Kuwa single mother siyo laana, msiwaseme vibaya
Umeongea Kwa details na feelings, nimekuelewa...
Lakini bado umeweka wanaume kama wao ni malaika.
Mtaani wanawake wengi wanasema wanaume huwa Wana tabia ya kuomba "nizalie mtoto" .
Ili ku prove Kama wanapendwa...
So wanaume wa hivyo pia husababisha idadi ya single moms kuongezekaa.
Tusiwanyooshee Sana mikono....factors ni nyingii
Kwahiyo kwa binti au mwanamke timamu mwanaume akikwambia nizalie na wewe unazaa tu kwasababu hauna akili timamu, akikwambia tembea uchi barabarani utatembea? [emoji848]
 
H
Nakubaliana nawe kwa 100 kabisa. Hao wapo tena wengi tu. Ila nimekua nikisema kila siku hapa, wanaume wa aina hii ni wasen ge na wanastahiri kuchomwa tu.

Ila mapenzi bana, eti nizalie nikupende zaidi jamani😂 na kuna binti wa mtu anajaa.

Niongezee na kundi lingine la wanaume wenye kujisifu anamtoto ili hali dogo anakaa either kwa bibi au kwa dem aliezaa nae dem anataabika kuhudumia alafu kenge mmoja anajisifia tu ana mtoto mkubwa. Nyaambaf
Hao nao tuwafungulie Uzi...
Tuwasimange hahaha.
 
Kwahiyo kwa binti au mwanamke timamu mwanaume akikwambia nizalie na wewe unazaa tu kwasababu hauna akili timamu, akikwambia tembea uchi barabarani utatembea? [emoji848]
Siyo hivyo...
Mapenzi Yana nguvu Sana...na mostly wanawake tunapendwa kudanganywa...
Only if mngeelewa...mnge waonea huruma.
 
Chanzo hicho hapo soma hiyo post ambayo si ya kutengeneza na video ipo kabisa kama ushahidi. View attachment 2988829
Huyu mtu mmoja hawezi kujustify chanzo cha single mother wote,

Kumbuka pia hata wanaume hua wapo wanaotaka wanawake wakuzaa nao tu,hata hapa JF zipo thread za hivyo,

Kuna single mother wamekutana na moto kwenye ndoa zao mpaka wakasalimu amri,the same na kwa wanume pia.
 
Huyu wa kwangu ni debe tupu asee,mwanaume timamu hawezi ishi naye,alafu suala la kugawa uroda kwake sio tatizo anaweza kuwapa wote ni nyie tu
Na asilimia kubwa wapo hivyo anakuwa na wanaume ili hatibu personal needs mwingine kwaajili ya kumkaza vizuri, the rest ni kwaajili ya kupewa hela kutatua shida zake
 
Huwa nasema mara nyingi humu,wako kama wamevurugwa akili,huwa wanaingia kwenye ndoa sio kuwa wamependa ni kwakua wako desperate na wanataka kuwaonyesha baba watoto zao kuwa na wao wanapendwa,ila utashangaa jamaa akija kumuomba mapenzi ya wizi anakubali...
hii ndio shida yao kubwa hawana msimamo anaweza kukuelezea kuwa mzazi mwenzake amemtelekeza, mara anampiga mara mchekupakaji cha ajabu anaenda kumpelekea mzigo
 
Umeongea Kwa details na feelings, nimekuelewa...
Lakini bado umeweka wanaume kama wao ni malaika.
Mtaani wanawake wengi wanasema wanaume huwa Wana tabia ya kuomba "nizalie mtoto" .
Ili ku prove Kama wanapendwa...
So wanaume wa hivyo pia husababisha idadi ya single moms kuongezekaa.
Tusiwanyooshee Sana mikono....factors ni nyingii
Hakuna mwanaume ambaye anataka mtoto alafu baada yakuzaa na huyo mtu wake akamtelekeleza mtoto labda kutokee factors nyingine kama vile mwanamke kutakuwa mwaminifu
 
Sasa wakubwa mnanishauri nini mim nina demu mmoja hivi naye ni alikuwa single mother ila mtoto alivo kua kua alichukuliwa na baba yake, sasa kwa hizi story zilizo pigwa hapa zinanichanganya 😐 demu yuko vizuri ila romantic yake nahisi siyo ya dhati kabisa kama vile anafanya tu kutimiza wajibu,, nifanyaje wakuu
Naomba mnielewe sio mtaalamu sana kwenye uandishi
Kwanini unasema romantic yake sio ya dhati? Ili tujue tunakusaidiaje
 
Hayuko serious kwenye mawasiliano nakuwa kama nalazimisha tu, yeye yuko chap tu kutoa ngada tu ila kuhusu mambo mengine ni kama nalazimisha very short answers kwa kila ninacho muongelesha
Basi huyo hakupendi achana nae Usije ukajuta huko baadae ukishaamua kumpiga chini mwanamke usimrudie tena hata akuombe msamaha kiasi gani huwa wanakuja kwa mission maalumu baada ya kufeli huko alipoona panafaa. Zingatia hiki nilichokwambia utanishukuru baadae
 
Basi huyo hakupendi achana nae Usije ukajuta huko baadae ukishaamua kumpiga chini mwanamke usimrudie tena hata akuombe msamaha kiasi gani huwa wanakuja kwa mission maalumu baada ya kufeli huko alipoona panafaa. Zingatia hiki nilichokwambia utanishukuru baadae

Nashukuru sana kwa ushauri
hapa inawezekana yupo tu kimkakati maana anasisitiza sana suala la kumuoa hana story nyingine zaidi ya hiyo
 
Shaloom,

Dada mmoja aliamini kuwa mtu pekee anayestahili kuitoa bikra yake ni mwanaume atakayemuoa. Huu msimamo wa bibie ulifanya apoteze wachumba wengi kwani walipoambiwa hawataonja asali mpaka waingie ndoani walisepa.

Miaka ikaenda, umri wa dada ukazidi kusogea ila bibie hakubadili msimamo wake. Aliendelea kuitunza bikra yake na kuishi maisha ya heshima kama ambvyo binti yeyote mwenye maadili anapaswa kuishi.

Walokole tuna kamsemo ketu kuwa, wakati wa Mungu ndio wakati sahihi na kweli "Wakati wa Mungu ulipofika" bibie akaposwa na kijana aishie huko Marekani. Kilichomvutia kijana kwa bibie ni habari alizozisikia kuwa bibie hajawahi kuguswa na mwanaume yeyote.

Kijana akatuma washenga, akatoa mahari na kufanya taratibu zote ikabakia ndoa tu ambayo ingefungwa baada ya yeye kwenda Marekani na kurudi tena Tanzania.

Basi ikawa rasmi kuwa bibie sasa ni mke mrarajiwa wa mtu aishie Marekani. Viongozi wa kanisa na wazazi wakawa wanamtumia bibie kama mfano wa kuwaasa watoto wa kike kuwa ukijitunza Mungu atakuletea mume bora. Mabinti wakaambiwa si mnaona mwenzenu kajitunza sasa anaolewa na kwenda kuishi Marekani?

Basi bwana siku za mume mtarajiwa kurudi marekani zikakaribia na akaomba aende Dar na mkewe mtarajiwa akamfanyie shopping pamoja na kumuachia mradi wa ujenzi wa jumba lao lililoko Dar ausimamie.

Kwa vile kijana alishafanya taratibu zote wazee wakaona haina shida wakamruhusu binti asafiri na mumewe mtarajiwa kutoka mkoani kwao mpaka Dar.

Kufika Dar wakashukia hotel na huko kijana baada ya kushindwa kumshawishi binti atoe uroda kabla ya ndoa akatumia njia ya kumlewesha na ndipo akafanikiwa kuitoa bikra ya binti kabla ya ndoa.

Dada alilia sana alipozinduka na kujua kikichotokea, ila kijana wa Marekani akafanikiwa kumtuliza dada kwa maneno matamu matamu na ahadi ya kumpenda mpaka kifo kiwatenganishe. Dada akafanyiwa shopping kisha jamaa akakwea pipa akarudi state na bibie akarudi mkoani kwao.

Baada ya week kadhaa dada akagundua ana ujauzito wa mumewe mtarajiwa. Wazee wakajua na kijana wa Marekani akajulishwa na kuombwa kufanya hima aje aoe mkewe na kuondoka nae kabla wambea hawajajua kuwa ile bikra iliyotunzwa kwa miaka mingi ishatolewa kabla ya ndoa.

Kijana wa Marekani akazipokea habari kwa furaha na kuwaahidi wazee kuja ASAP lakini mpaka muda wa mtoto kuzaliwa ukafika ila kijana wa Kimarekani hakutokea.

Baada ya miaka kadhaa ikaja kugundulika kuwa kijana wa Kimarekani alikua ni muhuni tu aliyekuwa na fantansy ya kuchakata bikra na eti hata wakati anatoa ile mahari alikua tayari keshaoa zake huko Marekani na wale washenga aliowatuma walikua ni wahuni wenzie tu wazee wa hovyo, maana wazazi wake wa kweli walipofuatwa walishangaa sababu wao wanajua kijana wao alishaoa siku nyingi tu.

Ikawa asubuhi ikawa jioni dada mrembo aliyeishi kwa maadili akajikuta akichukua kadi yake kwenye chama kubwa la single mothers nchini.

Chama ambacho wanaume wa Kitanzania huwaona wanachama wote wa chama hicho ni wanawake wasiofaa sio kuoa tu bali hata kwa mahusiano ya kudumu, bali kwa kuwagonga na kukimbia haraka uwezavyo kuokoa maisha yako.

Kabla sijajiunga JF nilikua nawaona single mother ni wanawake kama wanawake wengine. Wako wanaojitambua, wako empty sets. Wako wanaojiheshimu, wako micharuko. Wako wapole na wanyenyekevu wako vichomi pia. Inshort tabia zote za wanawake single mothers utazipata hata kwa wanawake wasio single mothers.

U single mother sio laana ambayo automatically inamfanya mwanamke awe na tabia za hovyo kama hakua hivyo mwanzo na wala kutokuwa single mother sio baraka/neema/kinga ya kumfanya mwanamke awe wa maadili/bora.

Mwanamke yeyote single mother or not, tabia zake zinatokana na malezi au mtazamo wake katika maisha.

Mimi sio single mother ila as long as mim ni mwanamke kama ilivyokuwa kwa bibie mtunza bikra, hata mimi iko siku naweza kuangukia kwa bazazi nikalielewa tukadanganyana danganyana pale at the end of the day bila kujua imekuwa kuwaje nikajikuta na mimi nachukua kadi kwenye chama kubwa la single mothers.

Ikitokea nimekua single mother sitapenda kuongelewa kwa namna single mother wanaongelewa hapa JF.

Hapa JF single mother wanaongelewa kama jamii ya watu wenye laana wanaopaswa kutengwa kama walivyotengwa wale wakoma wa kwenye biblia.

Hapa JF wanaume mnawaongelea single mothers kama viumbe wasio na akili wala maadili, lakini naomba niwaambie hawa single mothers ni nyie mmewatengeneza na tena ni kundi la wanawake wenye akili kubwa na ndio maana wanaweza kulea na kusomesha watoto wao ambao baadhi yenu mmewakataa na kuona ni bora hela yako ununulie msambwanda wa barmaid kuliko kununua daftari za mwanao.

Sio ajabu yule kijana wa Marekani nae yuko hapa JF akiandika nyuzi za kuwaongelea single mother kama walaaniwa kumbe yeye ndio mlaaniwa.

Naombeni wanaume wa JF mtoe hiyo lebel mliyowapachika single mothers, sio sawa duniani wala mbinguni sababu hamjui mwanamke amepitia mitihani gani mpaka kuishia kuwa single mother.

Naomba viongozi wa JamiiForums muliangalie hili. Kuna single mother anaweza kujiua akifikiria aliyopitia na kulinganisha namma jamii inavyomhukumu. Sio sawa jamii kusema watu wote wa kundi fulani wana tabia fulani kwani hiyo sio kweli na sio sawa.

Iweje mwanamke aliyeishi maisha yake yote kwa kujitunza na kujiheshimu halafu badae jamii imuone takataka kisa tu analea mtoto/watoto wake bila baba?

NB: Wanawake wa JF njooni tuwaeleweshe wanaume wetu kwa heshima na upendo kuwa kunyanyapaa single mothers sio sawa. Maana kama leo sio single mother kesho unaweza ukajikuta single mother au binti yako akawa single mother. Utapenda anyanyapaliwe?

Hata wewe mwanaume unayenyanyapaa single mothers leo huwezi jua iko siku wanaume wenzio watamdanganya aishie kuwa single mother. Utapenda jamii imnyanyapae?

Hivi kweli Yule wife nilieachana naye miaka 10 iliyopita anafaa kweli? Aisee single Mama wote hawafai, Sababu?

1. Wanaume wote waliomdanganya akaacha ndoa yake walimuibia mali alizopata kwenye Talaka, wakamuacha.

2. Nataka niwaambieni ukweli, siwezi lala naye kabisa, ni misimamo tu ya kikwetu. Ila nikitaka nampata dakika hii!

3. Msicheze na hizi ndoa, kilio na madhara yake ni Magumu sana sana. Huo ndo ukweli na waambia
 
mnaonekana ni mijitu ya hovyo tuu, wengi humu wamelelewa vizuri na hao mnaowaita singo maza na wengi wamewazidi maisha, pelekeni stress zenu chooni
Hakuna kitu kama hicho. Watoto wa single mother huwa ni changamoto.
 
Back
Top Bottom