Mkataba unahusu bandari ya Dar es salaam tu na SI vinginevyo. Fuatilia mijafala ya kibunge na hoja ya waziri
 
Siasa nyingine nyepesi ni huu uzi. Bandari ya Zanzibar ni ndogo sana kulinganisha na ile ya Dar. SSH ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kazi kwa niaba ya watanzania wote.

Chuki na ubaguzi unakuja kutokana na watu kulishwa matango pori na kuaminishwa kuwa wazanzibari hawana nia njema ya watu wa bara. Kitu ambacho ni uongo wa mchana kweupe.

Tunawasema wazenji ni wabaguzi, vipi kuhusu ubaguzi wetu sisi wenyewe huku bara?. Vipi kuhusu ubaguzi wa awamu ya tano wakati JPM alipoamua kwa makusudi kuwainua jamaa wa kabila lake?.
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amehoji kwanini Bandari za Zanzibar hazimo Kwenye Mkataba wa Dubai

Mbowe amesema kama Mkataba ni Mzuri mbona Bandari za Zanzibar hazimo?

Chanzo: Jambo TV

My take: Zanzibar ni nchi
Mbowe kaongea kutafuta mileage za kisiasa tu. Bandari ya Zanzibar utailinganisha vipi na hii ya Dar?.
 
Mwacheni Mama Afanye KAZI Yake
 
Hayo mengine ni yako wewe , sisi tumeandika uzi kuhabarisha umma wa Watanzania mipaka ya Waarabu kwenye uwekezaji wao baaaasi
 
Hayo mengine ni yako wewe , sisi tumeandika uzi kuhabarisha umma wa Watanzania mipaka ya Waarabu kwenye uwekezaji wao baaaasi
Kuwekeza ni mikakati ya miaka na miaka na huu wa DP World haukuanza na urais wa SSH ni kazi ya toka nyakati za JPM. Aliyeamua kujenga reli ya SGR kwa nguvu zake zote, ili kuongeza mzigo unaotoka na unaoingia nchini.

Kwanini SSH anakutana na matusi pamoja na ubaguzi wote huu?. Kaamua kuipambana vita ya kiuchumi kikamilifu.
 
Huu ni utoto, Samia alikuja na sera ya kufungua nchi. Tulishangilia na kila aina yaa sifa
Akaenda Dubai mwaka Jana akasaini mikataba hii, tukashangilia na kusema raisi ndio huyu anayesafiri na kuleta wawekezaji sio Kama Magufuli ambae alikua hasafiri kabisa

Leo ime-backfire unataka kusema eti ilikuwepo muda mrefu. Mpeni Samia sifa zake kama mlivyompa kipindi anasafiri na kusaini mikataba

Mwisho kabisa kinacholalamikiwa zaidi ni terms za mkataba
 
Ni uelewa wa watu fulani wenye sera zenye chembe chembe za ubaguzi, hakuna kilicho back-fire hata kimoja.

Hizo terms za mikataba ndizo zinazokwenda kujadiliwa kuanzia muda huu, kama unayo mawazo yenye kulinda maslahi ya nchi usikubali ubakie nayo moyoni mwako kisha uende ukalalamike katika vijiwe vya maongezi ya jioni, huu ndio muda wa kuweka wazi hisia zote tulizonazo.
 
Ingekua haijabackfire nguvu kubwa isingetumika hivi.

Hayo mawazo nilipaswa kuyatoa kabla ya mkataba, kabla hata ya raisi kwenda kusaini kule Dubai.
Juzi spika aliwaambia, Kama haujasainiwa hakukuwa na haja ya kupelekwa bungeni ili fanya ratification. mkataba unasainiwa kwanza ndio uende bungeni kufanyiwa ratification kama walivyofanya
 

..Wizara ya Ujenzi si ya muungano.

..Mzanzibar ana haki ya kuongoza wizara za muungano, kama fedha, mambo ya ndani, etc.

..Mzanzibari hana haki ya kuongoza wizara au taasisi zisizo za muungano, kama wizara ya ujenzi, kilimo, afya, ..

..Kwa msingi huo, uteuzi wa Prof.Mbarawa kuongoza wizara isiyo ya muungano una makosa.
 

..Luhaga Mpina wa Ccm ametoa maelezo mazuri.

..Tundu Lissu wa Cdm ametoa ufafanuzi mzuri.

..Kilichopitishwa na bunge ni MSINGI wa hiyo mikataba itakayokuja kusainiwa.

..Kuna wanaosema mkataba kati ya DP na bandari utakuwa kama ule wa Ticts.

..Lakini mimi sikusikia Bunge likipitisha azimio la " kuruhusu " majadiliano kati ya bandari na Ticts. Naomba kusahihishwa.

..Maazimio ya Bunge huwa ni kwa masuala mazito kama mikataba ya East African Community, na SADC, si kwa masuala ya uwekezaji wa makampuni toka nchi za nje.

..Labda serikali ingetoa maelezo ya kina kwanini wanahitaji azimio la bunge ktk suala la uwekezaji bandarini.

..Kwanini wanahitaji hilo azimio, wakati huko nyuma hawakulihitaji?

..Mazingira hayo ndiyo yanayozua taharuki kwamba kuna jambo kubwa la kifisadi wamepanga dhidi ya bandari lakini hawako tayari kulieleza kwa wakati huu.
 
 
Wanakusikia sasa hawa, naona mijadala mingi mtaani ni kombe last shirikisho kati ya Azam na Yanga, hamna mtu ana muda na bandari, so sad enough.
 
Ukubwa wa kinachokwenda kufanyika. Mawanda ya biashara zinazotegemewa kuingiwa katika makubaliano ya pande zote mbili.

Hizi ni biashara kubwa zinazokwenda kubadili kabisa utendaji kazi uliozoeleka bandarini. Ni mradi mkubwa unaogusa maslahi ya wadau wengi wa biashara wa ndani na wa nje.

Safari ya kwenda uchumi wa juu wa kati mwanzo wake ni kujiamini lakini watanzania tumekosa hiyo sifa tunataka kwenda mbinguni lakini kifo tunakiogopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…