Kuwa single mother siyo laana, msiwaseme vibaya
Mwanaume halalamiki mjitunze bali tunawaonya mjitunze maana athari ni kubwa kwenu sio kwetu. Tulalamike kwani sisi tutapungukiwa na nini, mnaonywa ila hamsikii. Wanawake ndio wanalalamika kutokuolewa kwakuwa ni single mothers. Mtu atalalamikaje kitu anachopata faida nacho. Ila mwaonywa, kwasababu the truth is, ujitunze usijitunze mwanaume hatapungukiwa na kitu maana wapo watakaojitunza. Mnaonywa mjitunze ili kupunguza haya malalamiko yenu sijui ya jamii kuwatenga na kuwalabel vibaya, mwanaume alalamike wewe kutokujitunza kwani anayeshirikiana kukuharibu sihaohao wanaume wasio na hekima. [emoji23][emoji23][emoji23] swala ni very subjective maana huishi kwakufuata mkumbo wa jamii bali unaishi kwa malezi na maadili uliyofundishwa kutoka kwa wazazi yakiongozwa naakili zako. Ishi kwakufuata mkumbo wa jamii uzidi kuona single mums watakavyozidi. It's your life, your choices, no one will ever die with you or for you.
Hapo kwenye jamii kumlabel vibaya mwanamke ndipo exactly point ilipo kwanini wanaume wawalabel vibaya wanawake, ilihali wao ndio hawataweza kuvumilia endapo wanawake wote wataamua kujitunza na hayo masuala ya athari ni mtazamo tu wa kijamii, sababu ukienda kwa wazungu utakuta mitazamo tofauti na ukienda kwa waarabu utakuta mitazamo tofauti so hii ya kusema mwanamke ndio anapata madhara zaidi si uhalisia bali ni perception tu ya jamii za kiafrika
 
at dawn he was warned by the mods 🤣 I don't think he will do the same today If he is reported by any chance he will be banned. I doubt he will risk that 😀
Here we go again... He disliked your comment as well
 
Here we go again... He disliked your comment as well
coz I am his buddy he knows I can't report him😅
Screenshot_20230521_100339_Chrome.jpg
Screenshot_20230521_100454_Chrome.jpg
 
Shaloom.

Dada mmoja aliamini kuwa mtu pekee anayestahili kuitoa bikra yake ni mwanaume atakayemuoa.

Huu msimamo wa bibie ulifanya apoteze "wachumba" wengi kwani walipoambiwa hawataonja asali mpaka waingie ndoani walisepa.

Miaka ikaenda,umri wa dada ukazidi kusogea ila bibie hakubadili msimamo wake.Aliendelea kuitunza bikra yake na kuishi maisha ya heshima kama
ambvyo binti yeyote mwenye maadili anapaswa kuishi.

Walokole tuna kamsemo ketu kuwa wakati wa Mungu ndio wakati sahihi na kweli "wakati wa Mungu ulipofika" bibie akaposwa na kijana aishie huko Marekani.

Kilichomvutia kijana kwa bibie ni habari alizozisikia kuwa bibie hajawahi kuguswa na mwanaume yeyote.

Kijana akatuma washenga,akatoa mahari na kufanya taratibu zote ikabakia ndoa tu ambayo ingefungwa baada ya yeye kwenda marekani na kurudi tena Tanzania.

Basi ikawa rasmi kuwa bibie sasa ni mke mrarajiwa wa mtu aishie Marekani.Viongozi wa kanisa na wazazi wakawa wanamtumia bibie kama mfano wa kuwaasa watoto wa kike kuwa ukijitunza Mungu atakuletea mume bora.Mabinti wakaambiwa si mnaona mwenzenu kajitunza sasa anaolewa na kwenda kuishi Marekani?

Basi bwana siku za mume mtarajiwa kurudi marekani zikakaribia na akaomba aende Dar na mkewe mtarajiwa akamfanyie shopping pamoja na kumuachia mradi wa ujenzi wa jumba lao lililoko Dar ausimamie.

Kwa vile kijana alishafanya taratibu zote wazee wakaona haina shida wakamruhusu binti asafiri na mumewe mtarajiwa kutoka mkoani kwao mpaka Dar.

Kufika Dar wakashukia hotel na huko kijana baada ya kushindwa kumshawishi binti atoe uroda kabla ya ndoa akatumia njia ya kumlewesha na ndipo akafanikiwa kuitoa bikra ya binti kabla ya ndoa.

Dada alilia sana alipozinduka na kujua kikichotokea ila kijana wa marekani akafanikiwa kumtuliza dada kwa maneno matamu matamu na ahadi ya kumpenda mpaka kifo kiwatenganishe.

Dada akafanyiwa shopping kisha jamaa akakwea pipa akarudi state na bibie akarudi mkoani kwao.

Baada ya week kadhaa dada akagundua ana ujauzito wa mumewe mtarajiwa.Wazee wakajua na kijana wa marekani akajulishwa na kuombwa kufanya hima aje aoe mkewe na kuondoka nae kabla wambea hawajajua kuwa ile bikra iliyotunzwa kwa miaka mingi ishatolewa kabla ya ndoa.

Kijana wa marekani akazipokea habari kwa furaha na kuwaahidi wazee kuja ASAP lkn mpaka muda wa mtoto kuzaliwa ukafika ila kijana wa kimarekani hakutokea.

Baada ya miaka kadhaa ikaja kugundulika kuwa kijana wa kimarekani alikua ni muhuni tu aliyekua na fantansy ya kuchakata bikra na eti hata wakati anatoa ile mahari eti alikua tayari keshaoa zake huko marekani na eti wale washenga aliowatuma walikua ni wahuni wenzie tu wazee wa hovyo maana wazazi wake wa kweli walipofuatwa walishangaa maana wao wanajua kijana wao alishaoa siku nyingi tu.

Ikawa asubuhi ikawa jioni dada mrembo aliyeishi kwa maadili akajikuta akichukua kadi yake kwenye chama kubwa la single mazas nchini.

Chama ambacho wanaume wa kitanzania huwaona wanachama wote wa chama hicho ni wanawake wasiofaa sio kuoa tu bali hata kwa mahusiano ya kudumu bali kwa kuwagonga na kukimbia haraka uwezavyo kuokoa maisha yako.

Kabla sikajiunga JF nilikua nawaona single maza ni wanawake kama wanawake wengine.Wako wanaojitambua wako empty sets.Wako wanaojiheshimu wako micharuko.Wako wapole na wanyenyekevu wako vichomi pia.Inshort tabia zote za wanawake single mazas utazipata hata kwa wanawake wasio single mazas.

U single maza sio laana ambayo automatically inamfanya mwanamke awe na tabia za hovyo kama hakua hivyo mwanzo na wala kutokua single maza sio baraka/neema/kinga ya kumfanya mwanamke awe wa maadili/bora.

Mwanamke yeyote single maza or not tabia zake zinatokana na malezi au mtazamo wake katika maisha.

Mimi sio single maza ila as long as mim ni mwanamke kama ilivyokua kwa bibie mtunza bikra hata mim iko siku naweza kuangukia kwa bazaz nikalielewa tukadanganyana danganyana pale at ze end ov ze dei bila kujua imekua kuaje nikajikuta na mim nachukua kadi kwenye chama kubwa la singo mazeriz.

Ikitokea nimekua single maza sitapenda kuongelewa kwa namna single maza wanaongelewa hapa JF.

Hapa JF single maza wanaongelewa kama jamii ya watu wenye laana wanaopaswa kutengwa kama walivyotengwa wale wakoma wa kwenye biblia.

Hapa JF wanaume mnawaongelea singo maza kama viumbe wasio na akili wala maadili lakini naomba niwaambie hawa single maza ni nyie mmewatengeneza na tena ni kundi la wanawake wenye akili kubwa na ndio maana wanaweza kulea na kusomesha watoto wao ambao baadhi yenu mmewakataa na kuona ni bora hela yako ununulie msambwanda wa barmaid kuliko kununua daftari za mwanao.

Sio ajabu yule kijana wa marekani nae yuko hapa JF akiandika nyuzi za kuwaongelea single maza kama walaaniwa kumbe yeye ndio mlaaniwa.

Naombeni wanaume wa JF mtoe hiyo lebel mliyowapachika singo maza sio sawa duniani wala mbinguni sababu hamjui mwanamke amepitia mitihani gani mpaka kuishia kuwa singo maza.

Naomba viongozi wa Jamii forums muliangalie hili.Kuna singo maza anaweza kujiua akifikiria aliyopitia na kulinganisha namma jamii inavyomhukumu.

Sio sawa jamii kusema watu wote wa kundi fulani wana tabia fulani kwani hiyo sio kweli na sio sawa.

Iweje mwanamke aliyeishi maisha yake yote kwa kujitunza na kujiheshimu halafu badae jamii imuone takataka kisa tu analea mtoto/watoto wake bila baba?


NB:wanawake wa JF njooni tuwaeleweshe wanaume wetu kwa heshima na upendo kuwa kunyanyapaa single mothers sio sawa mana kama leo sio single mother kesho unaweza ukajikuta single mother au binti yako akawa single mother.Utapenda anyanyapaliwe?

Hata wewe mwanaume unayenyanyapaa single mothers leo huwezi jua iko siku wanaume wenzio watamdanganya aishie kuwa single mother.Utapenda jamii imnyanyapae?

H
Malalamiko mengi ya wanaowapinga single mother yapo kwenye ukishakuwa na single na kama baba wa mtoto yupo hai basi jiandae kupigiwa mzigo kupitia connection ya mtoto na siku zote ipo hivyo
 
Hapo kwenye jamii kumlabel vibaya mwanamke ndipo exactly point ilipo kwanini wanaume wawalabel vibaya wanawake, ilihali wao ndio hawataweza kuvumilia endapo wanawake wote wataamua kujitunza na hayo masuala ya athari ni mtazamo tu wa kijamii, sababu ukienda kwa wazungu utakuta mitazamo tofauti na ukienda kwa waarabu utakuta mitazamo tofauti so hii ya kusema mwanamke ndio anapata madhara zaidi si uhalisia bali ni perception tu ya jamii za kiafrika
Sasa sista, kwani ukiwa labeled tofauti siopinion ya mtu mwenyewe. Kwani utakufa, utashindwa kuishi😂😂😂😂. Wanaume tumeshaitwa mbwa na kila mwanaume ambaye hajaoa mpaka hajafikisha miaka 30 anaonekana ni kitombi asiye na mwelekeo wa maisha, umemsikia amelia au kulalamika. Kwenye jamii mwanaume kashakuwa labelled ni muharibifu na asiyemwaminifu hapo hata kabla mapenzi hayajui umesikia akilalamika. That's how life is, wanawake ndio mmeshatuchukulia hivyo, kwamba nyie ni watakatifu na innocent kuliko sisi yaani hadi kwenye baadhi ya kazi na ajira mwanamke ameonekana ni bora na anafaa kuliko mwanaume hasa HR na Treasurer. Ila sibado tunaishi na wanaume wamekubali kiroho safi. Sasa wewe unataka kila mtu aendane na fikra na mawazo yako😂😂😂😂, hatuishi hivyo. The world is diverse na every one has his/her own opinions sasa kama wanaume hizo ndizo fikra zao kwanini mzibadilishe wakati nyie hambadilishwi zenu. Live your life my sister, live men to be men!
 
Sio mother sio wazuri hata kidogo na tena hawafai kuolewa maana mioyoni mwao wanakuwaga na visasi vikubwa Sana ambavyo huwa wanalipiza.

Tena wanaingiaga kwenye ndoa kimachale Sana kwa sababu wanaogopa kupata maumivu mengine Kama Yale waliyopata mwanzoni.In short, masingle mazas hawanaga mapenzi ya kweli.
 
Oh! Your talking about exceptions. Kwanza fahamu naujue kuwa dunia inaendeshwa kwa generalizations, no gender is favoured there. Kuna mtoto wa kiume kazaliwa yatima nakakua akiwa chokoraa mtaani ila kwabahati nzuri Mungu akafanikiwa kupata mlo angalau wa siku moja, akitafuta mwanamke ataitwa masikini vilevile na atadharauliwa na kuchekwa na jamii hawatojali the background. That's how cruel the world is, no gender is the victim here. Pili jua, jinsia inayoongoza kwa generalization ni mtu mke kwasababu since childhood mwanaume anaonekana ni jinsia yenye tabia mbaya na haribifu kuliko mwanamke, ila have you seen complains my sister. Then just know, that is the world. You can't judge yourself, society judges you.
Bro Una madini sana. Nahisi unasoma sana vitabu
 
Nikiendelea kuongelea ili jambo, nitajikuta naweka wazi kitu ambacho mpaka leo sijaamuaga kukiongelea.

Labda nikufafanulie jambo moja, lawama wanazotoa single mothers, nyingi zinabase kwa wanaume waliozaa nao (their present and past life). Lakini zinazotolewa na wanaume, ni pale wanapokuwa kwenye mahusiano na single mothers (their present n future life).

So ni mwenye present & past VS mwenye present &future. Sijui kama umenielewa.

Hii mada ni too deep kuliko unavyoiona.

Ngoja niishie hapa [emoji4][emoji4].
Afadhali umejibu kwa kina sana na hapo ndipo matatizo yote yanapoanzia
 
Wewe mweleze ukweli kuwa kuna wadada umewzalisha likiwemo shangazi yule wa safari ya analyse[emoji3]

kifupi mwambie kwamba yule shangazi alitaka mwenyewe. Mbali na kuwepo njia za uzazi wa mpango zote na kujitahidi kote kumwaga nje[emoji16] shangazi alitaka mwenyewe kuzaa abebe mzigo wake[emoji2]
Ila habari ya shangazi noma sana,mpaka mshua akamwita mtoto wake legend
 
Aah wapi
Kuna baadhi wamelaaniwa aisee, na wataishia kuishi maisha ya kilaana laana TU kwenye generation yao kiss kung'ang'ania damu za Koo zingine
Sababu zinazotajwa za kijinga, majivuno, tamaa, kujiona na kujigamba Ni baadhi ya mambo ambayo single mother wakijihusisha wataendelea kuwa wengi.

FEMINISM,
FEMINISM,
FEMINISM
Inaenda kiwa deal kwenye hii dunia ya LAANA.
 
Hasa kwa wale ambao baba wa mtoto kala kona mazima, naongea kwa ushahidi kabisa kuna uhakika wa asilimia 90 kulala na single mother siku hio hio.

Mara nyingi huwezi kujua ni single mothers sababu bado ni umri mdogo bado ni pisi kali tu, ila ndio hivo tena ukiingia line suala la kupewa mzigo ni kawaida sana, nikuvuta tu

Sababu inayopelekea sana hizi ishu ni kupata pesa ya kulea mtoto na kutafta zali la kupata mme wa kumheshimisha kwenye jamii na mtoto awe na baba.. katika mzunguko huu sex inakuwa cheap sana
 
Back
Top Bottom