Hans Pope: Manara hataki kusaini mkataba ambao atalipwa milioni 4
Manara anadeka, Manara ni mropokaji, Manara ni mswahili. Ila kwenye suala la Manara kuihujumu Simba siungi mkono asee. Kajamaa kanaipenda Simba!
 
Je, hiyo laki 7 mnayompa ni Mshahara na kasaini mkataba au ni Posho 😕😕😕
 
Kwa muda mrefu Haji amekuwa akijihusisha na GSM kama one of the brand ambassador na pia amekuwa brand ambassador wa wafadhili wa azam. Tatizo ni kwamba kuwa ambassador huko kwingine kunamnyima yeye nafasi ya kutangaza bidhaa za mtu ambaye amewekeza pesa nyingi pale Simba kwa sababu za kimikataba na hao wengine.

Sasa haiingii akilini, muajiriwa wasimba anashindwa kutangaza bidhaa za mdhamini wa Simba, ila anaenda kutangaza bidhaa za madhamini wa Yanga!

Hivi ishawahi kufikiria leo Hasan bumbuli awe na mkataba wa kibiashara na Mo dewji kutangaza bidhaa zake na mashabiki wa yanga wamuangalie tu?

Linapokuja swala la mshahara, Simba wanampa laki Saba huku hao wengine wanampa wakimpa zaidi ya million 5 Sasa unafikiri huyo anayempa million 5 akija kumuomba taarifa za huyu anayetoa laki 7 atakataa?? Ni halali viongozi wa Simba kuwa na mashaka na haji manara.
Tatazo simba bado wachanga kimfumo, mnasafiri ndefu kuifikia Yanga.

Akili zenu mmeziweka kwa Mo, asiposema Mo mnakuwa kama nyumbu,
 
GSM ni wadhamini wa Yanga na wana interest na Yanga, Azam wana products ambazo zinafanana na products za wadhamini wa Simba 'mo energy' , kumbuka simba walisaini mkataba rasmi wa udhamini na products hizo na Simba inavuta mpunga. Huoni conflict of interest hapo? Yaani uwe msemaji wa Nike alafu uwe balozi wa products za Adidas.
Watizii wengi hawajui maana ya conflict of interest ni vizuri manara aende kwa GSM mall kabisa atuachie timu yetu.
 
Hanspope aache unafiki milioni4 pesa gani walau milioni8 tuwe wakweli Simba ya Manara ni Simba tofauti sana, thamini kazi ya Manara, mnaona wivu thamani anayopata huko nje ndio mnajenga hisia za kiutopolo. Manara hata Yanga itamfaa tu maana kaishi ndani ya Yanga maish yake yote.
Ndio aache Simba aende huko wanakompa masilahi makubwa Simba existed since 1935 without him aisee, acheni kumpa huyo bichwa aisee, Tena kipindi team Ina mechi ngumu analeta shombo zake na kujiona mkubwa, Simba imemvumilia naomba imtoe kabisa ahamie huko GSM mfyuuu kweli huyu.
 
Haya yote ni kutokana na matokeo ya tarehe 3

Sababu hii mikataba ajaanza kuwa nayo Jana wala leo ni ya mda sasa siku zote hizo mbona walikua kimya?

Mo ni mwekezaji simba na baadhi ya bidhaa zake zina dhamini jezi ya simba kwa makubaliano yao lakini manara ni mfanyakazi wa simba na haimnyimi haki ya kufanya matangazo ya bidhaa tofauti. Labda no aingie mkataba personal na haji wa kutangaza bidhaa zake

Ng'olo kante ( mtu mbad) yuko Chelsea inayodhaminiwa na Nike but yeye ana mkataba wa kutangaza bidhaa za Adidas lakini sijawahi kusikia Chelsea akikutana na man u wanaodhaminiwa na Adidas eti anavujisha siri.

Hapa kinachotafutwa ni namna ya kumfukuza tu haji
 
Kwanza Mo kamvumilia na kumdekeza sana,nimefatilia hili swala kwa kina na nilikuwa upande wa Haji kumbe Haji ni tatizo na Mo halilifumbia macho kwa muda mrefu sana.Haji asepe akafanye kazi kwa uhuru na gsm kipenzi chake.
 
Back
Top Bottom