Shalom from Jerusalem,
Awali ya yote napenda niweke wazi kuwa sikumpenda kabisa Magufuli kutokana na ukatili wake ambao uliumiza wengi Tanzania. Lakini ukweli usiopingika ni kwamba ukatili wa Magufuli waafrika wengi nje ya Tanzania na hata ndani ya nchi hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kiufupi kulikuwa na kitu kama brainwashing iliyowafanya wengi kutokuona maovu ya rais huyo dikteta.
Nimepata wakati mgumu sana kuwaaminisha watu (waafrika wa nchi nyingine mbali na Tanzania) kuwa Magufuli hakufaa na kwamba alikuwa muuaji, alikandamiza wapinzani, alibambikiza kesi wapinzani na uovu unaofanana na huo.
Hivyo kujitokeza kwa wanaharakati wakiongozwa na Maria Sarungi wanaotaka BET imwondoe Diamond eti kwa sababu alimuunga mkono Magufuli , "kipenzi cha waafrika", kunaweza kusieleweke kwa waafrika wengi ambao ndiyo hasa wapiga kura kwenye tuzo za 2021 za BET.
Wala siyo siri weusi wengi huku ugaibuni wanamwona Magufuli alikuwa shujaa na ni ngumu sana kuwaaminisha vinginevyo.
Jambo baya zaidi wanalolifanya akina Maria ni kumpinga Diamond lakini wakati huo huo na kwa nguvu isiyo na mfano kumuunga mkono Burna Boy. BET inaweza isiwaelewe na inaweza kuona kuwa wanatumika.
Imani yangu ni kwamba hata ikiwa Diamond atashindwa basi siyo kwa sababu ya akina Maria bali ni ushindani wa kawaida kabisa wa mziki.
ANGALIZO: KUPENDWA KWA HAYATI MAGUFULI TANZANIA NA AFRIKA HAKUMAANISHI KWAMBA ALIKUWA NI KIONGOZI MZURI LA HASHA, BALI NI UJINGA WA WATU KUTOKUTAMBUA YALIYOKUWA YANAENDELEA NYUMA YA PAZIA. KWA WAELEWA WA MAMBO MAGUFULI HAKUWA KIONGOZI MZURI HATA KIDOGO.