Mtu mwenye uwezo kuliko wewe kifedha unaweza kumpa zawadi gani?

Mtu mwenye uwezo kuliko wewe kifedha unaweza kumpa zawadi gani?

Habari zenu wakuu.
Tufanye una ndugu au jamaa yako aliyekupita mbali kifedha, unaweza kumbebea zawadi gani ili usiende mikono mitupu? Ile imetokea tu unataka kwenda kumtembelea sio kwamba ni mgonjwa au ana changamoto yoyote.
Mnunulie chupa ya whisky, au wine safi. Hakuna mtu anaacha kufurahia zawadi kama hiyo labda awe mlokole au mwisilamu shehe ubwabwa wanaojionyesha
 
Kwa tanaduni zetu watu wa nyanda za juu kusini,
Ni mwiko kwenda kwa watu mikono mitupu.
Hata kama wewe ni bilionea, lazima nibebe chochote.

Na ukija kwetu, Lazima tukupe kitu, hata kama umeleta vikubwa kiasi gani
Hauondoki mikono mitupu .
Umeona eeh? Hata wenyeji watashangaa japo hawatasema chochote
 
Andika kwa kuchonga kwenye Kibao kizuri cha mbao (au tafuta wa taalamu wa sanaa hiyo) maneno haya 'muda huu utapita'.
Maneno hayo yana tumika kwenye hali mbili tofauti ambazo ni wakati wa furaha sana na wakati wa huzuni sana.
Asante kwa mawazo boss
 
Back
Top Bottom