Mkataba wa kuendesha Bandari za Tanzania wa DP WORLD ya Dubai hautazihusu Bandari za Zanzibar
Mkataba unahusu bandari ya Dar es salaam tu na SI vinginevyo. Fuatilia mijafala ya kibunge na hoja ya waziri
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WADAU
Siasa nyingine nyepesi ni huu uzi. Bandari ya Zanzibar ni ndogo sana kulinganisha na ile ya Dar. SSH ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kazi kwa niaba ya watanzania wote.

Chuki na ubaguzi unakuja kutokana na watu kulishwa matango pori na kuaminishwa kuwa wazanzibari hawana nia njema ya watu wa bara. Kitu ambacho ni uongo wa mchana kweupe.

Tunawasema wazenji ni wabaguzi, vipi kuhusu ubaguzi wetu sisi wenyewe huku bara?. Vipi kuhusu ubaguzi wa awamu ya tano wakati JPM alipoamua kwa makusudi kuwainua jamaa wa kabila lake?.
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amehoji kwanini Bandari za Zanzibar hazimo Kwenye Mkataba wa Dubai

Mbowe amesema kama Mkataba ni Mzuri mbona Bandari za Zanzibar hazimo?

Chanzo: Jambo TV

My take: Zanzibar ni nchi
Mbowe kaongea kutafuta mileage za kisiasa tu. Bandari ya Zanzibar utailinganisha vipi na hii ya Dar?.
 
A huge miscalculation by SSH. Watanzania (watanganyika) wameibiwa sana kwa mgongo wa ubinafsishaji, yaani serikali inatumia matrilioni kuwekeza kwenye kitu alafu mwisho wa siku wahuni wachache wanapiga dili na kuuziwa kwa bei za kutupa.

Imetokea tena na tena na tena, ATCL, TTCL, TRC, NBC, mashamba ya serikali, nyumba za serikali, viwanda vya serikali na mengine mengi. Bado CCM haijifunzi tu??

Watu wanamlaumu JPM kuwa alikuwa katili lakini bwana yule alikuwa na akili za kutatua changamoto, akiona sehemu kuna mapungufu basi anaumiza kichwa kuona taitizo ni nini, watu? Mifumo? Sheria? Kisha anajaribu kutatua.
Mwacheni Mama Afanye KAZI Yake
 
Siasa nyingine nyepesi ni huu uzi. Bandari ya Zanzibar ni ndogo sana kulinganisha na ile ya Dar. SSH ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kazi kwa niaba ya watanzania wote.

Chuki na ubaguzi unakuja kutokana na watu kulishwa matango pori na kuaminishwa kuwa wazanzibari hawana nia njema ya watu wa bara. Kitu ambacho ni uongo wa mchana kweupe.

Tunawasema wazenji ni wabaguzi, vipi kuhusu ubaguzi wetu sisi wenyewe huku bara?. Vipi kuhusu ubaguzi wa awamu ya tano wakati JPM alipoamua kwa makusudi kuwainua jamaa wa kabila lake?.
Hayo mengine ni yako wewe , sisi tumeandika uzi kuhabarisha umma wa Watanzania mipaka ya Waarabu kwenye uwekezaji wao baaaasi
 
Kuwekeza ni mikakati ya miaka na miaka na huu wa DP World haukuanza na urais wa SSH ni kazi ya toka nyakati za JPM. Aliyeamua kujenga reli ya SGR kwa nguvu zake zote, ili kuongeza mzigo unaotoka na unaoingia nchini.

Kwanini SSH anakutana na matusi pamoja na ubaguzi wote huu?. Kaamua kuipambana vita ya kiuchumi kikamilifu.
 
Huu ni utoto, Samia alikuja na sera ya kufungua nchi. Tulishangilia na kila aina yaa sifa
Akaenda Dubai mwaka Jana akasaini mikataba hii, tukashangilia na kusema raisi ndio huyu anayesafiri na kuleta wawekezaji sio Kama Magufuli ambae alikua hasafiri kabisa

Leo ime-backfire unataka kusema eti ilikuwepo muda mrefu. Mpeni Samia sifa zake kama mlivyompa kipindi anasafiri na kusaini mikataba

Mwisho kabisa kinacholalamikiwa zaidi ni terms za mkataba
 
Ni uelewa wa watu fulani wenye sera zenye chembe chembe za ubaguzi, hakuna kilicho back-fire hata kimoja.

Hizo terms za mikataba ndizo zinazokwenda kujadiliwa kuanzia muda huu, kama unayo mawazo yenye kulinda maslahi ya nchi usikubali ubakie nayo moyoni mwako kisha uende ukalalamike katika vijiwe vya maongezi ya jioni, huu ndio muda wa kuweka wazi hisia zote tulizonazo.
 
Ingekua haijabackfire nguvu kubwa isingetumika hivi.

Hayo mawazo nilipaswa kuyatoa kabla ya mkataba, kabla hata ya raisi kwenda kusaini kule Dubai.
Juzi spika aliwaambia, Kama haujasainiwa hakukuwa na haja ya kupelekwa bungeni ili fanya ratification. mkataba unasainiwa kwanza ndio uende bungeni kufanyiwa ratification kama walivyofanya
 
Sikulenga kitu nimeweka bayana kuwa wewe ni mbaguzi na mdini na mko wengi tu. Hamkupiga kelele bandari ya zanzibar walivyopewa wafarnsa lakini mnaanaza kutaja asili za mawaziri na raisi kana kwamba wao sio watanzania na hawana madaraka ya kufanya maamuzi yanahusu Tanzania. Dont get me wrong issue yote ya bandari inanuka uvunda lakini tatizo langu juu yako ni kuanza kulet mambo ya ukabila na udini. tuko mwaka 2023 na Tanzania bado kuna watu kama wewe ambao hamuoni watanzania wenzenu kama ni watanzania bila kujadili imani zao au wana asili ya pande gani wa tanzania.

..Wizara ya Ujenzi si ya muungano.

..Mzanzibar ana haki ya kuongoza wizara za muungano, kama fedha, mambo ya ndani, etc.

..Mzanzibari hana haki ya kuongoza wizara au taasisi zisizo za muungano, kama wizara ya ujenzi, kilimo, afya, ..

..Kwa msingi huo, uteuzi wa Prof.Mbarawa kuongoza wizara isiyo ya muungano una makosa.
 
Ni uelewa wa watu fulani wenye sera zenye chembe chembe za ubaguzi, hakuna kilicho back-fire hata kimoja.

Hizo terms za mikataba ndizo zinazokwenda kujadiliwa kuanzia muda huu, kama unayo mawazo yenye kulinda maslahi ya nchi usikubali ubakie nayo moyoni mwako kisha uende ukalalamike katika vijiwe vya maongezi ya jioni, huu ndio muda wa kuweka wazi hisia zote tulizonazo.

..Luhaga Mpina wa Ccm ametoa maelezo mazuri.

..Tundu Lissu wa Cdm ametoa ufafanuzi mzuri.

..Kilichopitishwa na bunge ni MSINGI wa hiyo mikataba itakayokuja kusainiwa.

..Kuna wanaosema mkataba kati ya DP na bandari utakuwa kama ule wa Ticts.

..Lakini mimi sikusikia Bunge likipitisha azimio la " kuruhusu " majadiliano kati ya bandari na Ticts. Naomba kusahihishwa.

..Maazimio ya Bunge huwa ni kwa masuala mazito kama mikataba ya East African Community, na SADC, si kwa masuala ya uwekezaji wa makampuni toka nchi za nje.

..Labda serikali ingetoa maelezo ya kina kwanini wanahitaji azimio la bunge ktk suala la uwekezaji bandarini.

..Kwanini wanahitaji hilo azimio, wakati huko nyuma hawakulihitaji?

..Mazingira hayo ndiyo yanayozua taharuki kwamba kuna jambo kubwa la kifisadi wamepanga dhidi ya bandari lakini hawako tayari kulieleza kwa wakati huu.
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WA
 
Tanganyika tunafungwa minyororo ya utumwa kwa Mara nyingine why not Zanzibar? TunatakabTanganyika huru!Tanganyika huru no Sasa!!!!!!!!!!?watanganyika amkeni! amkeni!amkeni! Huko mliko acheni Mambo za kushangilia Simba na. Yanga,Tanganyika kwanza! Tanganyika ni kubwa kuliko Simba na Yanga,kwenye ubinafsishaji watanganyika hatujawahi kufanya vizuri,tukipigwa Sana,tuliibiwa saaana,rejea ubinafshaji wa NBC,TRC,RICHMOND,IPTL,,ATCL,TIPER,kote huko tukipigwa saan,Hawa viongozi Hawana uchungu na raslimali za nchi hii,wanafanya Mambo Kama wanajiandaaa kufa kesho,wasitegemee kuishi Tena kesho,Amkeni watanzanzania Sera za kukunana migongo zimeanza Tena Bora magufuli alizikataa AMKENIIII
Wanakusikia sasa hawa, naona mijadala mingi mtaani ni kombe last shirikisho kati ya Azam na Yanga, hamna mtu ana muda na bandari, so sad enough.
 
..Luhaga Mpina wa Ccm ametoa maelezo mazuri.

..Tundu Lissu wa Cdm ametoa ufafanuzi mzuri.

..Kilichopitishwa na bunge ni MSINGI wa hiyo mikataba itakayokuja kusainiwa.

..Kuna wanaosema mkataba kati ya DP na bandari utakuwa kama ule wa Ticts.

..Lakini mimi sikusikia Bunge likipitisha azimio la " kuruhusu " majadiliano kati ya bandari na Ticts. Naomba kusahihishwa.

..Maazimio ya Bunge huwa ni kwa masuala mazito kama mikataba ya East African Community, na SADC, si kwa masuala ya uwekezaji wa makampuni toka nchi za nje.

..Labda serikali ingetoa maelezo ya kina kwanini wanahitaji azimio la bunge ktk suala la uwekezaji bandarini.

..Kwanini wanahitaji hilo azimio, wakati huko nyuma hawakulihitaji?

..Mazingira hayo ndiyo yanayozua taharuki kwamba kuna jambo kubwa la kifisadi wamepanga dhidi ya bandari lakini hawako tayari kulieleza kwa wakati huu.
Ukubwa wa kinachokwenda kufanyika. Mawanda ya biashara zinazotegemewa kuingiwa katika makubaliano ya pande zote mbili.

Hizi ni biashara kubwa zinazokwenda kubadili kabisa utendaji kazi uliozoeleka bandarini. Ni mradi mkubwa unaogusa maslahi ya wadau wengi wa biashara wa ndani na wa nje.

Safari ya kwenda uchumi wa juu wa kati mwanzo wake ni kujiamini lakini watanzania tumekosa hiyo sifa tunataka kwenda mbinguni lakini kifo tunakiogopa.
 
Back
Top Bottom