Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Yaani maoni yako ya kutokuwepo kwa Mungu hayaondoi uwepo wake. Yeye yupo
Zaburi 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema”.
Inaonekana huyo mungu wenu hajui hata Binadamu aliyemuumba anafanyaje kazi,

Hahahah Kwa andiko hilo tu linaonyesha huyo mungu ni kilaza wa kutupa maana tangu lini moyo ukawa na mawazo ? Tunachojua Ubongo ndo hubeba Akili na Mawazo,... na Mtu akisema basi hutumia Mdomo,

Sasa hayo ya Kusema kupitia moyo yanatokanaje ? Huyo mungu anajua kweli alichokisema au ? Enewei ngoja nimsaidie kiufupi moyo kazi yake ni kusukuma damu tu hayo ya kusema na kuwaza kazi yake hufanywa na Ubongo na Mdomo.
 
Kasi ya watu kuwa Atheist yaani watu wasioamini uwepo wa Mungu ni kubwa sana siku hizi. Tulizoea kusikia mambo haya kwa wenzetu Ulaya na America, lakini atheism imehamia Africa na inakuwa kwa kasi kubwa mno.

Ni nini sababu za watu wengi hasa vijana kuacha kuamini katika uwepo wa Mungu na nguvu zake? Je, wimbi hili la kukosa imani kwa Mungu ndio sababu ya kuporomoka kwa maadili Afrika? Tujadili.
Tatizo mtu unatumia energy na muda mwingi kuabudu, kusali na kuomba afu unachokitaka hukipati, mafanikio zero.

Hapo hapo unakuta Kuna mtu hata hajui kama Kuna Mungu lakini anatoboa kirahisi sana. Kwa mtindo huu unaanzaje kumuamini Mungu?
 
Amri kumi zimewekwa ni muongozo Ili wanadamu waishi vyema KWA amani na utulivu. Mungu hana hasara nawe kuzifuata au kutozifuata hata sheria za nchi na sheria za Jamii zimekopi toka sheria za MUNGU.
Hasara anayo maana nisipofuata amri zake atanichoma moto, so energy aliyotumia kuniumba inakua wasted
 
Kwangu mimi naamini uwepo wa Mungu, piga ua garagaza bado nitakwambia "God is Surely Alive"

Kwa vile nilivyovishuhudia hadi kufika hapa na experience yangu ya maisha ya kiroho na kijamii kwa ujumla siwezi kukataa uwepo wake. Mungu anaishi.

Though kwa dunia ya sasa tunakutana na mafundisho mengi ya kitapeli lakini vyote haviwezi ondoa dhana ya uwepo wa Mungu....

Ukitaka ujue uwepo wa Mungu basi fungua na hii dhana ya uwepo wa Majini, mapepo, mizimu, uchawi na ushirikina... Ukianza kuvielewa hivi basi hakika utajua kuwa kuna invisible spiritual power inayo monitor dunia hii...!!

Lengo la adui (Shetani) ni kuzifunga fahamu za kibinadan zisisadiki uwepo wa Mungu just kwa simple fact wanayoiita elimu na haohao vijana wanao jiita wameelimika wanashindwa kuchunguza kuyachunguza zaidi maandiko... Wanaanza kuelea na zile simple facts wanazokutana nazo mitandaoni na mitaani!!!

Msingi mkuu wa kumjua Mungu ni maandiko na si kuyasoma tu kama gazeti lakini pia omba uvuvio wa Mungu uwe na wewe unapoanza kuzifahamu siri zilizofichwa kwenye maandiko

Nawasilisha

Agapeboy nimemaliza
 
Sababu Mungu sio dikteta thus kampa mwanadamu freewill achague kutenda mema au maovu kwa faida na hasara yake mwenyewe.
Freewill?? Ukichagua asiyoyapenda anakurusha motoni. Hivi kwa nini nguvu anayotumia mungu kuandaa moto wa milele kwa wale tusiomuelewa/amini asingeitumia kumalizana na shetani once & for all?? Au kwa nini asiitumie nguvu hiyo kulinda amani ya dunia dhidi ya watu wanompigania katika ulimwengu huu??
 
Sababu kubwa mbili
Ya kwanza mungu hana faida duniani maana maovu yapo pale pale watu wanaiba watu wanaua watu wana dhulumiwa mfano hapa nchini kwetu tuliona wazi uchaguzi wa 2020 viongozi wengi waliingia madarakani kwa wizi wa kura na hakuna hata kiongozi hata mmoja wa dini aliekemea ule wizi wa kura je mungu anaruhusu kuiba sana sana tuliona masheikh na mapadri na wachungaji waliuenda kumpongeza raiasi aliyeiba kura kukaa madarakani maana yake dini zinabariki wizi

Jambo la pili elimu vijana wengi wana elimu kushinda wazazi wao hivyo wanakuwa wameelimika na kujua dini ni mpango maalumu wa kumtawala mtu kifikra na kimawazo wala hakuna jipya
 
Mungu haihitaji msaada wa Mwanadamu kumpigani hao wanaopigana KWA ajili ya Mungu Wana shida ya akili.
Atamalizna na shetani baada ya muda huu wa kutubu ukipita
Dunia si makao ya milele ni sehemu tu ya kupita KWA mwanadamu.
 
Tatizo mtu unatumia energy na muda mwingi kuabudu, kusali na kuomba afu unachokitaka hukipati, mafanikio zero.

Hapo hapo unakuta Kuna mtu hata hajui kama Kuna Mungu lakini anatoboa kirahisi sana. Kwa mtindo huu unaanzaje kumuamini Mungu?
Eti unatumia energy na muda mwingi kusali. hebu fafanua hayo matumizi ya energy na muda kwenye kuabudu
huo muda mwingi unatumia kumwabudu Mungu wapi
Yeye ameagiza siku sita fanya kazi ,ya saba upumzike . nani kakudanganya Mungu anaabudiwa ili kuwa tajiri
Fungu lingine linasema asiyefanya kazi asile
 
Sababu kubwa mbili
Ya kwanza mungu hana faida duniani maana maovu yapo pale pale watu wanaiba watu wanaua watu wana dhulumiwa mfano hapa nchini kwetu tuliona wazi uchaguzi wa 2020 viongozi wengi waliingia madarakani kwa wizi wa kura na hakuna hata kiongozi hata mmoja wa dini aliekemea ule wizi wa kura je mungu anaruhusu kuiba sana sana tuliona masheikh na mapadri na wachungaji waliuenda kumpongeza raiasi aliyeiba kura kukaa madarakani maana yake dini zinabariki wizi

Jambo la pili elimu vijana wengi wana elimu kushinda wazazi wao hivyo wanakuwa wameelimika na kujua dini ni mpango maalumu wa kumtawala mtu kifikra na kimawazo wala hakuna jipya
Uliona kura zimeibwa? Au viongozi wa dini waliona kura zikiwa zinaibwa? Shida yetu vijana tunaishi kwa kuamini tunachokiona mitandaoni wakati hamjui behind the scene kuna kipi kimepikwa!!

Na huwezi kuniambia sababu ya elimu basi ndo tuseme Mungu hayupo "Never" Hiyo elimu tuliyonayo ni juu ya mambo mengine bado hatujataka kuipata elimu kuhusu Mungu...

Na tunapoingia kujifunza kuhusu Mungu tunaingia huku tukitafuta sababu za kutokutaka kujua kama Mungu yupo
 
Back
Top Bottom