Kampeni dhidi ya Diamond Platnumz: Wanaharakati kuweni serious kidogo
Kwani wananchi ni Chadema,na kipi kinachowafanya muamini nyie ndo mko sawa na wala sio yeye,ila namsifu dogo yaani hajataka hata kuwajibu yaani kuiweka level yake juu zaidi ya mgombea mmoja wa uraisi yule kichaa wa ubelgiji
Too late man, that's a wake up call, mitandao siku hizi ina nguvu zaidi ya polisi na Ndugai, liwe funzo kwa Diamond mwenyewe na wasanii wenzake kina Harmonize, Kiba na wengine, ole wao tena washiriki kampeni za CCM, mbaya zaidi alijitutumua twitter hajawahi kushindwa vita ndio akajiharibia kabisa.
Kwani sasa kashindwa,kwa kipimo gani kilichoonyesha kashindwa,nyie ndo mmejionyesha msivyo na akili
 
Ninazo sababu nzuri, sasa unazihitaji za nini wakati umeshaniita mfuata mkumbo?

Wewe umefanya kwa sababu zipi mkuu, ili tukuondoe pia kwenye group la wafata mkumbo, maana umeshasema si mwanasiasa na si mwanaharakati.
 
Wakati watu wanawasema akina Karume na Nyerere ulishawahi ona Makongoro anamtetea Baba yake

legacy haitetewi inajitetea

Nyerere anasemwa sana lakini hotuba zake na kazi zake zianajitetea zenyewe

Hatufanyi kazi ya kuhesabu viwanda vya nyerere na Madaraja

Hao wanavuna chuki waliyoipanda
Ni kwelu
 
Kumbe wewe ni mpumbavu kiasi hiki. Wanaharakati ni watu wanaodai uhuru, haki na usawa na utawala unaoheshimu, kulinda na kuitetea Katiba.

Kama huyo msanii wako akachagua upande wa watekaji, watesaji na wauwaji wa Watanzania wenye misimamo tofauti kisiasa huo ni uamuzi wake.

Watanzania walipotekwa alikuwa kimya, walipoteswa alikuwa kimya, walipopotezwa hakupaza sauti...hii ina maana kuwa aliwaunga mkono wahusika.

Halafu leo anawataka hao hao waliopitia machungu huku yeye akiwa kimya wamuunge mkono katika kutafuta umaarufu kupitia mgongo wao, ili iweje?

Hiyo tuzo itawarudishia uhai wapendwa wao? Hiyo tuzo itawaponyesha vilema wa maungo? Hiyo tuzo itawafuta machozi wazazi, ndugu na marafiki wa waliopotezwa?

Acheni ujinga, huyo na usanii wake tupa kule...kama mnampenda mkanywe naye chai huko kuzimu aliko huyo dhalimu anayemvisha kofia.
Lissu ni mwanaharakati au ni kiongozi wa Chadema?Ukijibu hili swali utajielewa kama wewe ni Nyumbu au binadamu wa kawaida
 
Unapo simama na upande usio wa haki una poteza yote kutoka kwa wapenda haki na ustawi wa taifa.
𝚄𝚙𝚊𝚗𝚍𝚎 𝚞𝚜𝚒𝚘 𝚗𝚊 𝚑𝚊𝚔𝚒 𝚔𝚠𝚊 𝚖𝚊𝚘𝚗𝚘 𝚢𝚊𝚔𝚘 𝚋𝚘𝚝𝚑𝚎𝚛..! 𝚠𝚊𝚙𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚘𝚗𝚊 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝙸𝚜𝚛𝚊𝚎𝚕 𝚗𝚒 𝚑𝚊𝚔𝚒 𝚢𝚊𝚘 𝚔𝚞𝚛𝚞𝚜𝚑𝚊 𝚖𝚊𝚔𝚘𝚖𝚋𝚘𝚛𝚊 𝙶𝚊𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚠𝚊𝚞𝚊 𝚆𝚊𝚙𝚎𝚕𝚎𝚜𝚑𝚒𝚗𝚊 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚠𝚊𝚙𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚘𝚗𝚊 𝚆𝚊𝚙𝚊𝚕𝚎𝚜𝚝𝚒𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊 𝚑𝚊𝚔𝚒 𝚔𝚞𝚕𝚒𝚙𝚒𝚐𝚊𝚗𝚒𝚊 𝚃𝚊𝚒𝚏𝚊 𝚕𝚊𝚘.
 
Unapokuwa

1. Mfanya biashara

2. Msanii

3. Mtumishi wa Mungu (sheikh, mchungaji no)

Unayehudumia watu wa vyama, dini, itikadi na mitazamo tofauti.

Epuka kujifungamanisha upande mmoja, toa huduma kwa usawa bakia katikati...

Ukijifungamanisha na upande mmoja nakuwazodoa wa pande zingine basi kubali matokeo. Watakapo kusurubu usitafute mchawi.
 
Huu uzi wakipumbavu na umeandaliwa na mjinga wa ccm.

1. Watanzania kila mmoja anahaki kutoa maoni yake.

2. Chadema hawana uhusiano kama chama Kwenye sakata hili

3. Uhuru, haki na Amani .... matunda kila mtanzania angeyatamani kuyafurahia

Uhuni wa wasanii kila nyakati za uchaguzi kujiweka ccm na kuwabagua watanzania wengine ni ujinga na upumbavu

Ikumbukwe na ieleweke wazi, msaani yeyote anawashabiki katika vyama vyote na pia kwawasio na vyama

Act, Chadema, ccm, cuf, NCCR nk,

Msanii anapojifungamanisha na ccm pekee na kuwatukana wale wengine wote,anajiharibia.

Namaanisha yeye anajirasmisha kuwa Mali ya ccm na hivyo basi mashabiki wake ni ccm..... waliobakia wote nje ya ccm anakuwa amewakanana

Waliobakia wote, haramu kwa msanii huyo. Hii concept ya cdm unaipataje hapa? Hawa wengine unawaweka wapi?

Kauli ya kuwafungamanisha cdm na kuwaacha wengine wote kama cuf, nccr, Act, Tlp nk ni upumbavu wa uccm na propaganda za kijinga.
Umeelewa ninacho kuuliza?
[emoji116]
1. Unaushahidi wa unachokiongea hapa

2. Wa Chadema na kiongozi gani ametamka?

3. Nccr, cuf, Act, tlp nk wapo kundi lipi na kwa ushahidi upi?

4. Alipokuwa anapanda majukwa ya ccm lini alipanda majukwa ya Nccr, cuf, Act, tlp nk ili kuwapa watanzania wa itikadi zote haki ya usawa?
Naona unachanganya biashara na haki. Yule ni mfanyabiashara, na mfanyabiashara yeyote anafata masirahi. Weka hii akilini
Ashakula biashara yake, bila shaka ilimlipa sana.

Sasa ni nini tena anataka?

Kama anataka biashara nyingine atayapata Chato makaburini

Si ana miguu aende
 
Ninazo sababu nzuri, sasa unazihitaji za nini wakati umeshaniita mfuata mkumbo?
Punguza jazba mkuu,

Tusaidie izo sababu ili tunufaike na kuelimika pamoja.
 
Haikuwa busara kwa mond kipigania ccm kwenye uchaguzi wakati akijua watz ni wanachama wa vyama mbali mbali!!!Hata ivyo atamfuata mwendazake kimziki halafu badae kiroho na nafsi!!
 
Lissu ni mwanaharakati au ni kiongozi wa Chadema?Ukijibu hili swali utajielewa kama wewe ni Nyumbu au binadamu wa kawaida

Kwanza upo nje ya mada by 180 degrees hebu jitafakali uone hilo la Lisu na huu uzi.
 
Bila kumtaja Ney wa mitego na Roma utakuwa unajidanga akili yako tu
Wasanii wanaojitambua duniani hawafanyu ujinga unaofanywa na wasanii wetu hapa Tz, wengi hujiweka mbali na siasa ili kuepuka kuwavuruga fans wao wanaoweza kuwa na itikadi tofauti, hawa wetu walizubaa akili zao muda mrefu sana sasa ndio wanaamshwa, next stop kwa wale wajinga bongo movie kina Steve Nyerere, Wema, Uwoya, na wenzao, hakuna kununua movie zao.
 
1622993623237.png
 
Unapokuwa

1. Mfanya biashara

2. Msanii

3. Mtumishi wa Mungu (sheikh, mchungaji no)

Unayehudumia watu wa vyama, dini, itikadi na mitazamo tofauti.

Epuka kujifungamanisha upande mmoja, toa huduma kwa usawa bakia katikati...

Ukijifungamanisha na upande mmoja nakuwazodoa wa pande zingine basi kubali matokeo. Watakapo kusurubu usitafute mchawi.
Mkuu unataka kusema Abood Mabasi yake hayana wateja, Mwana FA mziki wake hausikilizwi pia gwajima kanisa lake sasa ivi halina waumini.

Au nataka kutuambia kuwa wanaccm wasi support mziki wa professor J kwa sababu ni wa upande wa pili
 
Hawa watu wanatuchanganya mkuu, Wako bungeni miaka kibao leo wanataka mapishi yaliyowashinda wao wakati wako jikoni wamtwishe Diamond.

Yani Diamond leo ndo kawa sababu ya chama fulani kutofanikiwa katika mambo fulani.
Niliingia kwenye website ya change.org nikaangalia petition inayotaka diamond asiwemo kwenye kinyang'anyiro na nikaangalia petition inayotaka diamond abaki kwenye kinyang'anyiro.

Zote zimetoa sababu kwanini zinaamini petition yao inastahili kupigiwa kura. Hata wewe kama una hamu ya kujua kilichopelekea petition kuanzishwa ingia change.org juu kulia kuna mistari 3 inaangalia chini. Bonyeza hiyo mistari utaona option ya search.

Kubali search na andika 'bet diamond' itakuja petition utasoma sababu za walioanzisha petition na utaacha kubishana na watu humu.

Kutoka hapo mimi nasema kwamba ilikua ngumu sana kwa diamond na wasanii wengine kujiweka mbali na makonda na ccm kwa ujumla. Na wala haina haja ya kuelezea kila mtu anajua maisha yalivyokua.

Roma alisema vyema, alisema 'Siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki?' ile crackdown ilikua ni ama ikuguse au uwe karibu na serikali ili isikuguse. Wanafananisha na swala la kile kitengo cha SARZ cha Nigeria, kuna tofauti kubwa kati ya kutaka askari waache ukatili na kutaka rais aache ukatili.

Watu wana chuki zinaishi kwa miaka katika hii petition ndiyo wamepata pa kupumzikia. Jana nacheki ilikua signed na watu 7K leo jioni imepostiwa screenshot ni 12K and counting. Ya kutaka asitolewe jana niliona ina saini 100 leo 1K and counting.

Mashabiki badala ya kuonyesha mnavyomkubali kwa kwenda kusaini petition ili asiondolewe mpo bize kuanzisha nyuzi za lawama.
 
Narudia,
Nina sababu tofauti kabisa na wanzosema wengi lakini nieleze kwa nini nikueleze wakati kila post yako unanipachika jina la kejeli?

Umeanza kuniita mfuata mkumbo sasa unaniita mwenye jazba sijui utakanijibu hii utaniitaje.

Punguza jazba mkuu,

Tusaidie izo sababu ili tunufaike na kuelimika pamoja.
 
Hawa watu siku wakishika usukani tutegemee visasi tu
Kwahali iliyopo ni bora hao na visasi vyao kutawala maana watadeal ns wabaya wao kuliko ninyi mnaowaua waliowashinda katika chaguzi wasiohatia ili mtawale kwa dhulma.
 
Kumbe wewe ni mpumbavu kiasi hiki. Wanaharakati ni watu wanaodai uhuru, haki na usawa na utawala unaoheshimu, kulinda na kuitetea Katiba.

Kama huyo msanii wako akachagua upande wa watekaji, watesaji na wauwaji wa Watanzania wenye misimamo tofauti kisiasa huo ni uamuzi wake.

Watanzania walipotekwa alikuwa kimya, walipoteswa alikuwa kimya, walipopotezwa hakupaza sauti...hii ina maana kuwa aliwaunga mkono wahusika.

Halafu leo anawataka hao hao waliopitia machungu huku yeye akiwa kimya wamuunge mkono katika kutafuta umaarufu kupitia mgongo wao, ili iweje?

Hiyo tuzo itawarudishia uhai wapendwa wao? Hiyo tuzo itawaponyesha vilema wa maungo? Hiyo tuzo itawafuta machozi wazazi, ndugu na marafiki wa waliopotezwa?

Acheni ujinga, huyo na usanii wake tupa kule...kama mnampenda mkanywe naye chai huko kuzimu aliko huyo dhalimu anayemvisha kofia.
Hahahahaha
Kama wao walishindwa kubadili mapishi wakiwa kule jikoni na walikuwa wengi, Diamond ndo ataweza?
 
Back
Top Bottom