Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Umekurupuka maswali yote hayana mashiko ukweli unabaki hapohapo wananchi wengi hawakubaliani na suala la ubinafsishaji wa bandari kwa sababu ya mkataba mbovu hilo liko wazi habari za takwimu msituulize Ila kama nyie mnazo za kwenu wa wengi kukubali zilete hapa na wakati huohuo mtueleze kwa nini mnahangaika kubadili sheria ili kufunika maovu yaliyopo katika huo mkataba kwa nini serikali inahangaika unataka kufanya utapeli gani kwenye rasilimali za Taifa?

Maamuzi ya mahakama hatujayakubali na ndio mana tutakata rufaa ngoja Mwabukusi na team yake wapumue kwanza baada ya kuwa huru leo tunarudi vitani
Mfumo wa vyama vingi ulikataliwa na wananchi mbona Serikali walifanya maamuzi kuuanzisha? Wao waliwahi kutoaga tamko kupinga?
 
Hawataki kwa sababu ya uelewa mdogo wa nini kinachokwenda kufanyika, hawataki kwa sababu ya kudanganywa na wapigaji wa bandarini na wao wakaingia kichwa kichwa kwenye siasa za kibaguzi.

DPW wapo katika bandari za maana za dunia hii, UK, USA, China kote huko wapo, eti Tanzania wasiwepo kwa sababu waarabu inaaminika wanataka kurudisha sera za utumwa mwaka 2023!!.

Hatupo informed wabongo na hatujui kwamba hatujui lolote.
Shida sio DP World. Shida ni huu mkataba una maslahi kiasi gani kwa wana siasa wa Tanzania?
Wana siasa wetu haaminiki labisa na hawajali kabisa nini kinaweza kutupata sababu ya negligence zetu. Mfano halisi ni hizo kesi za mikataba tunazoendelea kushindwa
 
Hawataki kwa sababu ya uelewa mdogo wa nini kinachokwenda kufanyika, hawataki kwa sababu ya kudanganywa na wapigaji wa bandarini na wao wakaingia kichwa kichwa kwenye siasa za kibaguzi.

DPW wapo katika bandari za maana za dunia hii, UK, USA, China kote huko wapo, eti Tanzania wasiwepo kwa sababu waarabu inaaminika wanataka kurudisha sera za utumwa mwaka 2023!!.

Hatupo informed wabongo na hatujui kwamba hatujui lolote.
Kasome masharti ya hiyo mikataba ya uwekezaji kwa nchi ulizozitaja ulinganishe na wa kwetu ndiyo utafahamu kwa nini watu wanapinga huu mkataba ulivyo na si ku question uwezo wa DPW.
 
Wao wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari kesho BAKWATA wakitoa tamko Serikali iendelee na mkataba wa Bandari wanataka Serikali imsikilize nani? Kesho kutwa mabudha wakitoa tamko pia wanataka Serikali imsikilize nani kati yao?
Wameshauri tu na sio lazima ushauri wao ufuatwe
 
1. Wanadai Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo!
Swali langu kwao, Ni jambo lipi nchi hii limewai kukubaliwa na asilimia 100 ya wananchi wote? Kwenye Mfumo wa vyama vingi, Mbona asilimia kubwa ya Wananchi walikataa mfumo huo ila Serikali wakauunga mkono! Je kwa nini hawakutoa tamko kipindi icho kutaka nchi iendelee kuwa ya Chama kimoja? Kwa tamko lao walilosema maamuzi ya wananchi yaheshimiwe basi wanaungana mkono Serikali I reverse maamuzi yake ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja?

2. Kwenye tamko lao wanadai Mihimili ya dola iheshimiwe. Swali langu kwao! Juzi Mahakama Kuu wametoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya watu walioshtaki mkataba wa Bandari.

Sasa kwa nini wanataka mihimili ya dola iheshimiwe na wao hawataki kuheshimu maamuzi ya Mahakama? Kama Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hasa ibara ya 107A inasema Mahakama ndio Mhimili wa mwisho katika kutoa haki sasa kwa nini hawaheshimu maamuzi ya Mahakama alafu wanatoa tamko kusema Mihimili ya dola iheshimiwe?

3. Wao wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari kesho BAKWATA wakitoa tamko Serikali iendelee na mkataba wa Bandari wanataka Serikali imsikilize nani? Kesho kutwa mabudha wakitoa tamko pia wanataka Serikali imsikilize nani kati yao?

Kwa hali hii sasa naamini kwa nini mapadre wa kanisa katoliki walishtakiwa kwa kuhamasisha mauaji ya kimbari Rwanda!

Mods! Naomba sana msiunganishe huu uzi!!
Hii ni dharau kubwa sana kwa Waislam. Hivi kwa nini huwa mnawadharau sana Bakwata?!!! Hata kama mtu hukubaliana na bakwata ndo uwadharau kiasi hicho? Hivi kweli mnaiona bakwata haijielewi kiasi hicho eti ije itetee mikataba ya kuuza mali za wananchi (waamini) wake?!!!!! Ili iweje?
 
Ndo hapo wanadai mihimili ya dola iheshimiwe.

Bunge lilitoa maamuzi, Mahakama imetoa maamuzi wao hawataki kuheshimu alafu wanasema eti Mihimili iheshimiwe. They don't practise what they preach sasa sijui wana preach nini

Hao sio wajinga.....wanajua nini kinaendelea nyuma ya pazia. Na wana maanisha wanaposema mihimili ya uongozi iheshimiwe
 
Hii ni dgarau kubwa sana kwa Waislam. Hivi kwa nini huwa mnawadharau sana Bakwata?!!! Hata kama mtu hukubaliana na bakwata ndo uwadharau kiasi hicho? Hivi kweli mnaiona bakwata haijielewi kiasi hicho eti ije itetee mikataba ya kuuza mali za wananchi (waamini) wake?!!!!! Ili iweje?
Kwa kifupi ni wajinga.
 
Watu wanaosapoti ule mkataba vilevile ulivyo wanapatikana jamii forums tu na mitandao ambayo watu hawajulikani majina yao halisi. Tangu hili sakata lianze sijawahi kukutana na ndugu, jamaa au rafiki anaye sapoti huu mkataba. Kila sehemu ninapoenda watu wote wanakandia sana. Hata mleta mada vijiweni au maofisini hawezi kuutetea. Ni kichaa peke yake atakubaliana na vile vipengele vinginevyo kama mtu ana maslahi binafsi au kashalamba ela za DP WORLD 🌎.
Mpaka vijiwe vya ghahawa waislamu hawauungi mkono maana washenzi baadhi wanataka kutengeneza sakata hili kwa sura ya kiimani.
 
Mkataba wa bandari ni mkataba wa kurudisha utawala wa sultan sio wa kuleta maendeleo

Alichofanya samia ni kusaidia waarabu kuja kutawala TANGANYIKA
Kivipi, hao jamaa walikowekeza kwote wanatawala? Hizi ni hoja zinazoshawishi kweli?
 
Ndo hapo wanadai mihimili ya dola iheshimiwe.

Bunge lilitoa maamuzi, Mahakama imetoa maamuzi wao hawataki kuheshimu alafu wanasema eti Mihimili iheshimiwe. They don't practise what they preach sasa sijui wana preach nini
Hakuna watu wenye akili watawasikiliza wapumbavu hao. Wanadhani hatujui nyuma ya pazia wanapigania nini?
 
Mkiishiwa hoja mnakimbilia kusema watu wamehongwa. Mimi sio wa kihivyo kijana. Jiheshimu!

Jitahidi mkuu utakumbukwa na waarabu labda watakupa kazi ya kusafisha vyoo. Maana elimu yako ya sheria haijakusaidia chochote
 
Mfumo wa vyama vingi ulikataliwa na wananchi mbona Serikali walifanya maamuzi kuuanzisha? Wao waliwahi kutoaga tamko kupinga?
Mfumo wa vyama vingi haukuwa na mambo mengi ya kimangungo kama huu mkataba wa bandari
 
Back
Top Bottom