Kwanini Viongozi kutokea Zanzibar wanapenda kuuza ardhi ya Tanganyika?

Kwanini Viongozi kutokea Zanzibar wanapenda kuuza ardhi ya Tanganyika?

Kwa vile kuna ardhi iliuzwa huko nyuma basi ni sawa tu na wao wauze ....!!? Sijui unataka kujustfy nini hapa!!

Nafiki tatizo kubwa siyo uwekezaji. Watu hawana shida na uwekezaji. Watu wanashida na aina ya mkataba wa uwekezaji!!
Mkataba wameuona wapi!?
 
We mrundi ndomana unashabikia Tanganyika kuuzwa
Mimi naweza kuwa mtanzania kuliko wewe. Hakuna anayetaka kuiza nchi yako, ni ujinga wa hao wanaoendesha taasisi zetu unaochanganyika na wizi wa mabilioni huko bandarini ndio unaowapa kiburi cha kutetea maslahi yao haramu.

SSH anayo nia nzuri sana kwa uchumi wetu, tatizo letu ni lile lile la uzembe wa kufikiria. Hatutaki kutoka kwenye comfort zone yetu inayowapa faida wachache na kuwaumiza walio wengi.
 
Kwa vile kuna ardhi iliuzwa huko nyuma basi ni sawa tu na wao wauze ....!!? Sijui unataka kujustfy nini hapa!!

Nafiki tatizo kubwa siyo uwekezaji. Watu hawana shida na uwekezaji. Watu wanashida na aina ya mkataba wa uwekezaji!!
Hakuna anayetaka kuiza Tanzania, bandari inataka kupewa mwekezaji mpya ili aje na changamoto mpya zitakazotusaidia kuinua uchumi wetu.

Wapo mafisadi wachache wanaofaidika na huo uzembe hapo bandarini ndio wanaopotosha watu kwamba SSH anataka kuuza nchi, that is bull shit.

Tafuta video ya yule Mama mwenyekiti wa wenye viwanda Tanzania uweze kuelewa ambacho hukijui kwa sasa.
 
Huyu ni Freeman Mbowe na maoni yake. Mnataka kuja na hoja zilizofilisika kwamba Tanganyika inaibiwa na Zanzibar.

Vipi kuhusu ufisadi wa miaka na miaka uliofanywa enzi za hayati Mkapa, akaja Kikwete na wenyewe tumeusahau?.

Mkataba haujasainiwa na muda wowote tunaweza kuukata. Vipi kuhusu madhara ya hizi chuki tunazozipalilia, nani atayaondoa wakati maji yakiwa yameshamwagika?.

Tunakimbilia akili za kipumbavu za kibaguzi lakini hatuna suluhisho ikiwa huu ubaguzi utakwenda mbali na kuuharibu Utanzania wetu.
Mkataba umekwishasainiwa, usiwadanganye watu eti haujasainiwa. Unapelekwa bungeni kufanyiwa domestication siyo maamuzi ya kuusaini au kuacha.
 
Mkataba umekwishasainiwa, usiwadanganye watu eti haujasainiwa. Unapelekwa bungeni kufanyiwa domestication siyo maamuzi ya kuusaini au kuacha.
Cha kupinga ni hizi hoja hasi zinazosambazwa wakati lengo la serikali ni jema.
 
Cha kupinga ni hizi hoja hasi zinazosambazwa wakati lengo la serikali ni jema.
Mashaka makubwa kuwa mkataba huu ni wa hovyo, na hakuna nia njema, kwanza ni tuhuma za rushwa.

Kwa nini wabunge waliopewa mwaliko kwenda huko Dubai wahongwe pesa na magari? Hongo siku zote inalenga kukupofusha.

Kitendo hicho tu cha mwekezaji kutoa hongo, kinatosha kuufanya mkataba huu kuthibitika kuwa hauna tija kwa Taifa
 
Hata huu mjadala wa bandari yetu kuuzwa kwa waarabu siamini kama Magufuli angekuwepo tungekuwa tunaujadili.

Wewe unafikiri Magufuli angewapa waarabu bandari yetu?
Hilo nina uhakika Maguguli asingelifanya. Magufuli tumlaumu kwa mambo mengine, lakini kwenye utaifa, alikuwa ni mtu mwenye proud na nchi, na kama angekuwa na uwezo alitaka kila kitu tufanye wenyewe, japo uwezo hatukuwa nao.
 
Mashaka makubwa kuwa mkataba huu ni wa hovyo, na hakuna nia njema, kwanza ni tuhuma za rushwa.

Kwa nini wabunge waliopewa mwaliko kwenda huko Dubai wahongwe pesa na magari? Hongo siku zote inalenga kukupofusha.

Kitendo hicho tu cha mwekezaji kutoa hongo, kinatosha kuufanya mkataba huu kuthibitika kuwa hauna tija kwa Taifa
Una ushahidi gani kwamba hayo magari wameyanunua kwa pesa waliyohongwa Dubai?. Uje na hoja zenye kukaribia ukweli japo asilimia hamsini.

Hoja ya wafanyabiashara wenye kuitumia bandari kila siku ni kuwepo kwa huduma za kisasa, ni kutaka makontena yasiwe yanakaa wiki nzima huku storage ikiongezeka kwa uzembe wa bandari yenyewe.

Tuwasikilize wadau wenyewe wa viwanda na biashara kuliko kuzipa kipaumbele hoja za kisiasa za watu wenye kufaidika na huu wizi wa bandarini.
 
Bandari zetu zikiuzwa kwa Waarabu, nina uhakika, mtanzania kusogea kwenye maeneo hayo ya bandari itakuwa ni kama kwenda Uarabuni.

Waarabu kiasili ni wabaguzi. Waulizeni waafrika wanaoenda huko Uarabuni, hasa wale wafanyakazi wa kada za chini.

Mnakumbuka lile tukio la mtanzania aliyekuwa anafanya kazi Uarabuni kwenye kiwanda cha nyama, alipopandishwa cheo na kuwa mkuu wa kitengo cha ukataji, wafanyakazi wa chini yake ambao ni waarabu, wakala njama ya kumwua? Jamaa siku hiyo alipoingia tu, walimshika, mzimamzima na kumtumbukiza kwenye mashine ya kukatia nyama, ndiyo ikawa mwisho wa maisha yake.

Lazima kwenye bandari zote, kila kitengo, wakuu na wasimamizi watakuwa waarabu. Waswahili au watwana, kama walivyozoea kuwaita waafrika huko Omani, watakuwa kwenye nafasi za chini kabisa hata kama watakuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko hao waarabu. Waarabu na wahindi, kati ya vitu ambavyo wanaona ni kama haiwezekana, ni kufanya kazi chini ya mtu mweusi.

Nimefanya kazi nje ya Tanzania, kwenye kampuni ya Waingereza, nikiwa project Manager, chini yangu expatriates 71, na nationals 360, sikuona mzungu yeyote kuwa na ukakasi wa kunikubali kuwa ndiye mkuu wake wa kazi (japo wengi walikuwa wanadhani mimi ni black American). Lakini kwa waarabu ni vigumu sana. Wanakubali kufanya kazi chininya mzungu lakini siyo mtu mweusi.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Kumekuwa na sintofahamu kila mara kiongozi mkuu wa nchi (Rais wa JMT) akitokea nchi ya Zanzibar jambo la kwanza ni kuuza ardhi ya Tanganyika.

Rais wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi aliuza ardhi ya wamaasai huko Loliondo kwa waaarabu wa Dubai UAE.

Rais Samia Suluhu Hassan na yeye anauza Bandari zetu zote za Tanganyika kwa waarabu wa DUBAI huku Bandari za Zanzibar zikisalimika katika uporaji huu uliotukuka.

Ifahamike BANDARI ni suala la MUUNGANO lakini utashangaa suala la kuuza BANDARI zetu zote kuanzia MTWARA, TANGA, BAGAMOYO na Dar limezigusa bandari za TANGANYIKA peke yake huku BANDARI za Zanzibar zikisalika. Ijulikane mapema zoezi hili la uporaji litagusa pia BANDARI zilizoko katika maziwa yetu yote yaani Ziwa Victoria, Nyasa,Tanganyika.

Wahusika wote katika uporaji wa wahusika wakuu ni WAZANZIBAR kwa maana ya RAIS na Waziri.

Kwa hakika suala la katiba mpya sasa haliepukiki.

Ngongo kwa sasa safari Dubai - Deira
Kama ni kuuzwa, Loliondo imekuja kuuzwa mwaka 2022 baada ya wenyeji kuondolewa kwa nguvu za kineshi na maeneo ya vijiji vyao kumegwa. Kabla ya hapo ardhi ilibakia kuwa mali ya wenyewe huku shughuli za uwindaji zikiendelea bila matatatizo yoyote.
 
Huyu ni Freeman Mbowe na maoni yake. Mnataka kuja na hoja zilizofilisika kwamba Tanganyika inaibiwa na Zanzibar.

Vipi kuhusu ufisadi wa miaka na miaka uliofanywa enzi za hayati Mkapa, akaja Kikwete na wenyewe tumeusahau?.

Mkataba haujasainiwa na muda wowote tunaweza kuukata. Vipi kuhusu madhara ya hizi chuki tunazozipalilia, nani atayaondoa wakati maji yakiwa yameshamwagika?.

Tunakimbilia akili za kipumbavu za kibaguzi lakini hatuna suluhisho ikiwa huu ubaguzi utakwenda mbali na kuuharibu Utanzania wetu.
Ufisadi wa sasa wa bandari umekithiri
 
La bandari labda tupige kelele terms za mkataba lakini hakuna ubaya kuwapa watu toka nje. Tatizo la nchi yetu huwa tunaingia mikataba ya kijinga sana na terms za ovyo ndiyo maana huwa tunakosa meno kuwawajibisha pindi wanapoenda kinyume cha makubaliano.
Pengine nahisi watu wetu hawajui negotiation na utaalamu wa mikataba.
Sababu unashangazwa tunaingia mikataba na makampuni yaleyale ambayo yanafanya vema nchi zingine cha ajabu wakiwa kwetu mambo mara nyingi huenda mrama.
Kabudi hajaona huu mkataba?
 
Waarabu kiasili ni wabaguzi. Waulizeni waafrika wanaoenda huko Uarabuni, hasa wale wafanyakazi wa kada za chini.
Mbali kote huko! Nenda hapo Loliondo kwenye ardhi waliyogawiwa na mwinyi uone uhalisi wa mambo.
 
Hakuna anayetaka kuiza Tanzania, bandari inataka kupewa mwekezaji mpya ili aje na changamoto mpya zitakazotusaidia kuinua uchumi wetu.

Wapo mafisadi wachache wanaofaidika na huo uzembe hapo bandarini ndio wanaopotosha watu kwamba SSH anataka kuuza nchi, that is bull shit.

Tafuta video ya yule Mama mwenyekiti wa wenye viwanda Tanzania uweze kuelewa ambacho hukijui kwa sasa.
Kama nilivyosema hapo juu. Tatizo ni mkataba ndiyo wenye matatizo. Siyo kwamba watu hawataki Mwekezaji.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Kumekuwa na sintofahamu kila mara kiongozi mkuu wa nchi (Rais wa JMT) akitokea nchi ya Zanzibar jambo la kwanza ni kuuza ardhi ya Tanganyika.

Rais wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi aliuza ardhi ya wamaasai huko Loliondo kwa waaarabu wa Dubai UAE.

Rais Samia Suluhu Hassan na yeye anauza Bandari zetu zote za Tanganyika kwa waarabu wa DUBAI huku Bandari za Zanzibar zikisalimika katika uporaji huu uliotukuka.

Ifahamike BANDARI ni suala la MUUNGANO lakini utashangaa suala la kuuza BANDARI zetu zote kuanzia MTWARA, TANGA, BAGAMOYO na Dar limezigusa bandari za TANGANYIKA peke yake huku BANDARI za Zanzibar zikisalika. Ijulikane mapema zoezi hili la uporaji litagusa pia BANDARI zilizoko katika maziwa yetu yote yaani Ziwa Victoria, Nyasa,Tanganyika.

Wahusika wote katika uporaji wa wahusika wakuu ni WAZANZIBAR kwa maana ya RAIS na Waziri.

Kwa hakika suala la katiba mpya sasa haliepukiki.

Ngongo kwa sasa safari Dubai - Deira
watanganyika mabwege
ona haya
 
Back
Top Bottom