Kiti cha Rais Samia kanisani Vs Rais Ruto kanisani Homa Bay, Kenya

Kiti cha Rais Samia kanisani Vs Rais Ruto kanisani Homa Bay, Kenya

Badala ya kujadili jinsi watanzania wanavyoumizwa na utawala wa Samia kupitia matozo mnajadili kiti cha Rais kanisani?

Hivi mmeishiwa na akili kabisa hadi mnajadili viti vya Rais kanisani au msikitini?

Hivi mmesahau kuwa hizo ni itifaki na mambo ya kiusalama?

Hivi tunaacha kujadili jinsi utawala wa huyu mama unavyoacha wananchi wateswe na mifumuko ya bei na matozo ya kijinga kijinga mnapoteza muda kujadili kiti cha rais kanisani?

Unahitaji kuwa akili haipo kabisa yaani umefilisika kabisa ubongo wako umebakia na juisi tu ndo ujadili kiti cha Rais kanisani

Tunapoteza muda kujadili upumbavu na ujinga usio na mantiki huku tukiacha mambo ya msingi
 
Yote yana umuhimu, ya tozo yanatokana na Rais kuwa kama Mungu (ya kupelekewa kitu kanisani) na hivyo kuwa juu ya sheria. sasa Rais anakuwa juu ya Kanisa!
 
Achana na wajinga hao mbona Askofu au padri ana kiti chake tofauti na waumini? Papa mwenyewe alitembelea Tanzania mbona alikuwa na kiti spesheli?

Labda wajibu kwa nini padri au Askofu.ana kiti specheli na kwa nini yeye huwa anakula mkate na kuteremshia na divai wakati waumini wengine kanisani wanaowasalisha wanapewa mkate peke yake wameze kwa kutumia mate yao? Kadivai ana enjoy padre au Askofu peke yake ndie anadudumia

Huo ni utaratibu wa ibada zao, je rais kuingia na kiti chake ni sehemu ya ibada yao?
 
Huo ni utaratibu wa ibada zao, je rais kuingia na kiti chake ni sehemu ya ibada yao?
Hujui Biblia inatanka wazi astahiliye heshima anastahili heshima kubwa

Heshima inaanzia kuanzia mapokezi atakapokaa ,atakachokula ,atapolala nk

Raisi ni mtu mwenye heshima kubwa huwezi m treat kama mtu wa kawaida

Mlitaka kumfanyaje mbona mnakomaa? AFTER All yeye na Makamu sio waumini wa hapo kanisani kwenu Bukoba walikuja kama wageni wa heshima wana makanisa yao Parokia au misikiti wanakosali Hawako kigango chenu au jumuiya ya kwenu!! Wamesafiri kuja kama wageni wa heshima tu huwezi kuwaweka kundi moja na wanywa Rubisi wa Kagera
 
Sio kweli, wakimpangia kuingia na viatu msikitini ataingia navyo?
Hawawezi kumpangia hivyo !! Kwani kiti cha Rais hakiruhusiwi kuingizwa kanisani ? Nadhani kimeingizwa kwa ruksa ya hapo kanisani na wamekubali kwa sababu hawakuona ubaya wowote ! That's My take lakini sina hakika !
 
Hivi ni Rais wa Tanzania tu ndio huwa anatembea na kitu chake maalum au marais wote??
Huwa sioni hata POTUS akiwa anatembea na kiti chake maalum!
Wamarekani wanatembea mpaka na shuka za vitanda!! Tulishuhudia alipokuja Obama !! The Beast ndio haisahauliwi kabisaaa!! Gari la mkulu wa dunia !!
 
Alipoenda UK alienda na hicho kiti chake?
Masuala ya ulinzi wa Rais ni mengi na magumu pia na yanaweza yakabadilika wakati wowote kulingana na hitajio la wakati husika na mahali popote pale !! That's my take!!
 
Hujui Biblia inatanka wazi astahiliye heshima anastahili heshima kubwa

Heshima inaanzia kuanzia mapokezi atakapokaa ,atakachokula ,atapolala nk

Raisi ni mtu mwenye heshima kubwa huwezi m treat kama mtu wa kawaida

Mlitaka kumfanyaje mbona mnakomaa? AFTER All yeye na Makamu sio waumini wa hapo kanisani kwenu Bukoba walikuja kama wageni wa heshima wana makanisa yao Parokia au misikiti wanakosali Hawako kigango chenu au jumuiya ya kwenu!! Wamesafiri kuja kama wageni wa heshima tu huwezi kuwaweka kundi moja na wanywa Rubisi wa Kagera

Heshima inaanzia kwenye kuheshimu uchaguzi, kama unapata madaraka kwa kunajisi uchaguzi heshima unaitakaje? Mungu hadhihakiwi.
 
Masuala ya ulinzi wa Rais ni mengi na magumu pia na yanaweza yakabadilika wakati wowote kulingana na hitajio la wakati husika na mahali popote pale !! That's my take!!

Hamna kitu Boss, ni kutaka ufahari usio na sababu yoyote. Kwangu mimi najua heshima halisi inatokana na kuingia madarakani kwa kuheshimu uchaguzi. Lakini kwa zile chaguzi za kihayawani sijui wanataka ufahari wa nini.
 
Busara! maana yake, kutenda kistarabu.
Litendwe mahali pake, mipango usiharibu.
Kuna pale utamke, pengine ubaki bubu.

Sasa watanzania tunaelekea ujingani kwa kasi isiyomithilika.tumezaa kizazi kisicho na vipaumbele wala malengo.
Tuko kwenye wakati ambapo kila mmoja anadhani anaweza aidha kuwa kiongozi au mwanasiasa bila hata uelewa au elimu ya siasa yenyewe.

Tumegeuza simu janja kuwa madarasa ya kueneza kila tunachoamka nacho kichwani bila tafakuri ya upana na umuhimu wake kwa jamii au madhara yake kwa jamii.

Tuna kizazi cha ubinafsi na unyang'au wa hali ya juu kupitia mgongo wa siasa,wakati kinachoendelea sio siasa bali uhasama baina ya pande mbili zinazogombea ulaji.

Huku wananchi tukionekana kama mazombi tusiojitambua mbele ya wao wajiitao wasomi lakini wasio na uwezo wa kupenya ajira za kimataifa,sambamba na wasomi wenzao huko Duniani.
Badala yake wanarudi kutafuta short cut kupitia siasa uchwara za kibunge.

Inapofikia wanaojiita wanaharakati kushindwa kujenga hoja nzito zenye mashiko na maslahi mapana kwa wananchi.
Na hivyo kuibana serikali na watendaji wake kuwajibika ipasavyo.kuendana na katiba ya JMT,pamoja na viapo vyao.

Badala yake ...
Tunarudi kujadili hoja ya kiti cha Rais kanisani......

Huku sio tu kuporomoka kisiasa,bali ni kubomoka kisiasa.
Wewe Erythrocyte ukiwa chawa ndani ya jengo linalobomoka kwa kasi.
 
Yote yana umuhimu, ya tozo yanatokana na Rais kuwa kama Mungu (ya kupelekewa kitu kanisani) na hivyo kuwa juu ya sheria. sasa Rais anakuwa juu ya Kanisa!
Huu ni ujinga umecomment unazijua itifaki za usalama kweli wewe
 
Huu upinzani wa kupinga kila jambo sasa nimeanza kuona unakengeusha akili, na kufubaza uwezo wa kufikiri, vyema wawe wanajipa muda wa kutafakari kabla ya kutoa maoni yao.

Naamini hii ni tabia ya kawaida kwa mwanadamu, kama umeizoesha akili yako kuona mabaya pekee ya upande fulani, basi hata likitokea jambo la kawaida kwa wengine, kwako litaendelea kuwa baya tu.

Lema kwa kuonekana kwake kuyajua maandiko ya kwenye biblia, sikutarajia aje na maneno yale ya kupinga lile jambo lililotokea kanisani, ule sio uwanja wa mashindano ya mambo ya ulimwengu - CCM vs CDM, ile ni nyumba ya mambo ya rohoni.

Hii ingemtokea kama angejua kutenganisha siasa za CCM vs Chadema, kwenye eneo tofauti na uwanja wa siasa, pale Rais alikwenda kama kiongozi wa mamlaka ya nchi, ambapo tunaaswa na maandiko tuziheshimu mamlaka zilizo juu yetu.

Hivyo binafsi sikuona sababu ya kugombania viti, hayo ni mapambo ya huu ulimwengu yasiyo na maana kwa mkristu aliyekamilika, ni wakati wa wapenzi na wanachama wa vyama vya siasa kutafakari mambo badala ya kupelekwa mbio na fikra za viongozi wao.
 
Back
Top Bottom