Kampeni dhidi ya Diamond Platnumz: Wanaharakati kuweni serious kidogo
Okay, umetumia vigezo gani kubaini Upande aliosupport yeye ulikuwa si wa haki.

Lakini si yeye tu alieshiriki,
Mbona sijaona kampeni ya kuzuia watu wasiende kwenye show za wasanii walioshiriki kampeni za ccm? Kama analengwa yeye tu na wengine Wanaachwa hii tutaitofautishaje na wivu.
Usemi kuwa Mungu sii Athumani ,una maana Sana,kuwa binadamu sii wa kutenda haki wakati wote,ila Mungu pekee.Binadamu aweza kutenda bila kujua kama anaathiri wengine nakuona ni sawa kwa kadiri ya uelewa wake.
 
Lissu ni mwanaharakati au ni kiongozi wa Chadema?Ukijibu hili swali utajielewa kama wewe ni Nyumbu au binadamu wa kawaida
Sikiliza wewe kilaza, sijaona popote Chadema ilipoweka msimamo kama chama kuhusu jambo hili. Si ajabu hata wewe dakika hii kwa akili fupi unaamini mimi ni Chadema, kisa? Simkubali huyo mfuasi na mpenzi mkubwa wa mwendazake.

Sasa na mimi nakuuliza swali, je Lissu anapomtetea Sabaya akitaka atendewe haki kisheria anaongea kama kiongozi wa Chadema au ni maoni binafsi? Kumbuka haki ni haki, haijalishi itikadi yako.

Je huyo msanii wa CCM kuna popote amewahi kutoa kauli rasmi kama msanii kutetea na kudai haki akiwa jukwaani? Kuna mahali amewahi kulalamikia utekaji, uteswaji na mauaji ya Watanzania waliothubutu kumkosoa jiwe?
 
Usemi kuwa Mungu sii Athumani ,una maana Sana,kuwa binadamu sii wa kutenda haki wakati wote,ila Mungu pekee.Binadamu aweza kutenda bila kujua kama anaathiri wengine nakuona ni sawa kwa kadiri ya uelewa wake.
Sawa Mkuu,
 
Alipiga kampeni 2019 tena akiongea na muuaji kwa simu akiwa kigoma
 
Kama hivi

WASHOBOKAJI SASA...!!
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi, chinja, mashoga hao.
Wataweza kweli aah wapii, kushindana nasi aah wapi. Tuna Polisi tuna jeshi wamekwishaa!
 
Hata wacongoman waliwanyoosha wanamuziki wa congo kwa kumsapoti dikteta Kabila abadili mihula ya uongozi.Hakuna mwanamuziki yeyeto wa congo anaweza piga show ulaya yote si koffi,werason,wala inoss
 
Unataka chama gani kitoke kianze kujibu mambo binafsi ya watu.kwa hicho unachotaka hicho chama kifanye unadhani kitajibu ujinga wawatu wangapi ikiwepo na huu ujinga wako.
 
Kama hivi

WASHOBOKAJI SASA...!!
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi, chinja, mashoga hao.
Wataweza kweli aah wapii, kushindana nasi aah wapi. Tuna Polisi tuna jeshi wamekwishaa!
Eti, Magufuli baba lao, Makonda baba lao...



CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!

Halafu leo tunatakiwa tuungane Sadala apewe tuzo, really? Acheni huu upuuzi!
 
Twaingoja mkuu
subiria mkuu, inakuja!
ushabiki wangu kwa diamond ni mdogo ukilinganisha na nilionao dhidi ya alikiba (the best bongo flavour artist so far), lakini kwa hili linaloendelea jamaa atachukua kura nyingi sana (za huruma) kutoka kwa wabongo maana wanaona kama anaonewa.
 
Mleta mada angalia hizo comments za unao jadili nao utakuta zinaanza na neno.

Wewe ni mpumbavu

Wewe ni kilaza

Huna akili kabisa

Hujielewi
N.k

Unajua ni kwanini wanaanza na maneno Kama hayo?
Hujaona tu ni kiasi gani chuki na hasira ilivyo mbele badala ya kujibu hoja.

Anaanza na neno Kama hilo makusudi kabisa ili kuwavutia watu wasome comment yake huku wakikuweka wewe upande wa negative yaani watu kabla hawajasoma ulicho kiandika wakuone mjinga huku anachokisema yeye ndio kiwe cha maana.

Soma comments taratibu utagundua hiyo mijadala ya watu wanao jiita ma GT ilivyo ya ajabu.
 
Soma comments taratibu utagundua hiyo mijadala ya watu wanao jiita ma GT ilivyo ya ajabu.
Unasumbuliwa na utoto kijana, wengine tumeanza kutetea na kudai haki hata kabla ya CCM kuzaliwa mwaka 1977! Toka enzi hizo hatujatetereka katika maswala yanayohusu utawala unaozingatia sheria. Kwa bahati mbaya CCM imehakikisha hatuna utawala mwingine tunaoweza kuurejea na kuulinganisha nao.

Wengine tumepoteza mengi kwa kutoikubali CCM kwa muda wote huo na hatutachoka kudai utawala wa haki na serikali inayojitambulisha kama ya wananchi na si serikali ya CCM. Wewe endelea kuunga mkono tawala za kiimla ambazo hata zikiteua vichaa, wanapewa rungu la kutupigia sisi wananchi.

Tunataka kila moja apate hili somo, huwezi kulala na fisi wakati una jukumu la ulinzi na usalama wa kondoo...hicho ndicho kiwango cha unafiki unaowatafuna Watanzania walio wengi kwa sababu ya uelewa mdogo. Unaweza kunenepa kwa kula makombo unayotupiwa ukiwa chini ya meza kuu mradi ukubali utumwa.
 
Itakuwa funzo kwa Diamond.. kutokusimama na oppressors. Angalia walichofanya wasanii wa Nigeria dhidi ya serikali yao halafu alichokuwa anafanya Diamond.

Anastahili kuendelea kusagiwa kunguni.. Itakuwa ni funzo la yeye kutokudharau wananchi anatakiwa ajue msanii ni kioo cha jamii

diamond ataendela na harakati zake za kuiunga mkono ccm hata akishindwa hizo tuzo.

unajua mtu aliyekata tamaa ya uhai hurusha mateke hewani kwa lengo gani?!chadema imekwisha kwa sasa inaishi kwa kick tu.

msanii amabye yuko bega kwa bega na chadema ji nay wa mitego na roma.wengine wote wanaangalia maisha yao,hizo harakati kunuka washaona hazina future.
 
Back
Top Bottom