@TazamaRDC_Infos
Translated from French by
#Guerre_du_M23 : The air defense of #FARDC is now operational despite the absence of an official press release.At 11:50 a.m. this Friday, the position of #M23_RDF in Kanyangohe, in the locality of #Katsiru in the group of #Bukombo , has just been reduced to ashes by a drone strike. Some M23 survivors from surrounding positions are in disarray, says our source in the area.In the territory of #Masisi , in the chiefdom of Bashali Kaembe, since early this morning, clashes have been reported in Kalonge between the #wazalendo and rebels supported by #Rwanda and #Ouganda .
 
Uko sahihi sana. Hili linasemwa hata na askari wetu waliofanya tour ktk mission za Congo. Wanasema UN wanaiba lakini wao wanakatazwa na makamanda hata kuchukua au kutoka na dhahabu hata jiwe moja dogo. Na ndiyo maisha yao. JW hawaibi madini. Sasa kwa.mpango uliousema maana yake tutalipwa na Congo na hatutakuwa chini ya mwavuli wa UN au majeshi ya AU.
 
Umenipata vyema. Tukae chini tutengeneze specific strategy na policy kwaajili ya Congo. Tukae pia na Belgium, ambaye ndio mnufaika mkubwa wa hii vita tumwonyeshe wazi kuwa anaweza kuendelea kupata supply ya hayo madini na amani ikawepo Congo. Tukiamua naamini ndani ya muda mfupi pale patatulia.

Tupeleke manpower ya kutosha, CCP pale vijana wachemshe miguu wengi waondoke huko mitaani. JW wakiwatoa waasi eneo tunajaza askari wa kawaida, tunaweka vituo vya polisi, wanahakikisha maisha ya raia yanakuwa smooth.

Unajua shida ni kutoa watu eneo halafu ukaliacha tupu bila uongozi..
Unaposonga kwenye maeneo mengine huku nyuma cells za adui zinarudi kujipanga.

Tutengeneze structure ambayo baadae tutakuja kuwarithisha wakongo wenyewe.

Nakuhakikishia tukifanya hivi, Tanzania itakuwa tajiri soon enough
 
Naona jeshi letu lipo ktk ukombozi zaidi kuliko manufaa lakini hii ndiyo njia ya majeshi yote ya kisasa duniani. Rwanda atafanya hivyo huko Central Africa, Mozambique na hata hapo Kongo kwa njia ya M23
 
Naona jeshi letu lipo ktk ukombozi zaidi kuliko manufaa lakini hii ndiyo njia ya majeshi yote ya kisasa duniani. Rwanda atafanya hivyo huko Central Africa, Mozambique na hata hapo Kongo kwa njia ya M23
Kwanza hizo policies na strategies sio kazi ya Jeshi.. ni kazi wa wizara husika na serikali.

Pili, kupanga ni kuchagua! Kagame faida anayotupa kwa kudeal nae huwezi kuilinganisha na faida tunayoweza kupata Congo.

Tatu, nafikiri ni Chinua Achebe alisema dawa chungu ndio dawa nzuri. Tukimfundisha kagame jinsi ya kuendesha uchumi wa nchi kihalali, in the long term itakua faida kubwa kwa Rwanda hata wakati ambako Kagame atakua hayupo.

Ukiangalia vizuri huu mfumo wa kuiba Congo ndio unaosumbua hata ulinzi wa ndani wa Rwanda, Burundi na Uganda..
Wale wanaotumwa kuiba wanachukua kikubwa kuliko wanachopeleka..
Hivyo wana nguvu za kuyumbisha hata serikali zao.
Ukisikia watu wako msituni ujue hawali mawe...
 
Pointi za kutosha ila vichwa panzi humu wengi hawatokuelewa
 
M23 hawana lolote wapigwe na wameuwawa haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…