Bandari zetu zikiuzwa kwa Waarabu, nina uhakika, mtanzania kusogea kwenye maeneo hayo ya bandari itakuwa ni kama kwenda Uarabuni.
Waarabu kiasili ni wabaguzi. Waulizeni waafrika wanaoenda huko Uarabuni, hasa wale wafanyakazi wa kada za chini.
Mnakumbuka lile tukio la mtanzania aliyekuwa anafanya kazi Uarabuni kwenye kiwanda cha nyama, alipopandishwa cheo na kuwa mkuu wa kitengo cha ukataji, wafanyakazi wa chini yake ambao ni waarabu, wakala njama ya kumwua? Jamaa siku hiyo alipoingia tu, walimshika, mzimamzima na kumtumbukiza kwenye mashine ya kukatia nyama, ndiyo ikawa mwisho wa maisha yake.
Lazima kwenye bandari zote, kila kitengo, wakuu na wasimamizi watakuwa waarabu. Waswahili au watwana, kama walivyozoea kuwaita waafrika huko Omani, watakuwa kwenye nafasi za chini kabisa hata kama watakuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko hao waarabu. Waarabu na wahindi, kati ya vitu ambavyo wanaona ni kama haiwezekana, ni kufanya kazi chini ya mtu mweusi.
Nimefanya kazi nje ya Tanzania, kwenye kampuni ya Waingereza, nikiwa project Manager, chini yangu expatriates 71, na nationals 360, sikuona mzungu yeyote kuwa na ukakasi wa kunikubali kuwa ndiye mkuu wake wa kazi (japo wengi walikuwa wanadhani mimi ni black American). Lakini kwa waarabu ni vigumu sana. Wanakubali kufanya kazi chininya mzungu lakini siyo mtu mweusi.