Samia anaifanya sana kazi, ukiona hawa wengi wanaompinga sababu za kisiasa zipo nyuma ya hoja zao. Wengi walitanua sana awamu ya tano huko kwenye halmashauri na mawizarani amekuja Samia wameshindwa kuuweka sawa ule mrija wao wa upigaji.
Sio kweli .
JPM alijenga sana nchi kitaasisi .
Na kimiundo mbinu .
Hivi unaona magari yanayonunuliwa huko Halmashauri na idara Nyingine yalivyo ya kifahari na ya bei kubwa . Hilo nalo kweli ni jambo la kutumia darubini kuona kuwa linamaliza fedha za maendeleo .
Masoko yalijengwa vizuri ili kukusanya Fedha , Madaraja na barabara za lami ili kuonoka na tenda za kila siku kupiga pesa za kujenga miundo mbinu duni .
Umeme ulishuka bei mpaka elfu 27 na maji elfu 24 tu .
Na uchumi wa nchi ukawa imara .
Na watu walikua wanafanya kazi sana kwa akili na maarifa sio ujanja ujanja na kupeana mapesa ya kugawa kwenye nyumba za ibada na wasanii na machawa .
Hatua zilikua zinachukuliwa .
Hata nchi zilizoendelea sana labda uarabuni ambapo wana mifumo ya kifalme lakni hakuna watumishi wa umma wanaotumia fedha za umma kufanya starehe wakati huduma za jamii ziko chini sana.
Watu wanateseka na matibabu ya figo huku Tanganyika ambako kuna rasilimali nyingi sana lakini binadam hao hao kule Zanzibar wanapata huduma hiyo bure .
Wakati kodi ikiwa juu huku Tanganyika kule Zanzibar iko chini. Lakni cha ajabu asilimia kubwa ya Wazanzibari wapo kwenye ajira ama ya serikali yao au ya jamhuri pamoja na idadi ndogo ya watu . Yaani ukigawa ukubwa wa kanchi ka Zanzibar na idadi ya viongizi walionao ni kama vile kila kijiji kina mbunge na mwakilshi na diwani na sheha. Wajati huo bado mawaziri wengi katika serikali yao wenyewe na wakuu wa mikoa na wilya na viongozi wengi lakni pia idara zote kule Zanziba hawaajiri Watanganyika.
Sasa kwa hali hiyo ni lazimawaje kupora rasilimali za Tanganika ili kujinufaisha kwa sababu Watangayika wengi wanafanya shughuli zao binafsi hawana hanari na siasa na madaraka