya Maswali yangu Muhimu nitashukuru

" Wenye Akili Yanga SC nzima ni Watu Wawili tu Rais Mstaafu Kikwete na Baba yangu Mzazi Mzee Manara waliobakia wote hawana," alisema Haji Manara alipokuwa akihojiwa na EFM Radio Kipindi cha Sports Headquarters mwaka 2021...
Huyu jamaa yeye hakubaligi kushindwa kabisa, na amejitengenezea dhana ya kuwa eti anaogopwa na TFF ipo chini yake, hiv hajui kama anaonewa tu huruma!! Tumuombeeni sana...
 
Kama Rais Samia, Rais Mwinyi, Rais Mstaafu Kikwete wapo humu na ni 'Followers' wangu GENTAMYCINE Mtu Mmoja tu mwepesi Haji Manara ataacha kuwepo?

Kwa Taarifa yako tu ni kwamba 99% ya Mada zangu hapa JamiiForums nikiwa namuandikia Haji Manara ( hasa Kumsema ) huwa anafikishiwa na Chawa Wake na kupitia Kwako nikuibie Siri kuwa Haji Manara anajua kuwa Mimi GENTAMYCINE na hii ID ni Adui yake Mkubwa Mchambuzi Mahiri wa Soka wa EFM Jemedari Said Kazumari wakati hata siyo Kweli.

MImi ni Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura ( GENTAMYCINE) na siyo Jemedari Said Kazumari kama Haji Manara anavyodai na mara kwa mara huwa anadai hivyo.
Naona nawe pia umeanza kuota mapembe after kukula ya mbuzi. Unathubutuje kusema hivyo kweli? Mods toeni huyu mtu haraka mpelekeni hata huko Ukraine akaokote machumachuma ya Mmarekani
 
Manara ni original Brand iliyotoka kwa Familia ya mchezaji wa zamani wa Yanga baba Mzazi wa haji Manara ndio ikatokea Simba wakawa na tamaa na kufuata hii Manara Brand sasa kwa kuwa Simba walitumia dawa iliyo expire ya Gentamisene basi wameshindwa Manara akarudisha Brand kwa Yanga

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Namba 7

Haji anadai kua hajapewa nakala ya hukumu yake japo ameidai zaidi ya mara 2

Anataka nakala ya hukumu yake ili akate rufaa,

So,kwa vile hajapewa nakala ya hukumu anadai kua hiyo hukumu haitambui,

Hapa wanasheria watatusaidia ili kuliweka hili sawa.
 
Tatizo kubwa ninaliona mimi ni kuwa Manara alidekezwa sana na TFF, vyombo mbali mbali vya habari, watangazaji, viongozi wa vilabu, wawekezaji/wafadhili wa mpira, n.k. aidha kwa kumuogopa au kumuonea huruma kutokana na hali aliyonayo maana akiguswa tu siku zote anakimbilia ulemavu wake. Matokeo yake ndiyo haya ya kuchelea mwana kulia sasa TFF ndio italia. Manara alikuwa na makosa mengi sana tangu akiwa Simba lakini hakuchukuliwa hatua madhubuti kumuadhibu kwa kila kosa matokeo yake sasa amefanya kosa kubwa ameadhibiwa halafu anaona anonewa. Mbaya zaidi badala ya kufuata taratibu na kukata rufaa ili apate haki yake anaitisha "press" wakati siku zote taratibu za kutafuta haki ni kukata rufaa ngazi kwa ngazi.
 
Manara ni original Brand iliyotoka kwa Familia ya mchezaji wa zamani wa Yanga baba Mzazi wa haji Manara ndio ikatokea Simba wakawa na tamaa na kufuata hii Manara Brand sasa kwa kuwa Simba walitumia dawa iliyo expire ya Gentamisene basi wameshindwa Manara akarudisha Brand kwa Yanga

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Haji manara ni maarufu toka anazaliwa,Haji alipozaliwa magazeti yaliandika kuhusu Sunday Manara kupata mtoto,

Nacomment kama mwana JF na sio kwa kushabikia team yeyote au mtu yeyote.
 
Last kicks of a dying horse

Yani TFF na Karia watajua hawajui.
Wamefanya uchafu mwingi sana, sasa muda wao umefika.
 
Haji ni kama mfamaji na huyo injinia ana wahaminisha tu wanayanga wenzangu tuamke yajayo yanatisha au kama vp tuhame ligi tukacheze kombe la mbuz tabata maana mpira wa kitaaluma na ustaarabu umetushnda..huu ni wangu mtazam masela msijenge chuki
 
1. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

2. Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba

3. Waziri 'yupo yupo' Mzee George Huruma Mkuchika

4. Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde

5. Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete

6. Waziri wa TAMISEMI Bashungwa

7. Rtd. CDF Gen. Mabeyo

GENTAMYCINE nalisema hili mapema hivi na kwa nia njema tu kwani tayari kama Kawaida na Maono niliyobarikiwa nayo na Mwenyezi Mungu naona kuna HATARI Kubwa inakuja mbeleni kama Watajwa hawa hawatokaa pembeni ya hizi Jeuri zote za Mfungwa na Mdaiwa Haji Manara.

Msije kulaumu tu sikuwashauri sawa?
Ninaweza kukubali asilimia mia kabsa maana kabla ya kushikwa masikio alikuwa amenywea kabisa leo anakuja na kiburi na jeuri na kwamba wasimshauri akate rufaa mbona iko wazi kwann apige kelele kapewa adhabu yeye sio wiki ya wananchi anajiona yeye ananguvu kuliko yanga na wana yanga wana kubali ujinga
 
Umeandika matapu tapu

1. Haji hakusema hivyo akihojiwa na Efm alisema hivyo akihojiwa na salama.


2. Kuhusu hoja mfu yako kusema Haji kasema Yanga hawana akili alimaanisha Yanga wanaipenda sana timu yao.

Hata mwanaume akimpenda sana mwanamke kupita kiasi anaonekana hana akili.

Bushman kama wewe huwezi kuelewa kiswahili cha watoto wa mjini.

Wasalimie Bunda vijijini
 
Ninaweza kukubali asilimia mia kabsa maana kabla ya kushikwa masikio alikuwa amenywea kabisa leo anakuja na kiburi na jeuri na kwamba wasimshauri akate rufaa mbona iko wazi kwann apige kelele kapewa adhabu yeye sio wiki ya wananchi anajiona yeye ananguvu kuliko yanga na wana yanga wana kubali ujinga
Amesema hajakata rufaa coz mpaka leo hajapewa nakala yake ya hukumu.
 
Rais Karia ni mzaliwa wa Tanga na timu yake ni Coast Union ambayo siku ya tukio ilikuwa inacheza na YANGA ya Manara.
Mwenyekiti wa Bodi ya ligi ndie Mwenyekiti wa Coast Union ya Tanga.
Na pia ukiacha Hao kuwa wapenzi wa Coast Union pia ni wapenzi wa Simba.

Sasa pia hii kamati ya maadili hii inaundwa na viongozi wa juu wa TFF hakuna budi kusoma kuwa ndio hapohapo.

Sasa mfano wake ni kusema kuwa mtoto wangu wagombane na mtoto wa Jaji na kisha mtoto wa Jaji amehumizwa vibaya sana kisha kesi inaperekwa kusikilizwa na Jaji huyohuyo.

Mtu Haoni aibu iliyocheza ni timu yake na hadharani kafungwa hapohapo anaenda kufungua kesi kwenye vyombo ambavyo yeye anasimamia.
Hao viongozi wa TFF wanasimamia Michezo kwa maslahi yao wenyewe na waondoke watuachie TFF yetu

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom