LATRA waruhusu Mabasi kuanza safari saa 9 Usiku

LATRA waruhusu Mabasi kuanza safari saa 9 Usiku

Speed SIO chanzo pekee cha ajali nyingi hapa Tanzania, tatizo kubwa barabara zetu bado sana,Dar to Arusha ni kama 650km,huu ni mwendo wa saa nane kwa bus na mapumziko juu, nashauri tutengeneze hizi barabara kwa kiwango kinachokubaliwa na tuziwekee road tolls ili watumiaji wachangie gharama za uboreshaji wa barabara zetu, mabus yaruhusiwe 24hrs yatembee barabarani au majambazi wametuzidi kete?
Issue kubwa, ni kila barabara inapokamilika vijiji vingi vinahamia kwenye Kingo za barabara na hivyo kulazimisha hizi speed limit za 50kph kuwa nyingi! Safari inachosha sana Kwa kila dakika kupunguza speed to 50, fikiria barabara inaboreshwa kama Dar Moro mwanzoni masaa mawili Sasa masaa manne shida ni nini!? Tujiulize tuanzie hapo!! Hii kuongeza muda WA kuanza safari Haina maana kabisa!! Hawa latra na jeshi la polisi, na Tanroads wajiongeze waache Mazoea, wafanye researches, mshahara Mkubwa ufanisi Mashaka
 
Ndiyo maana tunasema humu wengine siyo wasafiri that's why mnapinga.

Si kwamba LATRA wamekurupuka, mfano wako tayari umefanyiwa kazi na hata mimi nimewahi na huwa nasafiri usiku kwa bus.

Dar to Moshi zipo, Dar to Mbeya zipo labda ukitaka watangaze kwenye kabisa.
Dar to moshi ni basI gani limesafiri saa tisa alfajiri?
Twende kwa data
BINAFSI NATAMANI MABASI KWA ROUTE ZILIZO SALAMA YASAFIRI 24HRS
 
Matokeo ya kulazimisha mambo huwa mabaya. Ajali zitakuwa nyingi sana na matukio ya magari kutekwa na majambazi yataongezeka.

Tuwe wavumilivu, SGR itatupa usalama zaidi kusafiri usiku.
Kwamba gari zitekewe wapi wakati muda huo pamepambazuka?
 
Speed SIO chanzo pekee cha ajali nyingi hapa Tanzania, tatizo kubwa barabara zetu bado sana,Dar to Arusha ni kama 650km,huu ni mwendo wa saa nane kwa bus na mapumziko juu, nashauri tutengeneze hizi barabara kwa kiwango kinachokubaliwa na tuziwekee road tolls ili watumiaji wachangie gharama za uboreshaji wa barabara zetu, mabus yaruhusiwe 24hrs yatembee barabarani au majambazi wametuzidi kete?
Ndivyo yatakiwa ila tatizo ni wamamchi na sisasa
 
Kabla ya kufikia kuruhusu hayo kwanza waboreshe miundombinu ya barabara...... barabara mbovu zinachangia asilimia kubwa za ajali za barabarani.........wasifanye maamuzi ya kisiasa na kutuangamiza sie tusiokuwa na hatia.....maana wao wanasafiri na vieiti na ving'ora sisi tunapelekwa kama ng'ombe......
Hawataki ushauri wako,
Wangeutaka wangekutafuta
 
Watu wengi wana uoga wa kufikirika.

Makampuni yana uwezo wa kufanikisha hili, labda shida ije kuwa na upungufu wa abiria kinyume na hapo ni jambo linalowezekana.
Makampuni yanataka iwe masaa 24 na sio kuanza saa 9 usiku
 
Usalama vipi? Mnachekelea tu kuruhusiwa kwa safar za usiku lkn hamuwazi side effects za hizo safar? Vip ujambaz, ubovu wa barabara na ujinga wa wale madereva wanaobeti kuendesha speed kubwa?

Hili walitolee ufafanuzi
Mbona zinaaza saa 11 lini umesikia kuna ajali imetokea?
 
Hahaha mpwa hujui usemalo, Wacha nikuonjeshe facts. Hii hapa chini nimechukua kutoka group Fulani sitalitaja.

MWANZA_DAR
[emoji625]KONGOWE

01:[emoji269]EBF[emoji521][emoji521]_ 22:49

02:[emoji269]KUFFI[emoji289][emoji289]_22:50

03:UNSTOPPABLE[emoji521][emoji521]_22:50

04:KATARAMA[emoji1095][emoji1095]_22:52

#VIDEO LOADING#[emoji91][emoji91]

Yaani saa nne wanaingia kongowe
Maana yake kama wangeondoka saa 9 Dar saa 1
 
Matokeo ya kulazimisha mambo huwa mabaya. Ajali zitakuwa nyingi sana na matukio ya magari kutekwa na majambazi yataongezeka.

Tuwe wavumilivu, SGR itatupa usalama zaidi kusafiri usiku.
Ajali zinazotokea saizi,wanasafiri saa ngapi?
 
Ukisikia usiku wa manane ni kati ya saa 7 hadi saa 10 mara nyingi hapo katikati ndiyo matukio mengi ya ajabu ajabu hutokea.
Acha uoga hakuna wa kumteka mtu.
Gari likitoka Kigoma saa 9 hadi lije fika kwenye hayo mapori saa 1 hiyo hapo
 
Acha uoga hakuna wa kumteka mtu.
Gari likitoka Kigoma saa 9 hadi lije fika kwenye hayo mapori saa 1 hiyo hapo
Unakubali au unakataa!
Ebu wapite hiyo saa 9 kwenye hayo mapori tuone,mimi sizungumzii saa moja nazungumzia saa 9 sasa unadai hakuna utekaji hapo hapo unasema kwenye hayo mapori gari zinapita saa 1 asubuhi!
 
Matokeo ya kulazimisha mambo huwa mabaya. Ajali zitakuwa nyingi sana na matukio ya magari kutekwa na majambazi yataongezeka.

Tuwe wavumilivu, SGR itatupa usalama zaidi kusafiri usiku.
Kazi ya jeshi la polisi ni nn?safari ziruhusiwe masaa 24 sio huo upumbavu wa kuanza saa 9 usiku.

Nchi tuna ushamba mwingi sana, mimi naamini wakiruhusu gari ianze safari muda wowote itakuwa salama zaidi kuliko sasa,

wakiruhusu kuanza safari muda wowote hata 6 usiku kila kampuni itaamua ianze safari muda gani na kila abiria ataamua asafiri muda anaotaka na kutakua hamna kukimbizana kama wanavofanya madereva saivi.

Mfano nilipata taarifa ya msiba saa 5 usiku mimi nipo dar na msiba umetokea mkoani, mazishi ni saa 10 jioni kesho yake lkn nilishindwa kuwahi msiba kwasababu hakuna gari inayoondoka usiku huo ila kama kungekua na magari yanaanza safari muda wowte ningeweza kupanda bus la saa 7 usiku na ningewahi.
 
Back
Top Bottom