Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Kama una sheria ambazo mwenyewe, kuna baadhi ya excuse ya kuzisimamia..unajitengenezea double standards kupitia sheria zako.

Piga chini hayo masheria, yatakufedhehesha siku za mbele, acha ukoloni pia.

Kila la kheri.
 
Haya ni mambo yenu ya kifamilia hayatuhusu...

Kwani akila ameshika simu chakula kinaingilia kwenye nywele???
 
We endelea tu kumuonya mkuu kila akikiuka mwisho wa siku hata yeye ataona kero ataacha...ana madili gani makubwa kwenye hiyo simu hadi aone hasara kuiacha wakati wa kula

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Tumia sheria hii itakusaidia:

Chini ya dari langu ni sheria zangu, au kwa kimakonde under my roof my rule.

Kama ulishamkanya subiri siku kukiwa kuna msosi aupendao sana, siku hiyo akigusa simu mwambie aile hiyo simu yake na umfukuze mezani aende kuchat vizuri, usimuonee huruma wala haya. Halafu tupe mrejesho kama amebadilika au la
Kula akiwa na sm kuna kosa gani.huo ni unyanyasaji
 
Nyumbani kwangu ikifika wakati wa chakula cha usiku (dinner) ni lazima tule pamoja kwenye chumba kimoja,

sasa kuna mtoto wa shangazi ni kama miaka 20 hivi hapendi kufata sheria ya mda wa dinner.

sheria ya muda wa mlo wa usiku ni kwamba simu hazitakiwi kutumika, simu inabidi ziachww vyumbani.

lengo ni kupata chakula cha usiku kama familia, ni muda ambao watu wote ndani ya nyumba tunajumuika.

sasa huyu dogo ni kama haheshimu huu utaratibu, yeye akija bado yupo busy na simu kwa kuibia ibia.

Shangazi yangu ni mtu ambae tumezoeana sana tangu nikiwa mtoto, naogopa nikimminya sana dogo ataenda kulalamika alafu ikala kwangu.

nimemwambia kama mara 3 anaacha ila anarudia.

suluhisho ni nini??
Mbona Una pafanya nyumban kwako kama gerezani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww ni hasidi,huyu ndugu yako Bora aondoke hapo aepukane na hasad zako
Ana tunga Sheria za kikoloni mtoto akiwa ana tumia simu muda wakula wamuache wao waendelee Kula tu mtoto akija kushtuka wenzake washafika mbali siku nyingine akili ita mkaa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia sheria hii itakusaidia:

Chini ya dari langu ni sheria zangu, au kwa kimakonde under my roof my rule.

Kama ulishamkanya subiri siku kukiwa kuna msosi aupendao sana, siku hiyo akigusa simu mwambie aile hiyo simu yake na umfukuze mezani aende kuchat vizuri, usimuonee huruma wala haya. Halafu tupe mrejesho kama amebadilika au la
kweli kuna watu mko kauzu zaidi ya dagaa[emoji1787]
mimi ujasiri huu sina
 
Shangazi yangu ni mtu ambae tumezoeana sana tangu nikiwa mtoto, naogopa nikimminya sana dogo ataenda kulalamika alafu ikala kwangu.

nimemwambia kama mara 3 anaacha ila anarudia.

suluhisho ni nini??

Tumia huo Urafiki na Ukaribu na shangazi kumweleza Juu ya Uvunjifu Wa sheria zako unaofanywa na Mwanaye, ili amkanye..
 
Ukiona hivyo ujue hamna mazoea kihivyo.

Mtoto anakula Hana wa kupiga naye Stori hivyo anakuwa bored. Simu ndio inampa kampani.

Wakati WA Kula jaribu kumpisha Stori Kwa kumpa mada za kuchangia Kama vile mpira, muziki, n.k.

Hata Mimi ningekuwa kwako wakati WA Kula alafu sina wakupiga naye Stori huenda ngefanya hivyo hivyo.

Alafu chukulia huyo Kwa sasa ni mtu mzima, miaka 20 ni mingi.

Sio ulete sheria za wakati Kula hakuna kuongea ukadhani kanuni hiyo inatumika Kwa watu wazima piah
Mkuu muda wa dinner kuna maongezi yake, hayo mambo ya mpira huwa ni sebuleni na mimi ni kijana nina 31 nakua ni vitu gani vya kuongea na hawa madogo maana hatujapishana sana.

Tatizo linapokuja ni kama vile anapenda kuchanganya maongezi ya kwenye dinner na simu kwa wakati moja.
 
Upo wakati unafika vile unavyovipenda wewe siyo lazima wengine wavipende.

Ipo siku hicho chakula utabaki na mkeo tu hapo dining room wengine watavizia mkishakula ndo waje kuchota chakula wakale vyumbani mwao.

Ushukuru hata kama wanasogea wakati wa kusali.

Kubali tu kila zama zinakuja na kupita.
 
Upo wakati unafika vile unavyovipenda wewe siyo lazima wengine wavipende.

Ipo siku hicho chakula utabaki na mkeo tu hapo dining room wengine watavizia mkishakula ndo waje kuchota chakula wakale vyumbani mwao.

Ushukuru hata kama wanasogea wakati wa kusali.

Kubali tu kila zama zinakuja na kupita.
Sipo hivyo mkuu, bianafsi ninajua kinachofanya watu wawe wanaogopa kula meza moja kwa huku afrika.

style yangu tofauti kabisa.

Na pia sio kama dogo anagekuwa ananiogopa hata hio simu angekuwa hathubutu kuja nayo, huyu dogo nimezoeana nae sana tu, ni yeye alietaa kuja mwenyewe huku kusherekea krismas, sio kwamba kalazimishwa na sangazi yake,
 
Nilianzisha uzi flani hapa jana


baadhi ya comments watu wamenifananisha na diktekta kwa utaratibu wangu wa kila mtu kujumuika kwenye meza ya chakula usiku.

Kwanza niseme tu ya kwamba ninajua tayari mambo yaayofanyaga watu wachukie kula pamoja usiku, sababu ni kama baba ukiwa mkali sana kuogopwa, kuifanya dinner kuwa mahakama ndogo, n.k.

Binafsi kwa kuyatambua haya sikukurupuka kuanzisha huu utaratibu,

mimi ni mtu friendly sana kwa watu wanaoishi kwangu, hata kwa jinsi house girl alivyonizoea ni kama kaka yake


na hata siku moja sijawi kuifanya dinner kuwa mahakama ndogo
 
Huo Ni ujima,udikteta na ushamba!! Unafosi mtu ale na wewe ili iweje sasa??
 
Duuh kuna muda hutojisikia jamen kula muda huo
Sawa
Sasa mzee tukimuita Nduli Idd Amin anasema kuwa watu wamemuita dikteta. Ofcourse sio kila wakati utakwepa kula mezani ila kuna muda haujiskii kula lazma uta dodge tu kama anataka awaone wanafamilia basi aombe wakae tu sebleni.
 
Back
Top Bottom