Mkataba wa kuendesha Bandari za Tanzania wa DP WORLD ya Dubai hautazihusu Bandari za Zanzibar
..Wizara ya Ujenzi si ya muungano.

..Mzanzibar ana haki ya kuongoza wizara za muungano, kama fedha, mambo ya ndani, etc.

..Mzanzibari hana haki ya kuongoza wizara au taasisi zisizo za muungano, kama wizara ya ujenzi, kilimo, afya, ..

..Kwa msingi huo, uteuzi wa Prof.Mbarawa kuongoza wizara isiyo ya muungano una makosa.
Magufuli aliyempa ubunge kabisa na baadae akampa uwaziri wa mawasiliano na uchukuzi alifanya makosa?.
 
Magufuli aliyempa ubunge kabisa na baadae akampa uwaziri wa mawasiliano na uchukuzi alifanya makosa?.
..Magufuli hakukosea kumteua Prof.Mbarawa kuwa mbunge.

..lakini alikosea kumteua Mbarawa waziri ktk wizara isiyo ya muungano.

..hili jambo tumelisema kwa muda mrefu ili Ccm haiheshimu hisia na maoni ya wananchi.

..Hata Shaka Hamdu kuteuliwa ukuu wa wilaya huku Tanganyika ni makosa.

..Binafsi maoni yangu hayajamlenga Prof.Mbarawa binafsi, au Rais Ssh.

..Hata Marais wa Kitanganyika kuna wakati wamevunja sheria kwa kuteua Wazanzibar ktk wizara na taasisi zisizo za muungano.
 
..Magufuli hakukosea kumteua Prof.Mbarawa kuwa mbunge.

..lakini alikosea kumteua Mbarawa waziri ktk wizara isiyo ya muungano...
Mwalimu Nyerere aliunganisha udongo wa nchi hizi mbili. Alitanguliza upendo zaidi hata hotuba zake zina msingi wa upendo.

Watanzania kama alivyosema Mwalimu Nyerere tukiguswa kidogo tunakimbilia kwenye ukabila na ubaguzi, na ndio hiki kinachotokea muda huu.

Mungu kwa neema na ukubwa wake atatuvusha salama.
 
Philipo umelipwa bei gani ?
Moyo wa uzalendo tu mkuu Erythrocyte. Kwanini hii biashara ya DP World iende ikamfaidishe jirani Kenya au Msumbiji wakati kuna reli ya SGR imeshatandikwa ardhini kwa mabilioni ya pesa?.

Ni uzalendo kuitetea nchi yangu na kusikitikia huu ukosefu wa upeo unaolikabili taifa kiasi cha hoja nyepesi zisizo na mashiko kuthaminiwa na kuonekana ndizo kila kitu. So sad.
 
Mwalimu Nyerere aliunganisha udongo wa nchi hizi mbili. Alitanguliza upendo zaidi hata hotuba zake zina msingi wa upendo...
Hakuna anayekataa kuwa Tanganyika na Zanzibar tumeungana.

Lakini muungano wetu umebainisha mambo ambayo ni ya pamoja ya muungano, na mambo yasiyo ya muungano.

Kiongozi yeyote asiyezingatia kwamba haya ni ya muungano, na haya sio, anavunja sheria.

Magufuli na Samia wamevunja sheria kwa kuteua Mzanzibari kuongoza wizara isiyo ya muungano.
 
Mwalimu Nyerere aliunganisha udongo wa nchi hizi mbili. Alitanguliza upendo zaidi hata hotuba zake zina msingi wa upendo...
Kuna umuhimu wakuwa na Serikali 3 , nakama Hilo haliwezekani basi tuwe na Serikali Moja, tuivunje Serikali ya Zanzibar natubakiwe na Serikali ya Tanzania tu.

Ili kudumisha huo umoja unaohubiri, Kwa nini umoja uonekane kwa vinavyoihusu bara tu, wao hawako tayari mtanganyika kuteuliwa Zanzibar.
 
..hakuna anayekataa kuwa Tanganyika na Zanzibar tumeungana.

..lakini muungano wetu umebainisha mambo ambayo ni ya pamoja ya muungano, na mambo yasiyo ya muungano.

..kiongozi yeyote asiyezingatia kwamba haya ni ya muungano, na haya sio, anavunja sheria.

..Magufuli na Samia wamevunja sheria kwa kuteua Mzanzibari kuongoza wizara isiyo ya muungano.
Kama anayefanya kazi kwa kuzingatia weledi na asipewe kazi kwa uzanzibari au utanganyika wake. huu ndio ubaguzi wenyewe.

Kwanini ujikite katika kumtazama mtu asili yake ni wapi?, Tanzania tumekuwa taifa lenye mtazamo finyu kiasi hiki?.
 
Kama anayefanya kazi kwa kuzingatia weledi na asipewe kazi kwa uzanzibari au utanganyika wake. huu ndio ubaguzi wenyewe.

Kwanini ujikite katika kumtazama mtu asili yake ni wapi?, Tanzania tumekuwa taifa lenye mtazamo finyu kiasi hiki?.

..Katiba ndio iliyotenga yapi ya muungano, yapi ya Tanganyika, na yapi ya Zanzibar.

..Sasa labda useme Katiba ni ya kibaguzi. Lakini Wale tunaosisitiza sheria ifuatwe hatustahili lawama.
 
Wajinga mtapinga lakini ndio ukweli wenye akili timamu wanaliona hili. Wanafiki wanaliona lakini kwa njaa zao watawatetea waarabu hao.
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WADAU
Nani anunue bandari ya wilaya ya Zanzibar au kata ya Pemba?
 
Erythrocyte ugonile.
Waziri anayeshabikia huu mkataba kausha damu Ni mzanzibari.
Katibu mkuu wake ambaye nae Ni signatory wa mkataba kausha damu Ni mzanzibari.
Hawa wazanzibari wamekuja kuleta maendeleo huku bara , maendeleo ambayo kule kwao hawayataki. Wangeyataka na bandari ya Pemba ingekuwamo.

Halafu mibunge sijui imepewa nini inashabikia wakati Kuna watu wanachekelea all the way to the bank.
 
Panua fikra zako usikariri maisha yaliyopita ukadhani ndio yatakuwa ya kesho.
Hakuna jipya lolote kwa serikali hii iliyojaa watendaji wale wale na wawekezaji ni wale wale.nafanya kazi kwa taasisi moja iliyobinafsishwa ukweli ni kwamba hakuna mwekezaji anayetaka kutupatia faida kubwa sisi.ni anatumia mbinu zote ku-declare faida kidogo kila siku na zaidi sana anaweka matumizi makuuubwa ambayo anafaidika yeye zaidi.
 
Back
Top Bottom