Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Heri MTU yule asiyeketi barazani pa wenye mizaha, je wewe unampenda Mungu? Kama jibu ndio basi wekeza nguvu zako, akili zako na moyo wako Kwa Mungu maana kila mtu atahukumiwa Kwa makosa yake hakuna atayebeba makosa ya mwenzake
 
Mungu wetu mwenye upendo Ameamua watu wauane tu hakuna wa kumuhoji kwa sababu yeye ni mpenda haki 😀 😀 😀 😀
mabaya yanayoendelea ni ushahidi kwamba yupo shetani na hukumu yake ilishaandaliwa anasubiri kuangamizwa, yeye ndo muongo na msababishaji wa mabaya yote.
Yesu alisema msiogope anayeua mwili tu

Mathayo 10:28 BHN​

Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.
tumwamini Mungu
 
Mungu ametuagiza tusamehe 7 mara 70, ila yeye kashindwa kumsamehe shetani. Ufafanuzi wa hili sijui ukoje.

Mungu alisema kuua ni dhambi lakini kwenye vitabu vya dini mara kadhaa Mungu ameua wale waliomchukiza.
1.Binadamu hana kibali cha kutoa uhai wa mtu.
Kibali hiko kipo kwa aliyetuumba peke yake.
Kama una uwezo wa kuumba uhai,ruksa kuutoa uhai.
2.Shetani alishavuka mipaka ya kusamehewa dhambi.
Kama itakavyotokea siku ya hukumu kwetu sisi wanadamu.
 
Mungu ametuagiza tusamehe 7 mara 70, ila yeye kashindwa kumsamehe shetani. Ufafanuzi wa hili sijui ukoje.

Mungu alisema kuua ni dhambi lakini kwenye vitabu vya dini mara kadhaa Mungu ameua wale waliomchukiza.

Kwa Mungu na shetani kuna agano usikurupuke.

Shetani aliapa kuharibu kila jambo jema la Mungu,hivyo hukumu dhidi yake inatoka a na kile alichonuia kukifanya milele.

Labda swali la msingi uulize kwanini hajaamua kumuua tu??
 

Kukandwa hata wewe unaweza kukandwa nyuma ya bajaji,ni swala la mkandaji na wewe mkandwaji mmeamua nini.

Dini haina mikono kwamba itakushika kukuzuia usifanye hiki.
 
Mungu anapewa vingi tofauti na yeye anavyodeliver in return

Biashara kati ya Mungu na binadamu ni biashara kichaka

Unatoa pesa unapata makelele yanayoitwa maombi

Biashara kati ya binadamu na ni biashara ya kimangungo

Mungu anataka/anatoa pesa!!!nani alikwambia???

Mungu anatoa gari nani alikwambia??

Mungu anatoa afya nzuri nani alikwambia??

Imani zinabebwa na vijana kama charger za simu ndio sababu mtu asipokiona alichotarajia anapitea jumla.
 
tumemchoka Mungu wa mchongo asiyekuwa na haki wala faida,, Mungu ni kiziwi hasikii👽
 
Mungu anapewa vingi tofauti na yeye anavyodeliver in return

Biashara kati ya Mungu na binadamu ni biashara kichaka

Unatoa pesa unapata makelele yanayoitwa maombi

Biashara kati ya binadamu na ni biashara ya kimangungo
Akiitoa Pumzi yako Kuna Jambo lolote utaloweza kufanya?
 
Hujalijua neno vizuri mkuu,, yote yapo hayo
 
Kuwa atheist sio kuporomoka kwa maadili, ni kupata akili

Wachungaji walizokula zinawatosha, watu wamepata akili
Kwa macho na masikio yangu naona na kusikia mchungaji maarufu katika eneo lake la kichungaji kafumaniwawa na kurekodiwa sehemu na mwanafunzi wa shule fulani ili jambo libaki sirini, kakubali kulipa fine Tsh 4,000,000/= katoa mil.2.5 nyingine kasema wamsubiri hadi jumapili akimaliza ibada atatoa iliyo baki. Nikasema kanisani siendi tenaaaa
 
Umenena ukwl mkuu,, Ila kumbuka hata shetani hutoa utajiri pia! Point yako unaweza kua na majibu mengi Sana Ila kumbuka hao waovu waliomatajiri Ni Kama ng'ombe anaenenepeshwa siku ya mnada wachinjwe!
 

Dini imekosa mashiko,ni stori kama stori zingine za kale,mbaya zaidi wanaojinasibu viongozi wa dini ndio wameiharibu dini.
 
Wewe nawe pia unasema MUNGU hayupo Mungu hana uwezo Mungu ni ameumbwa na simulizi za kusadikika za wanadamu Mungu hajawahi kuwepo, unamaanisha hivyo ? Na je pia wewe una-support ushoga na usagaji ?

Ukiona mtu anaingiza story za ushoga pasipo husika,tambua huyo mtu ni shoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…