Busara! maana yake, kutenda kistarabu.
Litendwe mahali pake, mipango usiharibu.
Kuna pale utamke, pengine ubaki bubu.
Sasa watanzania tunaelekea ujingani kwa kasi isiyomithilika.tumezaa kizazi kisicho na vipaumbele wala malengo.
Tuko kwenye wakati ambapo kila mmoja anadhani anaweza aidha kuwa kiongozi au mwanasiasa bila hata uelewa au elimu ya siasa yenyewe.
Tumegeuza simu janja kuwa madarasa ya kueneza kila tunachoamka nacho kichwani bila tafakuri ya upana na umuhimu wake kwa jamii au madhara yake kwa jamii.
Tuna kizazi cha ubinafsi na unyang'au wa hali ya juu kupitia mgongo wa siasa,wakati kinachoendelea sio siasa bali uhasama baina ya pande mbili zinazogombea ulaji.
Huku wananchi tukionekana kama mazombi tusiojitambua mbele ya wao wajiitao wasomi lakini wasio na uwezo wa kupenya ajira za kimataifa,sambamba na wasomi wenzao huko Duniani.
Badala yake wanarudi kutafuta short cut kupitia siasa uchwara za kibunge.
Inapofikia wanaojiita wanaharakati kushindwa kujenga hoja nzito zenye mashiko na maslahi mapana kwa wananchi.
Na hivyo kuibana serikali na watendaji wake kuwajibika ipasavyo.kuendana na katiba ya JMT,pamoja na viapo vyao.
Badala yake ...
Tunarudi kujadili hoja ya kiti cha Rais kanisani......
Huku sio tu kuporomoka kisiasa,bali ni kubomoka kisiasa.
Wewe
Erythrocyte ukiwa chawa ndani ya jengo linalobomoka kwa kasi.