Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Naomba mwenye uwezo hawatag wale wote waliomjibu kwenye uzi wake uliopita ule waje kumshambulia Tena uyu Dikteta
 
Nyumbani kwangu ikifika wakati wa chakula cha usiku (dinner) ni lazima tule pamoja kwenye chumba kimoja,

sasa kuna mtoto wa shangazi ni kama miaka 20 hivi hapendi kufata sheria ya mda wa dinner.

sheria ya muda wa mlo wa usiku ni kwamba simu hazitakiwi kutumika, simu inabidi ziachww vyumbani.

lengo ni kupata chakula cha usiku kama familia, ni muda ambao watu wote ndani ya nyumba tunajumuika, kila mtu anaelezea siku yake imeendaje, maendeleo ama changamoto kwenye shughuli zake, ushauri, kukumbushanana umoja ni nguvu, n.k.

sasa huyu dogo ni kama haheshimu huu utaratibu, yeye akija bado yupo busy na simu kwa kuibia ibia.

Shangazi yangu ni mtu ambae tumezoeana sana tangu nikiwa mtoto, naogopa nikimminya sana dogo ataenda kulalamika alafu ikala kwangu.

nimemwambia kama mara 3 anaacha ila anarudia.

suluhisho ni nini??
Acha ukolon mamboleo, una viashiria vya udikteta uchwara
 
Unalazimisha kula pamoja ili mapaja yote ya kuku ule wewe kisingizio baba mwenye nyumba
 
Kujumuika pamoja kwaajili ya chakula hasa cha usiku ni jambo jema kwani karibu kila mwana familia anakuwa amekwisha wasili.

Lakini hatupaswi kuutumia muda wa kupata chakula kuhukumu na kutoa adhabu kwa mwanafamilia aliyekosa. Tuuache muda wa chakula upite hayo mambo mengine yaendelee baada ya watu kushiba.
 
huu utamaduni kwa mzee wngu upo, mda wa kula lzm wote muwe mezani mle kwa pamoja...
 
Sipo hivyo mkuu, bianafsi ninajua kinachofanya watu wawe wanaogopa kula meza moja kwa huku afrika.

style yangu tofauti kabisa.

Na pia sio kama dogo anagekuwa ananiogopa hata hio simu angekuwa hathubutu kuja nayo, huyu dogo nimezoeana nae sana tu, ni yeye alietaa kuja mwenyewe huku kusherekea krismas, sio kwamba kalazimishwa na sangazi yake,
Yaani ni kaja tu kula sikukuu, haya sawa
 
Utaratibu w afamilia yako hapaswi mtu yoyote kuingilia na kama unauhakika utaratibu wa nyumva yako unakusaidia usiruhusu watu kuingilia kati...kama wanasema tofauti na itikadi zako wasikilize na uendelee na mambo yako kikubwa huvunji amani ya mtu wala sheria za nchi
 
Mpe muda,mazoea yana tabu,
Imagine we uende kwa shangazi alafu akawambie ndani kwake kulala ni saa1 jioni wote,utaweza?
Naamini mwanzo utapata tabu ila badae utazoea na kuadopt so mpe muda nae dogo huyo!
Mshamba sana huyu brother, hii ni roho mbaya yaan watanzania mtu akiwa na kamji kake anaweka visheria uchwara ili kuvimba tu.. mtu ana miaka 20 unataka kumpangia mpaka muda wa kushika sim!!
 
mmmh watu mna maisha magumu sana. Sio lazima aisee kula pamoja kila siku na eti wakati wa kula unaanza kuulizwa masuala ya shule etc khaa chakula kitashukaje hapo
 
Kila familia na utaratibu wake na utaratibu huo hupangwa na baba pamoja na mama kwahiyo watoto ni jukumu lao kufata utaratibu,,,
Pia wewe kama ni ndugu ukifika sehemu kuna utaratibu flani basi ufate huo utaratibu ikiwa ni sio uvunjifu wa sheria pamoja na haki,, ukiona utaratibu wa nyumba flani unakushinda unaweza kuondoka.
Kwahiyo mtoa mada yupo sahihi sabab n utaratibu wa nyumbn kwake wewe unaeona ni dikteta ni mtazamo wako.
Pia wengine wanalelewa kwa utaratibu wa hovyo sana anataka ale peke ake kila mda na anachagua vyakula kama mboga nk bila sababu,, kwahiyo wengine wanakula kinachopatikana na sio wanachokitaka kwahiyo fata utaratibu wa kila sehemu unapofika kama utaratibu umekushinda ondoka mara moja sio kulalamika bila sababu.
 
Back
Top Bottom