Ila wakishiriki za chadema itakuwa fresh tu!

Huu upumbavu upo tz tu
 
Funzo lipi mkuu, Diamond amewakwamisha wapi kufanya siasa za mafanikio?
Wasanii wanaojitambua duniani hawafanyu ujinga unaofanywa na wasanii wetu hapa Tz, wengi hujiweka mbali na siasa ili kuepuka kuwavuruga fans wao wanaoweza kuwa na itikadi tofauti.

Hawa wetu walizubaa akili zao muda mrefu sana sasa ndio wanaamshwa, next stop kwa wale wajinga bongo movie kina Steve Nyerere, Wema, Uwoya, na wenzao, hakuna kununua movie zao.
 
Ila wakishiriki za chadema itakuwa fresh tu!

Huu upumbavu upo tz tu
Elewa dada, hawatakiwi kujihusisha na siasa ili wasiwavuruge fans wao wenye itikadi tofauti.
 
Huu uzi wakipumbavu na umeandaliwa na mjinga wa ccm.

1. Watanzania kila mmoja anahaki kutoa maoni yake.

2. Chadema hawana uhusiano kama chama Kwenye sakata hili

3. Uhuru, haki na Amani .... matunda kila mtanzania angeyatamani kuyafurahia


Uhuni wa wasanii kila nyakati za uchaguzi kujiweka ccm na kuwabagua watanzania wengine ni ujinga na upumbavu

Ikumbukwe na ieleweke wazi, msaani yeyote anawashabiki katika vyama vyote na pia kwawasio na vyama

Act, Chadema, ccm, cuf, NCCR nk,

Msanii anapojifungamanisha na ccm pekee na kuwatukana wale wengine wote,anajiharibia.

Namaanisha yeye anajirasmisha kuwa Mali ya ccm na hivyo basi mashabiki wake ni ccm..... waliobakia wote nje ya ccm anakuwa amewakanana

Waliobakia wote, haramu kwa msanii huyo. Hii concept ya cdm unaipataje hapa? Hawa wengine unawaweka wapi?

Kauli ya kuwafungamanisha cdm na kuwaacha wengine wote kama cuf, nccr, Act, Tlp nk ni upumbavu wa uccm na propaganda za kijinga.
 
Kwaiyo hii ndo sababu ambayo iliyopelekea cdm kuanguka kwenye chaguzi.

Kama chama yako mambo ya msingi ya kufanyia kazi na si huu upuuzi eti hakuna kununua movie zao.

Kwaiyo ukishaacha kununua movie zao ndo wale wabunge 19 walofukuzwa chama wataondolewa bungeni?
 

Naomba urudie kusoma namba 3 hapo kwenye maelezo yako alafu uje unambie uhuru wa Diamond cdm mliununua kwa kiasi gani cha fedha.
 

1. Unaushahidi wa unachokiongea hapa ?

2. Chadema na kiongozi gani ametamka?

3. Nccr, cuf, Act, tlp nk wapo kundi lipi na kwa ushahidi upi?

4. Alipokuwa anapanda majukwa ya ccm lini alipanda majukwa ya Nccr, cuf, Act, tlp nk ili kuwapa watanzania wa itikadi zote haki ya usawa?
 
Shida ni yeye kuamua kujiunga na watesi wa jamii ya Tanzania,ilhali msanii anajiita kama ni kioo
cha jamii.Kwa hilo tuu amepoteza uhalali wa kuendelea kusimamia imani hiyo.Zaidi tutamwita msimamia au mpigania maslahi yake binafsi huku akiihitaji jamii kupata mafanikio yake binafsi.
 
Naomba urudie kusoma namba 3 hapo kwenye maelezo yako alafu uje unambie uhuru wa Diamond cdm mliununua kwa kiasi gani cha fedha.

Kwanza thibitisha madai yako kwamba hiyo ni move ya Chadema

Tena weka ushahidi

Tutajadili mengine yote, ila tuthibitishie Chadema unawahusishaje na kwa ushahidi gani
 
Naona unachanganya biashara na haki. Yule ni mfanyabiashara, na mfanyabiashara yeyote anafata masirahi. Weka hii akilini
 
Naona unachanganya biashara na haki. Yule ni mfanyabiashara, na mfanyabiashara yeyote anafata masirahi. Weka hii akilini

Umeelewa ninacho kuuliza?
👇
1. Unaushahidi wa unachokiongea hapa

2. Wa Chadema na kiongozi gani ametamka?

3. Nccr, cuf, Act, tlp nk wapo kundi lipi na kwa ushahidi upi?

4. Alipokuwa anapanda majukwa ya ccm lini alipanda majukwa ya Nccr, cuf, Act, tlp nk ili kuwapa watanzania wa itikadi zote haki ya usawa?
 

Your browser is not able to display this video.


Swali langu ni moja tu...je huyo Sadala angeweza kuhudhuria mikutano ya Watanzania wenye itikadi tofauti na hicho chama cha watekaji, watesaji na wauwaji hata kama angealikwa?

Kama jibu ni hapana, basi ni mahaba kwa CCM ndiyo yalimshawishi kuvalishwa kofia na huyo dhalimu. Hivyo mwacheni avune alichopanda...huwezi kupanda limau ukavuna nanasi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…