Kwanini Viongozi kutokea Zanzibar wanapenda kuuza ardhi ya Tanganyika?

We umeandika clever remarks. Marais wanaotokea Unguja wanauza ardhi ya Tanganyika kuliko hata rais wanaotokea bara.
Lakini you had better double check your statements,labda hawajampiku Kikwete.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 nyie viumbe mna tatizo mahala kwa hiyo hao waliosalia hawakuwahi kuwapa mali asili yetu NJE YA SISI tena kwa faragha?

Mkitaka tupige hatua orodheni tangu Mwalimu hadi leo hii nani aliwapa wakina nani na nani amewapa wakina nani?


Kwani yale mashimo yanayozungumziwa kila leo wachimbaji hao hao???!
 
Rais mstaafu Mzanzibar Ali Hassan Mwinyi ndiye aliyewauzia Loliondo waarabu.

Na huenda Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mzanzibar atawapa bandari zetu za Tanganyika waarabu.

(Zanzibar!)
Hawa Wazanzibari wana agenda yao na wajomba zao huko Omani kwamba sasa wanaweza kuingia kwa Bandari na kuondoka au kutua kwa ndege Loliondo na kusepa zao. Hebu tumuulize spika wa Bunge ana maoni gani.
Ndugai wew unaonaje haya mambo?
Aaa mimi Job Yustin Ndugai nilisha sema ccm wataipiga mnada hii nchi hayo ndio maoni yangu Asante sana
 
Acheni sumu ya ubaguzi, mnapanda kitu kibaya sana. Kilicho binafsidpshwa ni uendeshaji na siyo ardhi wala bandari yenyewe.
Hapo ni sawa na kunipa gari niendeshe maisha yangu yote lakini ukatae kunipa kadi ya gari.

Sasa kadi ya gari mimi ya nini ikiwa gari umeniachia nitumie navyotaka?
 
Huo mkataba uko wapi?
 
Hamia Rwanda bibie
 
La bandari labda tupige kelele terms za mkataba lakini hakuna ubaya kuwapa watu toka nje. Tatizo la nchi yetu huwa tunaingia mikataba ya kijinga sana na terms za ovyo ndiyo maana huwa tunakosa meno kuwawajibisha pindi wanapoenda kinyume cha makubaliano.
Pengine nahisi watu wetu hawajui negotiation na utaalamu wa mikataba.
Sababu unashangazwa tunaingia mikataba na makampuni yaleyale ambayo yanafanya vema nchi zingine cha ajabu wakiwa kwetu mambo mara nyingi huenda mrama.
 
Jibu ni rahisi; wametuona watanganyika ni wapumbavu.
 
Ubaguzi ni mbaya sana, lakini viongozi wetu waache vitendo vinavyoashiria hilo. Bandari zote za Tanzania utendaji siyo wa kuridhisha, hivyo kama ni majaribio ya kubinafsisha kwa nini za upande mmoja tu? Watu kupenyeza mbegu mbaya ya ubaguzi haishangazi.
 
Hivi tumeshaanza kuingiwa na Ubaguzi kiasi hiki. Huu Utanganyika na Uzanzibari umetokea wapi? Yatupasa kuwa makini na kauli kama hizi.
 
Ukishauza Bandari zote,maana yake umeshatawaliwa.

Huna uwezo wa kuagiza Chakula Wala silaha wakati wa Vita.
Kwa TICTS walivyokuepo nchi haikua ikiagiza chakula na Silaha? Mbona nyie jamaa washamba hivi?

1. Unabinafshishwa uendeshaji wa bandari
2. Sio Bandari yote/Zote bali sehemu tu ya Bandari kwa wataohitaji.

Kipindi cha Ticts mzigo uliweza kuingia na Tpa ama Ticts.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…