Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Aliekwambia sina ndoa nani🤣 au unadhani kila mtu alikamatiwa kama mama ako
 
Hii aya ya mwisho ndo umejivua nguo kabisa! Sasa huna kazi huna biashara kipato unapata wapi????! Na wewe ni mwanaume unataka nikusikilize? Nyie mbona kuna vituko humu?!!! Are you seriously a man na unaandika huo utopolo wako mwishoni eti bila kipato unaishi. Ndo mmefanya wanaume wanagombea kuvaa vibukta wapate vipato virahisi
 
Tunarudi kule kule, wanaume wanyanyasaji wapo au hawapo?! Yani kwanini mnageneralise wanawake wote? Mngeanzia kwenye chimbuko la kwanini mwanamke amefika hatua ya kujipambania. Ni kwamba wanaume mlimmis use power zenu!! Full stop. Hatukatai wanawake wanaojisahau wapo lakini hiyo sio sababu ya kusema wanawake kuwa makazini ni tatizo. Sema kila mtu a deal na mke wake nyumbani! Na ndo unakuta mwanaume
Akioa tu, anamuachisha kazi mkewe bila
Hata kumpima kama anahekima yakusimamia nafasi au la.

Kwa dhana hiyo ya kugeneralise basi tutengeneze sheria kwamba mwanaume yyote anaenyanyasa mwanamke auwawe kama mnavyotaka wanawake washinde majumbani kulea watoto.
Sijui hata kama tunaelewana au mnakaza mafuvu tu
 
Kwahiyo unakubaliana na mimi kwamba wanawake kutokuwepo makazini na wao kushinda nyumbani hakubadilishi uhalisia? Maana mnakomalia kusema mwanamke abaki nyumbani alee watoto. Saizi unasema wazaramo:

Basi mwanzoni mwa mada mngesema wanawake wa kihaya na kichaga wasifanye kazi walee watoto.

Ndo maana napata nguvu ya kusema wanaume mmekua tu intimidated. Kwasabau manzese huko sijui magomeni wanawake kibao hawana kazi na watoto wao wanazurula mtaani hakuna anaewalea.
 
Hiyo exposure unayoiongelea wewe ni moja uliyoiona kwenu. Mimi nimefanya kazi kwenye eneo ambalo kila siku cases zinakuja tofauti. Na kama umesoma ukaelewa sijasema mwanaume mmoja ana hizo
Sifa zote. Kila comment ilikua na sifa ya aina tofauti ya mwanaume. Hivi mnabisha kwamba wanaume wengi wamerudisha nyuma maendeleo ya mwanamke? Yani mwanaume anauza nyumba ya familia anaenda kuanzisha maisha na hawara anamuacha mke huku hana kazi wala kipato na watoto anawalea mke peke yake. au ndo mnateteana ujinga.
 
Ubaya wa hii feminism inawaaminisha wanawake kuwa wanajiweza bila uwepo wa mwanaume.
 
Sijui dunia ya wapi hiyo. Wajane wanaachwa peke yao baada za wiki 2 za msiba wabebe misalaba yao wenyewe. No one cares. Kila mtu yuko busy na familia yake.
Nashikwa na hasira kwasababu watu wanataka kufanya tuone kama maisha ni marahisi saana na wanaamini dhana zao wao ni halisi na za wengine ni za kutunga. Wajane wanakuja kutulalamikia kila siku ofisini jinsi ndugu walivyowatelekeza na watoto, mali za mume wamechukua. Na mara nyingi unakuta mume alikufa intestate mali wanazibeba kaka zake wanasema mwanamke haruhusiwi kuwa na mali wanasahau kuwa kaka yao alikua na watoto.

Majitu yanakuja kushupaza shingo hapa as if the world is full of butterflies yaani. Very stupid set of ignorant men
 
Aisee wewe ni much know halafu mbele kiza.
Mwanamke sababu ya kujipambania sio kwasababu mwanaume alimnyanyasa,kuna sababu nyingi za mwanamke kupambana na pia nj vizuri mwanamke kupambana,sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1)Hali ya maisha ya kwao alikoanza kuishi,wengine toka wadogo wameanza kupambania maisha yao,mfano mamaangu mzazi,alianza kazi akiwa mdogo huku anasoma,maaba hakukuwa na mtu wa kumuunga mkono na babu alifariki ye akiwa mdogo sana.
2)Kujitegemea kwaajili ya matumizi binafsi na maendeleo binafsi,hili pia mwanamke linaweza mfanya apambane,na wala sio jambo baya maana wanawake mna mahitaji mengi mengine madogo madogo huwa mnaona ni sahihi mjitimizie wenyewe.

Kiufupi jambo la mwanamke kupambana sio baya,ila je anapambana kwa namna gani na kwa mazingira gani??
Je unataka kusema wanawake wenye pesa hawanyanyaswi!!??
Wapo wanawake wenye pesa na wananyanyaswa vile vile.

Haki sawa kwa wote ilikuja kwaajili ya kumpa mwanamke nguvu ya kuweza kujitetea,na kujitetea huko sio kwa pesa,bali kwa kupewa usawa sawia na wa mwanaume kimaamuzi,kiajira n.k n.k ikienda sambamba na sheria za kumuwajibisha mwanaume ataemnyanyasa mwanamke.
TAMWA na TAWLA ndio moja wapo ya vyombo vinavyotekeleza hilo.

Akili yako inajijengea kuwa mwanamke anapambana kwasababu alipitia manyanyaso hapa unakosea.
Tatizo lililokuwepo hapa hili suala la haki sawa kwa wote limewafanya mjisahau ninyi ni kina nani.
Asilimia 90 ya wanawake wa siku hizi mnajifanya wajuaji,hamtaki kuelekezwa na wala hamtaki kuongozwa.
Mwishowe mnaishia huko mnakoishia.
Point kuu narudia pale pale msijisahau ninyi ni kina nani katika jamii.
Licha ya kipato jitambueni na mplay role yenu kama wanawake katika jamii.
 
Antidepressants ndio dawa za nn mkuu
 
Sasa suala hili na feminism wapi na wapi!?
Tena usikute waliodhulumu hizo mali za marehemu na kumtenga mjane ni MAMA WA MAREHEMU na DADA ZAKE wakiwemo,na hao pia ni sehemu ya wanawake pia wamemdhulumu mwanamke mwenzao.
Kwani haifahamiki katika familia kuwa ndugu wa mume wenye matatizo mara nyingi ni mama mkwe na mawifi!??
Inaonekana huelewi nini unakitetea hapa.
Hii kesi na mada husika ni irrelevant kabisa.
 
Uhalisia ni kwamba sio afrika tu mimi huwa napita huko Twitter kwenye page za wazungu huko mbele wanaowapa makavu mafeminist wanapost video nyingi sana za mabinti Generation Z na hata millennials wakiwa wanaongea wenyewe kwenye video post wakilaani sana mafeminist kuwaharibia future kwann hawakujisemea wao kama wao hadi wakawasemea generation ambayo sio yao na matokeo yao wao ndio wanakuja kuteseka kujitafuta na kutumia 90% ya income kulipa bills plus wana madeni ya mikopo ya chuo na life ni gumu sana wanakosa muda wa bata.

So unachosema sio kwa afrika tu ni duniani kote especially Western countries ingawa kwa mataifa kama urusi, Asia na uarabuni sio sana sababu wanaendesha maisha yao kitofauti sana ila sisi wazee wa kugeza ndio wanawake wetu wamekalia kuti kavu. Bills wanalazimika kujilipia wanaume wamepunguza kuoa na siku zinavyozidi kwenda alot of unmarried women rate inaongezeka of which watakuja teseka baadae umri wa utu uzimani maana watakuwa ni wao pekee yao.

Walishazoea wakifika umri huo wanategemea mirathi, au hela mafao za mwanaume kufanya maisha sasa kwa life hili la bongo, cost zilivyo juu, mtu hana mume wa kusapotiana nae, hana mafao, hawezi danga mwili umeshachakaa, wataishi vipi, kwa kutegemea watoto wao, na hao watoto nao wanaishi vipi sasa na wana majanga yao? [emoji848]
 
Saizi unarudi tena kwenye point yangu.

Sasa kama mnajua sababu za wanawake kujipambania na mnajua kwamba hata wanawake wenye pesa wananyanyaswa kwanini mnaruhusu wenzenu wakashfu wanawake kuwepo makazini?

Ni labda wewe ndo unaenda kama kipofu au vipi. Wenzako wanasema
Lengine wewe unaongelea lengine. Mimi na deal na hao wanaosema mwanamke anatakiwa akae nyumbani kwasbabu ni nature. Hapo ndo nnapotamani kulipua bomu humu. Wewe umesema sababu za mwanamke kupambana. Wenzio wanasema mwanamke ameumbwa akae nyumbani. How pathetic. Waelezee na wengine hizi sababu tufunge huu mjadala. Otherwise tutabishana hadi asubuhi
 
Hizo nyakati nadhani zimeshawadia. Kwasasa mwanamke mwenye pesa ndio kigezo cha mke mwema sababu hata yeye akiingia kwenye ndoa anapambania sana kumtuliza mwanaume maana kupata mwanaume wa kitulia nae ni kazi ya ziada.
 
Wewe kweli utakuwa na PTSD kama alivyosema mchangiaji m'moja hapa, hii sio kawaida kabisa. Upo so obsessed na wanaume wa hovyo as if ulishawahi kuishi nao.

Wenzako wanaongea wanachokiona na wanachokipitia wewe upo busy kuongelea unachohisi na unachodhania kuwa kitatokea. Wewe ni changamoto sana masikini ya MUNGU.
 
Narudi sasa kwenye point.
Wanakwambia mwanamke anatakiwa akae nyumbani alee watoto. That means hakuna kipato anachoingiza anasubiri cha mume. Akifiwa na mume wake hao ndugu no matter ni mashemeji au wamama wanakuja kumpokonya hizo mali wanasahau kwamba hakuwa na kazi so mnategemea ajipange lini ili aanze kutafuta ela kwa ajili ya watoto wake. Na muda wote mume alikua anatembeza kengele jamii forum anakwambia mwanamke ameumbwa kukaa nyumbani tu. Yani mnachefua

Kama mume angemruhusu huyo mwanamke afanye kazi hata hizo mali zikipotea mwanamke anakua na pa kuanzia. Sijui ata kama mnaelewa.
 
Ubaya wa hii feminism inawaaminisha wanawake kuwa wanajiweza bila uwepo wa mwanaume.
Wanajiweza wapi kenge wahid hawa!?
Kama wanajiweza kwanini waombe usaidizi?
Umenikumbusha nina mdogo wangu wa kike anamaliza chuo mwaka huu,ni much know,haelekezeki,haongozeki ukimuuliza kisa kasoma na yeye anaelewa mambo yanaendaje.
Mwishowe akiyabumburuwa anakufata wewe wewe kaka yake aliyekuambia hana shida ya support yako ili umsaidie.
Ujuaji mwingi unawapotosha.
Kama huyo mdada hapo juu,imagine anakwambia sababu ya mwanamke kupambana ni kwasababu wanaume tulikua wanyanyasaji.
Yani kakariri nadharia ambazo ni nje ya uhalisia,yote ni matokeo ya ujuaji mwingi kisa shule walizoenda.
Kwani bibi zao walikua hawalimi na kufuga kutengeneza kipato?
Je walisahau nafasi zao kama wanawake katika jamii?
Je kulima na kufuga sio njia mojawapo ya kupambana mkuu!?
 
Mimi naongelea kitu ambacho kipo na nimekiona kwa ndugu sasa kwanini mkatae wakati nyinyi pia mna share experience zenu. Umesema wenzangu wanaongea wanachokiona sasa kwanini na mimi nisiongee ninachokiona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…