Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

LISSU: Ndiyo madhara ya kuzuiwa kuniona.

Wangeruhusiwa kuniona, yasingekuwa hivi
Ndiyo uhalisia na Ukweli, kwanini kuwazuia Mawakili wake,Wanachama wenzake,Ndugu na marafiki? Mhaini anayependwa hadi na Mabeberu waliotunga Sheria za kidunia(Musungu) ambazo tume copy&paste.
Bi msumi mesababisha kutekwa,kubakwa,kubambikia kesi na kuuliwa waliompigia kura 98% !Atarudia eda.
Mh.Lissu aachiwe Huru awasidie kupooza joto,mnakumbatia moto na Moshi tunaouona?
 
MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISSU

LISSU: Sasa naomba nimalizie.

JAJI NDUNGURU: Je, ni sehemu ya submission?

LISSU: Ni sehemu ya submission, wala si maneno mabaya.

Ni hivi, Waheshimiwa Majaji, kesi ya uhaini ni kesi ngumu sana.

Ukiachilia mbali siasa zake, ambazo pressure zake ndizo zinafanya kesi kuwa ngumu.

Pamoja na kesi kuwa ngumu, nyinyi Majaji mmefanya kazi nzuri sana.

Mmetusikiliza, mmetupa nafasi ya kujitetea.

Hamjanikwaza.

Mmekuwa wavumilivu sana.

Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi nzuri sana.

Nilitaka nisimalize bila kusema haya, pengine hatutakutana tena.

Nilitaka mjue kuwa moyoni mwangu mmefanya kazi nzuri.

Hawa mawakili wangu wa Serikali na wao wamefanya kazi nzuri.

Wamepambana sana mpaka kufika hapa. Pamoja wamekuwa na kesi ya ovyo sana.

Ila wamepambana sana bila kujali nini kitatokea, wamepambana sana.

Nafikiri nawatakieni heri sana.

Asanteni sana.

Haya ndiyo nilitaka yaingie katika rekodi.

Nafikiri msipoyaingiza katika rekodi, mtanikwaza.
 
Ila Lisuu ni mtu sana
 
Hitimisho safi kabisa, mtu asiye na kisasi na yeyote pamoja na kuona figisu zote za kesi hii

Ni fahari kusoma hitimisho lake, proceedings za kesi hii zitabaki hapa JF hata baada ya sisi wote kuondoka Duniani

Amewafundisha akina Katuga sheria kwa mara nyingine baada ya kutoka Law school πŸ™πŸ™
 
Kwa kesi hii, mahakama zimeonekana za kifala.
 
Ona nyumbu wengine badala ya kujibu
Hoja

Wanatafuta majibizano wanayo yaweza nayo!!!
ni kutaja viungo vya Uzazi tu!!!!!

Ndio MAKAMANDA wasasa Chadema!!
chini ya Mwenyekiti mpya ndugu Lissu yasasa!!!!!!
Ubwabwa upo ondoa shaka
 
Kasho tukutane
Mana uyu mhe Lissu alitamani kuendelea mpaka ijumaa

Yote kagundua
Wenzie walikuwa makini kujenga Mashtaka yao na kuthibitisha makosa yake!!!

Mwisho muhimu Amani ya kila mmoja wetu
Ikiwemo na yake Lissu

Baada kwisha kesi hii
Watanzania tunatakiwa kutafakari Msingi kile kimetokea

Wenzetu wamekufa kwasababu za Kisiasa !!!

Tunapaswa kuwa Makini sn
siku zijazo!!!!
 
Yaani hata kama watu hatuna uzoefu na kesi za mahakamani lakini hii ni kesi nyepesi Sana kuwahi kushuhudia alafu wanataka kuifanya iwe nzito na ngumu yaani upande wa mashitaka Hawana points za msingi hata kidogo hata mtu mwenye uelewa mdogo analijua Hilo tumefatilia apa kuona ushaidi wao una uzito kiasi gani hamna kitu yaani
 
Upo sahihi. Kesi imekaa kisiasa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…