Kwanini Viongozi kutokea Zanzibar wanapenda kuuza ardhi ya Tanganyika?

Kuna mtanganyika anaweza kuwa Balozi wa nyumba kumi nchi ya Zanzibar
Hiyo nchi ya Zanzibar ina watu milioni mbili wakati mkoa wa Dar peke yake una watu milioni sita. Kapungukiwa nini huyo mtu wa bara mpaka akawe balozi wa nyumba huko Zanzibar?.
 
Mkuu wa kaya mpemba!
wasiri mpemba!
Bunge ni dhaifu na la wapenda kitu 'kdg'
Mkataba unapita kama ulivyo nawaambia!
 
I wish na wenyewe wangejitegemea tu kama ilivyo kwa hao Shelisheli, Madagascar, Comoro, nk. Hakukuwa na sababu ya msingi ya kuungana na Tanganyika.
 
Acheni sumu ya ubaguzi, mnapanda kitu kibaya sana. Kilicho binafsishwa ni uendeshaji na siyo ardhi wala bandari yenyewe.
Major means of production, mojawapo ni ardhi. Bila ardhi huwezi fanya chochote. Huo uendeshaji wanafanyia wapi? Wamepewa bandari, bandari ni ardhi siyo kitu kingine.
 
Ndugu zangu Watanganyika, hili suala la kuuzwa kwa Bandari zetu kwa Waarabu litoshe kutuamsha kutoka usingizini.

Kwa dalili hizi, ipo siku tutajikuta Rasilimali zote muhimu kwa upande wa Tanganyika zimehamishiwa na zinamilikiwa na watu wa upande wa pili wa shilingi.
 
Kwa wabunge gani? Hawa wabunge wa mchongo?
Hivi ina kuwaje wizara ambayo siyo ya Muungano inaongozwa na Mpemba??
Halafu Bara mna sema ni sahihi kubinafsisha?! Kweli??
Hii ni ajabu ya Karne hii
 
Kuna mtanganyika anaweza kuwa Balozi wa nyumba kumi nchi ya Zanzibar
Mchawi ni mfumo wa muungano wetu.

Kwa mujibu wa katiba, kuna mambo ambayo hayapo kwenye muungano; lakini Rais wa muungano kutokea Zanzibar ana mamlaka hata kwenye mambo ya Tanganyika yasiyo ndani ya muungano.

Namheshimu sana Mwalimu Nyerere, lakini alichotufanyia watanganyika kwenye huu muungano ilikuwa uhaini.

Mara nyingi sana najiuliza, hivi wanasheria hawawezi kulifikisha hili swala kwenye mahakama ya kikatiba ili kupata ufumbuzi wa hii mikanganyiko kwenye katiba?!
 
Ni ubaguzi tu wa kuwatizama wazenji kama wafaidika wa awamu ya sita. Vipi kuhusu wasukuma kuwa wafaidika wa awamu ya tano ya JPM?. Akili duni tatizo letu.
Unayo majibu ya sababu za bandari za Zanzibar kutokuwemo kwenye huu mkataba?!
 
IELEWEKE kuwa hata wizara anayoongoza MAKAME MBARAWA ya Ujenzi sio ya Muungano basi tu watu wamestahi mamlaka ya Rais kumteuwa …….maana siku hizi hadi wakuu wa Wilaya wanatokea Zanzibar Nafasi Ambazo pia sio za muungano
Mambo nyeti kama haya ndio kina Kibatara wangetusaidia kwenda mahakamani kupata tafsiri sahihi ya katiba, japo katiba yenyewe mbovu.
 

We mwenyew chuki tu zimekuzidi umejuaje kama Mbowe huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…