Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Naomba mwenye uwezo hawatag wale wote waliomjibu kwenye uzi wake uliopita ule waje kumshambulia Tena uyu Dikteta
 
Acha ukolon mamboleo, una viashiria vya udikteta uchwara
 
Unalazimisha kula pamoja ili mapaja yote ya kuku ule wewe kisingizio baba mwenye nyumba
 
Kujumuika pamoja kwaajili ya chakula hasa cha usiku ni jambo jema kwani karibu kila mwana familia anakuwa amekwisha wasili.

Lakini hatupaswi kuutumia muda wa kupata chakula kuhukumu na kutoa adhabu kwa mwanafamilia aliyekosa. Tuuache muda wa chakula upite hayo mambo mengine yaendelee baada ya watu kushiba.
 
huu utamaduni kwa mzee wngu upo, mda wa kula lzm wote muwe mezani mle kwa pamoja...
 
Yaani ni kaja tu kula sikukuu, haya sawa
 
Utaratibu w afamilia yako hapaswi mtu yoyote kuingilia na kama unauhakika utaratibu wa nyumva yako unakusaidia usiruhusu watu kuingilia kati...kama wanasema tofauti na itikadi zako wasikilize na uendelee na mambo yako kikubwa huvunji amani ya mtu wala sheria za nchi
 
Mpe muda,mazoea yana tabu,
Imagine we uende kwa shangazi alafu akawambie ndani kwake kulala ni saa1 jioni wote,utaweza?
Naamini mwanzo utapata tabu ila badae utazoea na kuadopt so mpe muda nae dogo huyo!
Mshamba sana huyu brother, hii ni roho mbaya yaan watanzania mtu akiwa na kamji kake anaweka visheria uchwara ili kuvimba tu.. mtu ana miaka 20 unataka kumpangia mpaka muda wa kushika sim!!
 
mmmh watu mna maisha magumu sana. Sio lazima aisee kula pamoja kila siku na eti wakati wa kula unaanza kuulizwa masuala ya shule etc khaa chakula kitashukaje hapo
 
Kila familia na utaratibu wake na utaratibu huo hupangwa na baba pamoja na mama kwahiyo watoto ni jukumu lao kufata utaratibu,,,
Pia wewe kama ni ndugu ukifika sehemu kuna utaratibu flani basi ufate huo utaratibu ikiwa ni sio uvunjifu wa sheria pamoja na haki,, ukiona utaratibu wa nyumba flani unakushinda unaweza kuondoka.
Kwahiyo mtoa mada yupo sahihi sabab n utaratibu wa nyumbn kwake wewe unaeona ni dikteta ni mtazamo wako.
Pia wengine wanalelewa kwa utaratibu wa hovyo sana anataka ale peke ake kila mda na anachagua vyakula kama mboga nk bila sababu,, kwahiyo wengine wanakula kinachopatikana na sio wanachokitaka kwahiyo fata utaratibu wa kila sehemu unapofika kama utaratibu umekushinda ondoka mara moja sio kulalamika bila sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…