Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Faida zipo, wakimbiza mwenge wanapata per diems na posho zingine, wauza condoms wanauza za kutosha ndio maana unapolala asubuhi yake zinaokotwa nyingi zilizotumika.
 
Faida za mwenge:- (kumbuka faida ya upande mmoja inaweza kuwa hasara kwa upande wa pili)
- Ni wakati wa kuuza sura kwa wakimbiza mwenge na kupata mademu wapya
- Ni kipindi cha kuvuna per diem bila kwere
- Ni wakati mzuri wa kuwaroga watanzania wote wasizinduke kwenye usingizi wa ujinga waendelee kuridhika na maisha yao ya kimaskini huku wakifurahia kufunguliwa baadhi ya miradi isiyoendelea
- Ni wakati mzuri wa wanafunzi kulala nje na nyumbani kwao wakisingizia wameenda kupokea mwenge.
 
Kennedy wewe unachezea ban hivihivi! unatukana mwenge!! hauugopi? Kumbuka hii kitu mwenge hadi wakuu wa wilaya wanaogopa. Unakuja hapa town tar13/09 au 14. Maandalizi yake sasa mara sare, mara magari mara wakuu wa idara kujipanga. Safari za kwenda kukagua miradi ya maendeleo sasa hizo fedha zinatosha kununua vitanda 20 na kuviweka hapa maweni kwenye wodi za wajawazito na watoto. Nasikia kule Kasulu kuna mtu aliwahi kuukojelea kipindi cha nyuma subiri nitafute huo mkasa niauelezea kilichompata.
Nafurahishwa na kile kiitikio chao cha mwisho MWENGE HOYEEEEE!!!!
 
wizi mtupu ni mradi wa kujipatia kipato
walishakuja kudai hela ya mwenge nkawatimua
mwenge ni janga la kitaifa
bilioni walizotumia zingejenga mashule na zahanati
kama ni kuzindua mkuu wa wilaya anaweza kuzindua miradi
 
mwenge ni more spiritual zaidi, nahisi una siri kubwa, pia nadhani ule ni zaidi ya mwenge, kwani wao hawaoni hizo hasara? ulimsikia lini SLAAA,MBOWE LIPUMBA N.K wanaushutumu unamaliza pesa? hebu jiulize lile lifimbo bungeni ni la nini hadi kuwe kuna high respect kiasi kile
 
Ni mradi mwingine wa jamaa kupiga pesa irresponsibly tu!!!!!
 
Ninavojua mm, one of the symbols used by secret societies km &illuminati' na wengine. Hii ni pamoja na matumizi ya alama ya jicho,piramidi nk. Kama mwenge wa Olimpic unatumiwa pia na hao jamaa. Nimekuwa nikijiuliza sana wazo la kukimbiza mwenge lilitoka kwa nani na ilikuwa mpaka ykafikiwa maamuzi ya kwamba uzungushwe nchi nzima. So,tunatumiwa au tuliiga tu bila kujua?,
 
chief72 na @Tram Almas kuna ukweli katika post zenu. nliwahi kusoma mahali. . .
 
Last edited by a moderator:
Hiv kikwete unaujasiri gani katika Taifa lililofikia hapa Polisi wanaua raia, raia wameanza kuua polisi, Waislamu wanachoma makanisa. Leo hii Kikwete unasema tunaumoja na utulivu. Hiv rais huoni shida kusema kuna amani na utulivu? Zanzibar wamechoma makanisa wakristo tumenyamaza hiv waislamu wako juu ya sheria?

Inasikitisha sana kuona Tanzania aliyoiacha mwalimu Nyerere imeharibiwa na uongozi uliopo madarakani kwa kuendekeza ushabiki wa kidini na tangu kuingia madarakani viongozi wengi umewaweka waislamu.

Wakristo tuendelee kumwomba mungu atende ili taifa hili likombolewe mikononi mwa wadhalimu CCM ili tuachane na chama hiki ambacho nimeamini ndo chenye kuleta mgawanyiko kati ya wenye nacho na wasio nacho, wakristo na waislamu. Na ndiyo maana leo kuna shule za wenye pesa na wasio na pesa.
 
hiv kikwete unaujasiri gani katika taifa lililofikia hapa polisi wanaua raia, raia wameanza kuua polisi, waislamu wanachoma makanisa. Leo hii kikwete unasema tunaumoja na utulivu. Hiv rais huoni shida kusema kuna amani na utulivu? Zanzibar wamechoma makanisa wakristo tumenyamaza hiv waislamu wako juu ya sheria?

Inasikitisha sana kuona tanzania aliyoiacha mwalimu nyerere imeharibiwa na uongozi uliopo madarakani kwa kuendekeza ushabiki wa kidini na tangu kuingia madarakani viongozi wengi umewaweka waislamu.

Wakristo tuendelee kumwomba mungu atende ili taifa hili likombolewe mikononi mwa wadhalimu ccm ili tuachane na chama hiki ambacho nimeamini ndo chenye kuleta mgawanyiko kati ya wenye nacho na wasio nacho, wakristo na waislamu. Na ndiyo maana leo kuna shule za wenye pesa na wasio na pesa.
op-out of the point
suala linalojadiliwa ni mwenge unaleta habari za kikwete ,uislamu na ukristo?what`s this bana?
 
Mwenge waUHURU hukimbizwa kila mwaka nchi nzima ukiwana kauli mbiu mbalimbali, katika mbio hizo mwenge huzindua majengo mbalimbaliya umma kama vile Ofisi, Zahanati na Shule ambapo zaidi ya 95% ya majengo hayo yanakuwa yamejengwa chini ya kiwango.Utasikia ndugu mgeni rasmi ofisi hii imegharimu shilingi milioni 10 wakati ujenzi wake halisi umeghlimu shilingi milioni 2. Hamisi Kagasheki mkoaniKagera aliwahi kuamuru shule iliyofunguliwa na Mwenge ipigwe nyundo yote kabla haijatumika kisa ilikuwa na nyufa za kuweza kupitisha simu ya mkononi.
Mwenge wa uhuru una gharama zifuatazo:
a) Mafutaya magari kuzunguka nchi nzima.
b) Malipokwa wanaoukimbiza nchi nzima.
c) Magariya kuzunguka nchi nzima na matengenezo yake ya mara kwa mara.
d) Gharamaza maandalizi ya kila mahali utakapolala nchi nzima.
e) Gharamaza walinzi mahali unapolala kila usiku nchi nzima.
f) Muda wananchi wanaopotezakuusubiri na kukesha nao n.k
Maswali ninayohitaji wenzangu mnisaidie majibu yaje:
a) Mbonakila mwaka mwenge unapozimwa hatujawahi kusomewa mapato ya mbio hizo?
b) Tunapatafaida gani kutokana na kuukimbiza mwenge kila mwaka?
c) Hivikweli viongozi wa mbio za mwenge wanapozindua majengo yanayotaka kubomokahawaoni kuwa yako chini ya kiwango?
WABUNGE WETU MWENGEHATUUTAKI,,,,,,,,,,,,,. HAUNA TIJA KWETU ……..
 
Jamani mimi mtanzania mwenzenu naomba mnisaidie hivi ule mwenge unaotembezwa nchi nzima kwa mbwembwe na gharama kibao faida yake ni nini? Kwa maisha ya watanzania kama akina sisi ambao kwetu Zahanati hamna shule hamana walimu wako kwenye mgomo kwa kudai mshahara uongezwe vituo vya afya havina dawa wala madakitari polisi ndo usiseme magari hamna hata penye gari mafuta hamna ikumbukwe kuna watu wanakufa katika nchi hii kwa kukosa dawa za marelia

Mwenye jibu anipe faida za mwenge zinazolingana na gharama zinazotumika kwenye mwenge kutembezwa nchi nzima zingatia unapokuwepo mwenge magari ya serikali na wafanyakazi wa serikali hufunga ofisi za umma wakaenda kuuza sura huko na kuwakosesha watz huduma mablimbali mhimu.
 
Wafanya kazi wote chini ya halmashahuri wanakatwa kwa lazma kuchangia mwenge. Wengi ni walimu na watumishi wa afya!
 
Mwenge wetu ni kielelezo cha uhuru, unamlika mabepari na huleta amani kila penye chuki, huleta mshikamano penye mgawanyiko(enzi za mwalimu). Huleta magonjwa hasa huku kwetu kijijini ambapo ukilala tunakesha tunacheza ngoma za kimila(enzi za sasa)
 
wastage ya pesa ya kodi zetu, ni upuuzi mtupu!
Si kodi tu baadhi ya halmashauri hukata mishahara ya watumishi kuchangai mbio za mwenge!! wakurugenzi huwa mnapata ridhaa ya muwakatao??
 
na nukuu katika bibilia,[isaya 50;11,tazama ninyi nyote mwashao moto,mjifungiao hiyo mienge;enendeni ninyi katika mwali wa moto wenu,na katikakati ya mienge mliyoiwasha,mtayapata haya kwa mkono wangu;mtalala kwa huzini,]mwisho wa kunukuu,swali langu kwa serikali ya ccm,kwanini wanaukimbiza mwenge na kutuletea watanzania laana,tafsiri ya neno kulala kwa uzuni,ni [a]umaskinimagonjwa[c]ulala hoi] kwa kutokujua au kwa kujua ccm imetuletea haya na mwenge wao,ndio maana hata fedha yetu haina thamani,inazidi kushuka samani,ushauri wangu kwa serikali ya ccm,warudi kwa mungu na kitubu,kisha waache kuukimbiza mwenge wao katika nchi,mungu atali bariki taifa hili,karibuni wana jf kwa michango yenu,na wasilisha,
 
Back
Top Bottom