Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Tambiko la Serikali.

ndio maana nasema wanajua maana ya huo mwenge wao unaotuletea laana na sisi tutamwomba mungu waondoke nao na ujue kwamba mungu amekasirika ndio maana chama kina nuka mbele ya watanzania,tena wasifikirie chadema ndio mbaya wao,wanajisumbua mungu amesha wakataa,wasubiri,2015,ndio watajua,chama kinapoteza mvuto kila kukicha,watanzania wana mlilia mungu kwa nini sisi ni maskini,miaka 51 ya uhuru bado cc maskini wakutupa,na mungu anashusha bakora yake na kuwaponya watanzania,
 
nilitaka kuingia kichwakichwa kumbe ni ya 31st May 2007.
 
Ndugu zangu wana JF, Leo hali hewa imechafuka kwa muda bungeni ktk kipindi cha asubuhi wakati wa maswali na majibu mara baada ya Mbunge wa Nkansi, Mh. Kessy kuuliza swali la nyongeza kwa serikali kwamba "hawaon kwamba MWENGE WA UHURU HAUNA FAIDA TENA KWA WATANZANIA ZAIDI YA KUIBEBESHA GHARAMA SERIKALI NA ZAID ZAID KUSIMAMISHA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI WAKATI UKIPITISHWA MAENEO KADHAA YA NCHI? Waziri akasimama akajiumauma kujibu na baadae WAZIRI MKUCHIKA akasimama kuongeza majibu lakin mwisho wake MKUCHIKA na MAKALA kaambulia ZOMEA ZOMEA tuu toka kwa wabunge.

Source:TBC Kipindi cha bunge.
 
Mh.Kessy ni mbunge pekee wa ccm asiye na unafiki!Wengine wanakula kodi zetu bure
 
Ndugu zangu wana JF, Leo hali hewa imechafuka kwa muda bungeni ktk kipindi cha asubuhi wakati wa maswali na majibu mara baada ya Mbunge wa Nkansi, Mh. Kessy kuuliza swali la nyongeza kwa serikali kwamba "hawaon kwamba MWENGE WA UHURU HAUNA FAIDA TENA KWA WATANZANIA ZAIDI YA KUIBEBESHA GHARAMA SERIKALI NA ZAID ZAID KUSIMAMISHA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI WAKATI UKIPITISHWA MAENEO KADHAA YA NCHI? Waziri akasimama akajiumauma kujibu na baadae WAZIRI MKUCHIKA akasimama kuongeza majibu lakin mwisho wake MKUCHIKA na MAKALA kaambulia ZOMEA ZOMEA tuu toka kwa wabunge.

Source:TBC Kipindi cha bunge.

Mwenge wa Uhuru sasa hivi hauna IDEOLOGY kama zamani, hapo kale ulikuwa na mantiki ya ukweli maana hata kama jana wapendwa waligombana siku ya mwenge watashiriki mchaka mchaka wakiimba "Ulete amani" kati yao, ilikuwa kama vile "DINI" fulani.

Leo mwenge huu ni kama "Guest House" kwa wote kwenda kuvunja amri ya 6 NI ZINAA TU HUTAWALA WAKATI WA MKESHA WA MWENGE. Pigeni marufuku mwenge kukesha.

Zamani tuliimba hivi, "Mwenge huo mweng, mbio mbio, umulike mafitini, mbio mbio, utuletee amani, mbio, mbio!!!

Leo wimbo ni, "Mwenge huo mwenge mbio mbio UTULETEE UKIMWI MBIO MBIO, HATA WATOTO WADOGO MBIO, MBIO......"

Hakuna cha maana juu ya hilo. Mikesha ya mwenge ipigwe marufuku kabisa.
 
subirini mkiingia madarakani yote hayo hayatakuwepo kwa sasa hayawahusu hata kidogo
 
Nashindwa kuelewa hili taifa ambalo laitwa masikini wakati kodi nyingi zinakusanywa kutoka kwa wananchi vilevile kodi hizi zinavyotumika inashangaza pia...serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi kwa ajili ya kugharamikia shughuli za mwenge, huu mwenge una faida gani jamani? Ni kweli kuwa lengo lake ni kuwakimbiza maadui katika mipaka? Kivipi?
Hebu nielewesheni watanzania wenzangu...maana akili yangu haitaki kubali hili!!!
 
bendera inaigharimu pesa taifa? nyimbo na picha? vitu hivyo unavyovitaja wewe,vinatumia pesa za walipa kodi?
 
bendera inaigharimu pesa taifa? nyimbo na picha? vitu hivyo unavyovitaja wewe,vinatumia pesa za walipa kodi?

hivi unajua kununua picha rasimi ya raisi siyo chini 15000 na maofisini unapaswa kuwa nayo ingawa mimi ninayo ya dr slaa
 
hivi unajua kununua picha rasimi ya raisi siyo chini 15000 na maofisini unapaswa kuwa nayo ingawa mimi ninayo ya dr slaa

Kama unajua unapaswa ofisini kuwa na picha rasmi ya Rais halafu wewe unakuwa na ya Dr. Slaa, akili zako zipo sawa kweli?!
 
Mwenge ulikuja hapa Arusha kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 800 kuja kuzindua matundu ya choo yaliyogharimu wananchi shilingi Laki 5.

Mimi nadhani kazi ya mwenge ni kuzindua miradi sugu ambayo Rais na serikali yake wameshindwa kuzindua, ndiyo tuseme moto wa kale ka karabai ni kiboko ya miradi sugu ambayo hata DC hawezi kuzindua.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hebu nielewesheni watanzania wenzangu...maana akili yangu haitaki kubali hili!!!

Umeshasema akili yako haitaki kukubali halafu unaomba tukueleweshe. Sasa kama akili yako imeshakataa kukubali ukieleweshwa utaelewa?

Huko kijijini kwenu mwenge ulikuwa haupiti? Inawezekana kabisa umekuwa hai mpaka leo hii kutokana na mradi/miradi iliyotokana na mbio za mwenge.
 
Kama unajua unapaswa ofisini kuwa na picha rasmi ya Rais halafu wewe unakuwa na ya Dr. Slaa, akili zako zipo sawa kweli?!

Slaa ni rais anayeongoza kwenye mioyo ya watu, wakati Kikwete ni rais anayetawala kwenye mioyo ya NEC na Polisi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom