Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Hiyo ndio maana ya regime of change??
 
Nahisi haya mashambulizi ya issel tunayo ambiwa yanalenga zaidi MAENEO ambapo vyuma vya Iran vinatokea wakimaliza hapo kazi itakuwa imekwisha.

Japo Iran nampongeza kwa kuonesha kupambana
 
Watu wanafuturu moshi tu huko yaan mpaka wakikohoa unatoka moshi🤣🤣🤣chezea mazayuni ....kuna panya moja hapa ilikua inatamba ohooo music wa kobaz ni balaa wamekutana na mziki mnene wanajamba moshi tu
 
Watu wengi wanaangalia mambo yanayotokea kimataifa wakifikiri ni kuhusu kuondoa madikteta au kupambana na silaha za nyuklia. Lakini ukiangalia kwa makini zaidi, kuna picha kubwa zaidi inayoonekana.

Hebu tuanze na China.

Ukuaji wa uchumi wa China umekuwa wa kasi sana kwa miongo kadhaa. Lakini kuna udhaifu mmoja mkubwa: nishati. China inaagiza zaidi ya 70% ya mafuta yake kutoka nje. Hilo linaifanya kuwa tegemezi kwa nchi chache muhimu sana zinazozalisha mafuta. Na hapo ndipo nafasi ya kimkakati kwa Marekani inaonekana.

Fikiria kuhusu Venezuela na Iran. Hizi ni miongoni mwa nchi zenye akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani. Venezuela inashika nafasi ya kwanza kwa akiba iliyothibitishwa, ikifuatiwa na Saudi Arabia, halafu Iran. Kwa pamoja, zinashikilia takriban 45% ya akiba yote ya mafuta duniani. Hiyo si takwimu ndogo.

Sasa, hoja ni hii: ukiweza kuwa na ushawishi juu ya nchi kama Iran na Venezuela , iwe ni kupitia siasa, vikwazo, au mabadiliko ya uongozi , unaweza kuathiri moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja nani anapata mafuta yao. Na kama China ni mnunuzi mkubwa, basi hilo linakuwa suala la kimkakati sana.

Kwa mfano, suala la Venezuela mara nyingi linaelezewa kwa hoja ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya. Ni kweli, hilo ni tatizo kubwa. Lakini ukiangalia kwa uhalisia, njia kuu ya dawa hizo kuingia Marekani ni kupitia Mexico. Pia kumekuwa na ripoti zinazoonyesha mchango wa China katika usambazaji wa kemikali za kutengeneza fentanyl. Hata hivyo, hatujaona hatua za kijeshi za aina ileile dhidi ya nchi hizo. Hapo ndipo mtu anaanza kujiuliza: je, hii ni kweli kuhusu dawa za kulevya pekee?

Halafu chukulia Iran. Kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia ni jambo la msingi kwa usalama wa dunia. Lakini tayari North Korea ina silaha za nyuklia na inaendelea kuendeleza makombora yake. Marekani haijachukua hatua ya moja kwa moja ya kuondoa utawala huko. Tofauti iko wapi? Moja ya majibu yanayowezekana ni nguvu ya kimkakati ya nishati.

Kwa kuiangalia kwa mtazamo mpana, hatua dhidi ya Iran na Venezuela zinaweza kuwa zaidi ya masuala ya ndani ya nchi hizo. Zinaweza kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kudhibiti mwelekeo wa nishati duniani na kwa njia hiyo, kuweka shinikizo kwa mshindani mkubwa zaidi wa kiuchumi wa Marekani.

Kupambana na dawa za kulevya ni muhimu. Kuzuia tishio la nyuklia ni muhimu pia. Lakini nyuma ya pazia, kuna uwezekano mkubwa kwamba mchezo mkubwa ni kuhusu ushawishi wa nishati na jinsi ushawishi huo unavyoweza kutumika kupunguza nguvu ya China katika muda mrefu.
Na hiki ndio chanzo cha vita na ndiyo maana kabla ya kuvuruga supply ya nishati ya Middle east walivuruga mtandao wa Venezuela na kuzuia mafuta yao
 
😄
😄😄😄

Kwamba wanashindwa kwenda wenyewe Iran wana waambia raia wawasaidie !?
 
🙌🙌😄
 
We nae tumekuchoka...tukitaka kujua huyo anasema uongo nawewe unasema kweli,tupimaje? Kwan unalipwa kiasi kwamba atakuharibia ulaji wako? Acha kila mtu alete habari iwe ya kweli au uongo! Au mtandao huu wa baba yako?
Kill him 😄😄
 
Hoja nzuri, lakini pia US na Israel wamekutana kila mmoja akiwa na goals zake halafu wakajikuta njia ya kupita kufikia hizo goals ni moja, hivyo wanashirikiana. Na pia wakitimiza malengo hayo wote watakuwa katika nafasi nzuri sababu kila mmoja yupo vizuri tokana na ushirikiano wao wa ki uchumi, kijeshi na ki siasa.

Nikiwa na maana ya kwamba Israel akiwa vizuri kwenye nyanja zote, US hawezi hangaika kupoteza rasilimali zake ili kumsaidia.
Israel inataka sana ukiranja wa kikanda mashariki ya kati na nchi inayoinyima amani ni Iran, huku US akiwa na malengo zaidi ya ushindani wa kiuchumi. Na wote wanajikuta ili wafanikishe hayo ni kuivamia Iran kwa nguvu zao zote. Wote mchawi wao ni Iran, syndicate imesoma waivamie Iran.

Japo ni kweli US huwa anamsikiliza Israel, naamini US isingekuwa na maslahi yeyote ya kiuchumi kwa Iran, nadhani hata kama Israel ingepambana na Iran, US ingetoa msaada wa silaha na baadae kuwakalisha kusuluhisha na si kuingia mzima mzima kama hivi labda tu endapo ingeonekana Israel inapigwa imezidiwa.

Hivyo hawa jamaa wanachofanya ni uonevu, na China atakuwa mpuuzi akikaa kimya, Russia ndio kabisa wana akili za kutengeneza silaha na kupigana vita, lakini uwezo wa kiushawishi, siasa na hata utamaduni hao jamaa wana zero. Na hilo ndilo lilivunja USSR. Na hata leo hii wanazidiwa kete na EU na US.

Russia imesinzia, wakati wa USSR walipoteza wanasayansi vichwa, wakakimbilia EU na US.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…