Context yako ya mwanaume kutaka mke wa kukaa nyumbani tu ni tofauti na context yetu wanaume kutaka mwanamke akae nyumbani.
Wewe unatazama kama mwanaume anataka mke akae tu kama msukule sababu haujui hata wanaume huwa wanalenga program gani kwa wake zao wakiwa nyumbani.
Mimi huwa nakuwapo nyumbani muda mwingi but i have my ways kumake money ambazo hata mwanamke wangu namtrain na anazimudu so ananisaidia hata nikuwa sipo hapa mjini. So kuna module ya maisha mwanamke anaweza ishi na akatengeza milioni 3 akiwa home yaani ile most of the time unamkuta home.
Mfano tunafuga kuku shambani huko ila hapo home ndipo tunawahifadhi kwenye mafriza na wateja wanakuja kuwachukulia hapo na amesomea accounting anatunza vitabu vya biashara zetu ila hatoki home yupo muda wote anarelax anatazama tv, anakula Netflix, anapika chakula nakuja kula narudi kitaa naendelea na harakati. Na tukipiga total ya mapato tunatengeneza zaidi ya milioni 4.5 kwa mwezi, shida inakuwa wapi?
Sasa wewe sababu ya kukosa kwanza exposure ya mahusiano, maisha ya ndoa, hujui vitu unaishia kutunga tunga unachokiona ni mwanaume akisema mke abakie home unaona mwanamke anaeteswa, amefunguwa kwenye chumba na kufuli, jamaa akirudi anamtandika bakora, anamuua halafu anamuua tena ana mfufua, yaani unaona maangamizi tu[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio maana nakwambia wewe unamatatizo ya akili na haya matatizo yatakuja kukupeleka direction ambayo sio yako. Endekeza tu hizi ligi, maneno yanaumba, ukikiwaza sana kitu kinakuja kukutokea maana si unakiita na mawazo yako?