Ulishawahi kununua au una-burn CD tu?Wasanii wanaojitambua duniani hawafanyu ujinga unaofanywa na wasanii wetu hapa Tz, wengi hujiweka mbali na siasa ili kuepuka kuwavuruga fans wao wanaoweza kuwa na itikadi tofauti.
Hawa wetu walizubaa akili zao muda mrefu sana sasa ndio wanaamshwa, next stop kwa wale wajinga bongo movie kina Steve Nyerere, Wema, Uwoya, na wenzao, hakuna kununua movie zao.
Kwahiyo na Harmonize, Zuchu mmewasusia? Vipi na wasanii wengine Kama wote walioshiriki campaign za CCM?Shida ni yeye kuamua kujiunga na watesi wa jamii ya Tanzania,ilhali msanii anajiita kama ni kioo
cha jamii.Kwa hilo tuu amepoteza uhalali wa kuendelea kusimamia imani hiyo.Zaidi tutamwita msimamia au mpigania maslahi yake binafsi huku akiihitaji jamii kupata mafanikio yake binafsi.
Wanapindua meza kila uchaguzi jiwe kwenye uchaguzi wa 2020 alikiri wabunge wasijisifu kujipeleka wenyewe bungeni ila wamepelekwa Mungu akafanya yake.Ahhh.. Kumbe!..
Sasa mbona ccm haifi kwa presha za chadema?
Ulitaka amuimbe mwenyekiti wa UDP...... cheki mashairi yake objectively utabaki mdomo wazi! "Wapinzani piga risasi"!
Magufuli baba lao, Makonda baba lao...
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!
Watashindwa inshalah.Vipi hawa "Wapuuzi" wasipo puuzwa Mondi amejipangaje kwa mengine yajayo?
Kibinadamu kuwa na mbadala ni muhimu.
Mshaurini na hilo pia
Tupe naomi yako,kwani wewe unasemaje.Kwahiyo na Harmonize, Zuchu mmewasusia? Vipi na wasanii wengine Kama wote walioshiriki campaign za CCM?
Wewe ndiyo mmoja kati ya wanaofanya Watanzania wengi waitwe wapumbavu. Yaani maiti imewekwa uwanjani, na Serikali imesema ni mapumziko, kwa nini unashangaa watu wanakwenda kuaga?Mkuu hayo ni maoni yako na yanaheshimiwa. JPM kama asingekuwa jasiri asingefanya mengi huko mikoani.
SGR isingefika ilipofika, ndege zisingenunuliwa, lile jengo la kupokea wageni airport lisingemalizika kwa wakati.
JPM alikuwa jasiri na marais wengine wa afrika waliuona uthubutu wake ndio maana alipoenda Ethiopia wakawa wanamzunguka.
Hiyo habari ya yeye kuwa mrundi ni hadithi za kitoto za humu jukwaani sehemu iliyojaa CHADEMA na wengi waliobaniwa mianya yao ya kutajirikia maofisini.
Uhuru wa habari uwe na faida kwa kila upande, huwezi kupewa uhuru halafu ukawa siku zote unaihujumu nchi yako. Wakati wa vita ya ugaidi kule MKIRU mtu anafanyia kazi wageni yaani anaihujumu nchi aliyozaliwa!. JPM hakutaka kabisa huo ujinga.
Ameshalala na hataamka, lakini naamini aliwagusa watu wengi, asingeweza kuuvuta umati ule pale uwanja wa ndege siku jeneza lake lilipoenda Zanzibar kama kweli alikuwa na roho mbaya.
Shalom from Jerusalem,
Awali ya yote napenda niweke wazi kuwa sikumpenda kabisa Magufuli kutokana na ukatili wake ambao uliumiza wengi Tanzania. Lakini ukweli usiopingika ni kwamba ukatili wa Magufuli waafrika wengi nje ya Tanzania na hata ndani ya nchi hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kiufupi kulikuwa na kitu kama brainwashing iliyowafanya wengi kutokuona maovu ya rais huyo dikteta.
Nimepata wakati mgumu sana kuwaaminisha watu (waafrika wa nchi nyingine mbali na Tanzania) kuwa Magufuli hakufaa na kwamba alikuwa muuaji, alikandamiza wapinzani, alibambikiza kesi wapinzani na uovu unaofanana na huo.
Hivyo kujitokeza kwa wanaharakati wakiongozwa na Maria Sarungi wanaotaka BET imwondoe Diamond eti kwa sababu alimuunga mkono Magufuli , "kipenzi cha waafrika", kunaweza kusieleweke kwa waafrika wengi ambao ndiyo hasa wapiga kura kwenye tuzo za 2021 za BET.
Wala siyo siri weusi wengi huku ugaibuni wanamwona Magufuli alikuwa shujaa na ni ngumu sana kuwaaminisha vinginevyo.
Jambo baya zaidi wanalolifanya akina Maria ni kumpinga Diamond lakini wakati huo huo na kwa nguvu isiyo na mfano kumuunga mkono Burna Boy. BET inaweza isiwaelewe na inaweza kuona kuwa wanatumika.
Imani yangu ni kwamba hata ikiwa Diamond atashindwa basi siyo kwa sababu ya akina Maria bali ni ushindani wa kawaida kabisa wa mziki.
ANGALIZO: KUPENDWA KWA HAYATI MAGUFULI TANZANIA NA AFRIKA HAKUMAANISHI KWAMBA ALIKUWA NI KIONGOZI MZURI LA HASHA, BALI NI UJINGA WA WATU KUTOKUTAMBUA YALIYOKUWA YANAENDELEA NYUMA YA PAZIA. KWA WAELEWA WA MAMBO MAGUFULI HAKUWA KIONGOZI MZURI HATA KIDOGO.
Wewe huongei hapo ukiwa mirembe kweli.Chadema na watu wake ni wagonjwa wa akili isipokuwa Mbowe anajitambua kidogo
JPM alikuwa kiongozi shupavu huko mtaani walimuelewa sana.Wewe ndiyo mmoja kati ya wanaofanya Watanzania wengi waitwe wapumbavu. Yaani maiti imewekwa uwanjani, na Serikali imesema ni mapumziko, kwa nini unashangaa watu wanakwenda kuaga?
Ubora wa mtu haupimwi na watu waliokwenda kuaga kwa kuwa Afrika hata wachawi na wezi huwa tunakwenda kuwaaga.
Watu mtaani kwenda kuaga maiti ya marehemu ni mila za Kiafrika. Hapa Dar hata Marehemu Stephen Kanumba naye alifunga mtaa kwenye msiba wake.
Hata Ruge Mutahaba naye alifunga nyomi
Waafrica wapi wewe lofa? Umelalia kifua cha mumeo hapo ndio akakudanganya hivyo? Mpuuzi kweli kweli!!!
Wew kama sio Sabaya basi ni Libashite na naongea kwa Staili ile ya Mkuu wa wilaya ya Iringa kuwa Tuliza mat...wewee. Magufuli ni muharifu tuu kama genge lake alilo unda la Sabaya na Makonda alistahili muda huu kuwa huko aliko Sabaya ila Mungu akaona kwa Ukatili na mauaji aliyo yafanya ni vema Amfyekelee mbali yeye mwenyewe kuliko kusubili mahakama za dunia.Alimbambikizia kesi Nani. Nguvu ya Rais wa Tz. Anahitaji kuzunguka kufanya jambo. Ukatili gani amefanya. Mana nyie mnasisitiza haki ya asili ya kujitetea. Ushahidi nk.
Malipo ni hapa duniani,yaani huyu kijana katoka kumdhalilisha baba yake hapa majuzi wakisaidiana na mama,machozi ya mtu hua hayapotei bureWatashindwa inshalah.
Ila ikitokea asikate tamaa, achukulie kama ajali tu aendeleze ubunifu wa kazi zake abaki Msanii kinara Africa Mashariki.
"a comedian".Africa ilikuwa inamfurahia Magufuli kama watoto wanavyomfurahia Mr Bean!
Asipoelewa ninachomaanisha, wadau saidieni kumwelewesha.
Maria S. Tsehai yupo chini ya mbawa za tai,amekumbatiwa na tai.Maria kama asingekuwa ni binti wa Mzee Sarungi aliyekuwa waziri na mheshimiwa miaka ya nyuma basi siku nyingi sana wasiojulikana wangekuwa wameshafanya mambo yao mabaya.
Dadavua mkuu. Umetema fumbo fulani hivi.Maria S. Tsehai yupo chini ya mbawa za tai,amekumbatiwa na tai.
Yuko sahihi kwa asilimia nyingi, hata mimi hitimisho langu kutokana na majadiliano na watu wengi nje ya nchi yetu wengi wanaamini dikteta mwendazake alikuwa kiongozi safi na mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine barani Afrika.
Nilikuwa nikijaribu sana kuwaelimisha kinachoendelea lakini nadhani alifanikiwa sana katika kuhadaa watu wengi(mataifa mengi) na hata raia(blacks) wa nchi za Ulaya na Amerika ya Kaskazini wanaofuatilia siasa za Afrika walimuona kama shujaa dikteta mwendazake.
Just a moment...! Mpaka hapo unakiri kuwa mwendazake alikuwa mkatili, au siyo? Kwamba vitendo anavyotuhumiwa navyo ni kweli! Hivyo na waliomuunga mkono kwa namna fulani ni wahusika.licha ya ukatili wake,
What...? Je na waliofanyiwa ukatili nao walimpenda? Kwamba pamoja na ukatili wake, Waafrika walimpenda! Kwa hiyo ukatili Afrika ni moja katika sifa inayokubalika katika uongozi au siyo?Afrika ilimpenda Magufuli,
My God...! Yaani kitakachowafanya waangukie pua ni kule kupinga na kulaani ukatili na kukataa kuwaunga mkono wanaofumbia macho vitendo vya kikatili? Masikini Afrika!mtaangukia pua vita yenu dhidi ya Diamond