kas
kashauri kwanza KINANA AKAE PEMBENI shain wahd
 
Noted
 
Ulichoandika hapa simply unamaanisha kiongozi akiwa madarakani chini ya miaka kumi hawezi kufanya makosa, ila atakapozidisha hiyo miaka ndio anaanza kukosea, kitu ambacho hakina mantiki kabisa, ni mawazo yako tu ya kufikirika.

Kiongozi anaweza kukosea muda wowote akiwa uongozini bila kujali miaka aliyohudumu, na kama hili kwako ni tatizo, basi watahitajika malaika washuke kutoka mbinguni ili waje kuongoza taasisi zetu, au kwako kiongozi kukosea akiwa na chini ya miaka kumi uongozini hilo sio kosa, kosa ni pale atakapokosea baada ya kuzidisha miaka kumi, hii nayo haina mantiki kabisa.

Hii hoja yako ya "miaka kumi" nikushauri uitafutie defence ya kueleweka, usitembee na mawazo yasiyoeleweka kichwani miaka na miaka kisha ujifiche kwenye kivuli cha "uhuru wa kutoa maoni"
 
Huyo jamaa anazo nadharia za kipekee sana, na huwezi kumwambia kitu chochote akakielewa.
Kwa mfano: kwa mujibu wake, sasa Tanzania hapawezi kutokea mabadiliko yoyote bila ya uwepo wa machafuko. Yeye anasubiri tu machafuko ndipo atambue kuwa mabadiliko yamepatikana.
 

Time limit kwenye uongozi hiyo ndio demokrasia. Sizungumzii kufanya makosa maana unaweza kufanya makosa hata bila kuwa kiongozi. Ni nadra kuzidi miaka 10 ukabaki kwenye ubora wako. Hili sikulazimishi kulikubali maana Kila mtu ana utashi wake. Kuna tatizo kwenye hilo? Lakini muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeshapita, na ukweli wa hilo uko wazi.
 
Mimi kutoamini unachoamini ww hilo sio kosa lako ni langu. Na siwajibiki popote kwenye kuamini unachoamini ww, kama ambavyo ww huwajibiki popote kwenye ninachoamini Mimi. Hapo kuna shida yoyote boss?
 
Nimeipenda hiyo list hasa Nyerere
 
Sijui huwa haelewi kwa bahati mbaya, au anajitoa akili makusudi ilimradi aonekane yuko tofauti, anachosahau kuwa tofauti na wengine lazima awe na logic, sio tu kuwa tofauti ilimradi ndio " uhuru wa kutoa maoni".
 
Time limit kwenye uongozi pekee sio demokrasia, demokrasia ni pana ambapo inajumuisha; wagombea kufanya kampeni, kuwashindanisha wagombea kwenye uwazi, kura kuhesabiwa, na mwishowe matokeo kutangazwa, hakuna time limit pekee inayoamua ukomo wa uongozi popote.

- Ndio maana siku hizi wanasema; mwisho wa uchaguzi mmoja, ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine.

Huko kulazimisha kwako kuwa akili ya kiongozi huchoka baada ya miaka kumi, hebu tuambie hapa, hiyo akili huchoshwa na kitu gani? na kama unaamini kweli huchoka, kwanini viongozi wastaafu hufuatwa na kuombwa ushauri? unaweza vipi kumuomba ushauri mtu unayedai amechoka akili? Hayo maswali sidhani kama utaweza kuyajibu.

Zaidi, unaposema huzungumzii kufanya makosa, wakati nimeona kwenye main comment yako umeorodhesha majina ya viongozi waliofanya makosa na kudai mwishowe wakapoteza thamani ya uongozi wao, hapo ndipo nazidi kukuona usivyojua kipi unachosimamia, hebu tuliza kichwa jitafakari upya na hii biashara yako ya "miaka kumi" uliyokaririshwa sijui wapi ...
 
Hao viongozi nimetaja walikaa muda gani madarakani. Rejea ubora wao katika miaka kumi ya mwanzo, na miaka baada ya hapo. Sehemu nyingi tu zina time limit, na tunashuhudia zikifanya vizuri kuliko kuliko kufia kwenye kitu.

Hilo la time limit hasa miaka 10 sikulazimishi ww ulikubali, na hiyo ni haki yako na naiheshimu. Mimi Nina mifano inayonipa nguvu hiyo, na kwa kutetea mtazamo wangu nimeweka majina ya hao viongozi, wala sikulazimishi ww kukubali popote. Ufahamu hapa ni jukwaani Kila mtu ana mtazamo wake na sio Sheria natunga. Kama unaamini mtu kufia madaraka hiyo ni haki yako, na sina tatizo nayo kabisa. Hii ndio demokrasia ninayoamini, ww unaweza kuamini nyingine yoyote uitakayo. Kuna shida yoyote hapo?
 
Mimi kutoamini unachoamini ww hilo sio kosa lako ni langu. Na siwajibiki popote kwenye kuamini unachoamini ww, kama ambavyo ww huwajibiki popote kwenye ninachoamini Mimi. Hapo kuna shida yoyote boss?
Shida ni kuwa na nadharia za kipekee sana, hayo mengine naweza kuyadadavua tu nikiyapa muda mahsusi.
 
Nyie jitoeni ufahamu tu..!!
Mnamchonganisha mbowe na risu, nafikili mnataka sasa risu apatwe na jambo tena muanze kuilalamikia ccm.
 
Mbowe ndiye anayeilostisha Chadema, nahisi anaweza kuwa anafanya haya makusudi kwa kuwa ni kibaraka wa chama tawala. Hivi Mbowe alishawahi rudishaga kadi yake ya CCM na lini atuambie.
 
Ndio maana nikakuuliza maswali kama unaamini ubora wa viongozi hupungua baada ya kuzidisha miaka kumi madarakani, nijibu.

- Kwanini tunawatafuta viongozi wastaafu na kuwaomba ushauri kama unaamini ubora wao hupungua?

- Unawezs kumuomba ushauri mtu aliyechoka akili?

Hayo maswali mawili nimekuwekea hapo, simply kukuonesha vile ulivyo na mtazamo hasi, usioendana na uhalisia popote pale hapa duniani, huo mtazamo upo kwenye kichwa chako pekee, na hapa usilete kisingizio cha "tupo jukwaani" ili kutafuta justification ya upotofu unaouamini, ulio kinyume na uhalisia wa ulimwenguni kote.
 
Kwanini nini usishauri mwenyekiti wa ccm awe makonda au sabaya? Chadema inakuhusu vipi?
Naunga mkono hoja,Makonda na Sabaya ni vijana wenye maamuzi magumu kuliko Mwenyekiti wao pamoja na katibu wake,Makonda awe mwenyekiti achukue nafasi ya Samia na Sabaya awe Katibu achukue nafasi ya Kinana ,halafu mwisho Mwenezi wao awe Msukuma au Kibajaji,hapo vipi?
 
Shida ni kuwa na nadharia za kipekee sana, hayo mengine naweza kuyadadavua tu nikiyapa muda mahsusi.
Mkuu ni kosa kuwa na nadharia za kipekee? Ninawajibika kwa ninachoamini kwanza, kisha hicho unachoamini ww ni juu yangu kukiamimini ama la.
 

Ninaamini kabisa ubora wa kiongozi hupungua baada ya muda Fulani, kwangu miaka 10 ni kipimo Bora kabisa, siwajibiki kwenye muda unaoamini ww Wala kukukatalia popote. Uzuri Nina mifano ya ninachoamini. Huyo Mbowe ni mmoja ya case study yangu ya kiongozi kukaa zaidi ya miaka kumi kwenye nafasi Moja ya kuteuliwa.

Kumfuata kiongozi mstaafu akupe ushauri, sio kumtaka arudi kuongoza. Kuna tofauti kubwa ya kuomba ushauri kwa mstaafu, na kuongoza. Ni kipi hakieleweki hapo?!

Mkuu ninasisitiza tena, ninachoamini hakimshurutishi yoyote kukiamini hata nikibaki mwenyewe kwenye hili ninaloamini. Kwangu Mimi miaka 10 ni muda tosha kabisa kwa kiongozi kukaa kwenye nafasi Moja ya kuchaguliwa hii ni bila kujali ww unaamini kwa muda gani, ama unatumia vigezo gani vingine. Wangalau miaka 15 kwa shingo upande. Baada ya hapo hata nishikiwe bastola siwezi kukubali hali hiyo. Sioni unapata wapi shida kwa jambo ambalo naamini mimi, wakati huo huo Sina tatizo na unaloamini ww, shida Iko wapi hapa?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…