voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Kabla hujaandika naomba uwe una jaribu kuvuta kumbukumbu kidogo!Uko sahihi sana, lakini mamlaka zinazopaswa kuheshimiwa ni zile zinazoingia madarakani kwa njia halali. Kwa uchaguzi ule wa 2020 ni ngumu baadhi ya watu kutoa heshima kwa hizo mamlaka za juu.
Mimi kwa mtazamo wangu sikuona umuhimu wowote wa rais kutumia kiti chake binafsi ndani ya kanisa kwani ni kujipa ukuu asiostahili, hasa ukizingatia namna yeye na chama chake walivyoingia madarakani.
Halafu hili neno kupinga kila kitu naona linatumika ndivyo sivyo, na sababu hasa ni kurudiwarudiwa kila mara. Sijawahi kuona watu wanapinga ujenzi wa shule, barabara, huduma za maji nk. Ama huenda hizo shule, barabara nk sio sehemu ya kila kitu.
Ni kwamba...Chadema kupitia mgombea wao wa urais ndugu Lissu!...2020,alitamka wazi kwamba "chadema hawataki maendeleo ya watu na sio vitu"
Nini maana yake hiyo?