Mdogo wangu Eeh! Kuoa mwanamke ambaye familia yake imekuzidi kila kitu ni mtihani sana. Usithubutu!

Ukioa kwenye hela na wewe huna hela au status, lazima utaonekana kolo ukweni. Na wao wataona sio hadhi yao, au umekuja kutaka kitonga.
Ni sawa uwe la nne B kama mimi, afu uoe familia watu wamebukua. 😊
Wanakuona MEMKWA tuu.
Ndio nachokipitia mkuu yaani kila nikijitahidi kujiattach na kujipendekeza pendekeza napigwa knok out nakaa pembeni kwanza ila naona dharau za mke na wakwe zangu zimezidi
 
nyie tena, hamtaki kujiattach kwenye familia za kishua?
Mi nashangaa sana watu wanashindwaje kujiattach kwenye familia za kishua? Mbona familia za kishua hazina taabu. Kuna namna mwanaume unatakiwa kuwa ili uweze kujiattach kwenye familia zenye uwezo.Ukijua kuishi na watu hakuna mahali utashindwa kuishi. Inatakiwa Mama mkwe awe mpenzi na baba mkwe awe mshikaji, utatoboa.
 
Kwa hiyo mkuu mpaka kupikiwa nako nipangiwe ratiba namwambia anipikie ananiambia agiza Msosi app yeye ameshachoka na anaenda kulala hivyo si dharau hizi
 
Ndugu yangu, pole sana kwa ulichopitia. Lakini usikubali kikao cha leo kikufanye uamini kwamba thamani yako kama mwanaume inapimwa kwa mali, elimu au uwezo wa familia ya mke wako. Ndoa si mashindano ya nani anamzidi nani.


Kama kuna tatizo kwenye ndoa, linapaswa kutatuliwa na wewe na mke wako kwa heshima, si kila jambo kupelekwa ukweni mpaka mmoja avuliwe heshima. Maneno ya “ukimshindwa mrudishe” yanaumiza, lakini usijibu maumivu kwa hasira au pombe.


Kwa sasa tuliza akili kwanza. Usifanye uamuzi mkubwa ukiwa umelewa au umejaa hasira. Kesho ukiwa umetulia, kaa na mke wako muongee wazi kuhusu mipaka ya familia zenu, heshima na namna ya kufanya maamuzi ya ndoa.


Na usijilaumu kwa kuoa mtu ambaye kwao wana uwezo mkubwa. Kinachotakiwa ni mwenza anayekuheshimu na anayesimama na wewe, si anayekufanya ujisikie mdogo kwa sababu ya tofauti za uwezo wa familia. Heshima ikikosekana, hata nyumba kubwa inaweza kuwa gereza.
 
Unamaanisha uishi kama Mwijaku?
Bro tuwe serious basi kidgo.
Yaani ujikombe tu maximum.? Kwa mwanaume sio sawa labda kama una damu kama ya Mwijaku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…