Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Kijana kamkimbia mchumba wake alietaka kumuoa baada ya kujua kwao kuna walemavu ni sawa?

Asingemwambia angefanya namna yeyote waachane! Ingekua Mimi hapo
Ningeextend mda wa uchumba labda kama tulikubaliana tufunge ndoa 2024 mwezi wa pili ningemwambia tufunge ndoa 2026 mwezi wa 11

Ningetengeneza matukio fake yatakayoonesha napitia kipindi kigumu Sana hali inayohitaji niwe mbali kidogo au inanitenga na Watu

Kwa sababu tulishakua kwenye uchumba ningekua najua hapendi nini na udhaifu wake upo wapi basi ningecapitalize mule mule mpaka ajiongeze
 
But kuna ulemavu huwa unakuja bila genes kuwa involved, mfano ajali, magonjwa makali ambayo huweza athiri mfumo wa umeme na mtu akapooza aidha viungo au mwili mzima, etc.

Sasa anaweza dhania anakwepa huko halafu mikosi ikamrudia yeye kwa namna nyingine kabisa halafu wakakutana na huyo binti akiwa na watoto wakubwa tu ambao hawana shida.
 
Hujafa Hujaumbika .....huku kwetu Kuna maza jirani yake kulikuwa na Albino ......so yule Kwa yule maza wale watoto albino wakija pale kwake kucheza ....

Wakila chakula ...vyombo alikuwa anavitenga + kutupa

At the end of the day....naye kapata mimba ....kuzaa mtoto ni albino

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Kudadadeki, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] apate sasa ile feeling ya kutenga vyombo akidhania ualbino unaambukiza?
 
Misemo ya "Hujafa hujaumbika" ni kuhalalisha matatizo yasiyo na ulazima.

Kijana kafanya vyema sana kuepuka balaa la mbeleni.

Ninyi mnao komenti ushubwada hapa wa hujafa hujaumbika, Huyo kijana akipata mtoto mlemavu mtamsaidia kulea?
 
Hujafa Hujaumbika .....huku kwetu Kuna maza jirani yake kulikuwa na Albino ......so yule Kwa yule maza wale watoto albino wakija pale kwake kucheza ....

Wakila chakula ...vyombo alikuwa anavitenga + kutupa

At the end of the day....naye kapata mimba ....kuzaa mtoto ni albino

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Chai..[emoji477]
 
Mnaodai jamaa hayupo sahihi hampo sahihi, kuna koo zina malaana mnyororo ukiingia kichwakichwa unaunga tela, Ndo maana tunaambiwa kabla ya kuoa tufuatilie background za hawa mabinti. Shauri yenu na shingo zenu ngumu
 
Jamani, hadi huruma.
Kwa nchi za wenzetu hizi shida wanazigundua tangu mtoto akiwa tumboni. Wanafanya genetic testing kama kuna tatizo wewe mwenyewe utaamua uendeleze ujauzito au lah.

Rafiki yangu yupo Marekani huko kaolewa. Akawa mjamzito akafanyiwa hivo vipimo akaambiwa mtoto wake ana shida kuna mawili mimba itaharibika au baada ya kujifungua mtoto hatamaliza masaa 24. Akawabishia akaamu kuendeleza ujauzito japo walikuwa wanamsumbua kila mara kumshauri atoe.

Kweli alibeba ile mimba full term akajifungua na kweli yule mtoto hakumaliza hata masaa manne akafariki. Aliumia sana.
Afrika wangesema kalogwa...[emoji1]
 
Ukiachana tu changamoto za kumlea, naamini kama mzazi kila ukimtazama unajisikia uchungu sana kwakuona kwamba anateseka bila makosa.

Mwaka jana mwanangu wa kiume wa 3 kuzaliwa, 5 years alipata changamoto ya mifupa ,serious bactrial infection kwenye mfupa mkubwa wa mguu karibu na goti. Ilikua ni ishu sana.. alikua halali usiku hospital kutwa kicha kakunja mguu analia sanaa .

Daktar alinambia kitaalam hapo maumiv anayoyasikia ni kama upigwe panga kwenye mguu.. aisee acha tu, mbaya zaid wakasema kuna uwezekana ikatokea eneo la maungio ya mifupa gotini ikaathirika na mguu ukashindwa kukua hivyo kubaki na mguu mfupi mmoja na kuwa mlemavu...

Aisee...usiku akilala mwanangu nilikua nikimtazama machozi yananitoka nalia peke yangu. 🥲🥲.
NIkawa namwambia Mungu naomba kama inawezekana hii hali ihamishie kwangu, mwanangu bado mdogo sana kwa haya maumivu.

It took us 4 months with alot of money mpaka dogo kuja kukaa sawaa.
Alikua anapigwa doz nzito za antibiotics kias kwamba leo hii hiv vi antibiotics vya kawaida akinywa anapoumwa kawaida tu, huwa ni kama havifanyi kazi.

Daktar alinambia it will take time mwil kurud sawa toka usugu wa madawa..

Kuwa mzazi ni kaz sana Mungu atusaidie wazaz na walez wotee.
Intelligent businessman we endelea tu kupiga selfie dogo [emoji23] haya mambo sidhan kama utayaweza
Aisee, pole sana mkuu mbona mnatoa shuhuda nzito sana
 
Binafsi mimi naona kijana kakosea, hakuwa sahihi, mkasa huu hapa nawapeni.

Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Hapa sasa nitaongea zaidi kama yeye mwenyewe alivyojitetea, ndipo penye kuamua kazingua au lah, twendeni pamoja.

Kijana ni kama alipata mstuko akataka kumuacha binti kienyeji ila alishindwa, ikabidi amuweke wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, alimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata ulemavu muda wowote maana hujafa hujaumbika, pia mtu yoyote anaweza kupata mtoto mlemavu maana hakuna anaemuumba mtoto atakavyo lakini yeye anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi endapo wao wakipata mtoto kwa kuhofia kwamba ulemavu wa wanafamilia ni magonjwa ya kurithi, hivyo hata kama binti ni mzima yawezekana karithishwa genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu, sababu ya zaida ambayo hakumwambia binti ni kwamba anahofia kuna mambo ya kiafrika kwenye mila au matambiko yaliyowahi kudanyika huko zamani yanarithishwa,

Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.

Je, ni sawa?
Uliona ukisema wewe ndo umemkimbia huyo binti tungekushambulia sana?? Anyway mrudie tu huyo binti
 
Kwa useful was story hii inaonyesha dhahiri muhusika ni wewe. But naona ni sahihi tunashauriwa kufanya ata vipimo ili kupunguza chances za magonjwa ya kurithi pia kama circle cell, magonjwa ya akili n.k. Kama unaona dhahiri kuna hatari hakuna haja ya kujiingiza. Nashangaa mabinti wanaoolewa na Manara wakimuona kabisa ni Albino. Wanaxhojisifia kwamba Manara anazaa watoto weusi, hawajui kwamba Manara anagenes za Ualbino kwa hiyo ata kama yeye hatozaa watoto Albino kizazi kitarudu kwa wajukuu wake na kusabahisha majutto.
Niliwahi kusikia Manara huwa anachukua tahadhari kupima wenza wake kama nao wana genes za albinism kabla ya kufanya maamuzi ya kuwa na watoto.

Ikitokea wote wawili mna hizo genes kuna uwezekano mtoto akapata albinism ama akabena genes za albinism,
 
Binafsi mimi naona kijana kakosea, hakuwa sahihi, mkasa huu hapa nawapeni.

Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.

Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.

Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi

Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.

Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.

kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.

Hapa sasa nitaongea zaidi kama yeye mwenyewe alivyojitetea, ndipo penye kuamua kazingua au lah, twendeni pamoja.

Kijana ni kama alipata mstuko akataka kumuacha binti kienyeji ila alishindwa, ikabidi amuweke wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, alimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata ulemavu muda wowote maana hujafa hujaumbika, pia mtu yoyote anaweza kupata mtoto mlemavu maana hakuna anaemuumba mtoto atakavyo lakini yeye anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi endapo wao wakipata mtoto kwa kuhofia kwamba ulemavu wa wanafamilia ni magonjwa ya kurithi, hivyo hata kama binti ni mzima yawezekana karithishwa genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu, sababu ya zaida ambayo hakumwambia binti ni kwamba anahofia kuna mambo ya kiafrika kwenye mila au matambiko yaliyowahi kudanyika huko zamani yanarithishwa,

Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.

Je, ni sawa?
Mjifunze kuwa na mipaka. Ana uhuru kufanya maamuzi yoyote anayotaka cha msingi hajavunja sheria za Nchi. Watu kama nyie hampo huru kiakili wala kimaisha. Mimi leo naweza kumuoa binti yako na kumuacha kesho na wala nisikose usingizi na siyo kwamba na roho mbaya bali najua umuhimu wa maisha yangu.
 
Kwanz huyo bint wa miak 22 mwaka huu na alimalz degree mwak jan alisom ndan ya Taifa letu , maan bachelor alimlz na 21[emoji2]

Mimi naona jamaa amefany maamuz sahihi kbsa na amewez kutoa maelekezo fasaha
Tatzo la sis nikuzchanganya hisia na akil zfanye kaz kwa PAMOJA [emoji3055][emoji4]

Mara mia uremavu wa viungo ila uremavu wa akil ambao ni genetically hapn labda uwe umetokea kwenye process ya kuzaliw (mtoto kucmama kweny njia cvx to vagin muda wa kutok na kupelekea kukosa oxgen kupelekea hali hyo au mtoto kukosa maziwa halis ya mam pind tuu amezaliwa.
 
Back
Top Bottom