Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
watu wa bukoba wamekejeliwa na michango yao kutiwa kwapani huku watu wanalipia kuabudu moto kwa sherehe
 
Kweli hata mimi hadi leo hii sijui faida hasa ya mwenge.

Ila hawa wanao utetea humu nina wasi wasi ndio labda wanao faidika nao.
Watuambie wanafaidika vipi nao!!!
 
Mwenge ndio uchawi wenyewe... sema watu hawajui. Ni kama kuwapumbaza watanzania waendelee kuwa wajinga...
 
Ule ni mvuaza mzee acha uzunguke uwendelee kutuvuaza maana 2020 sio mbali panapo majaaliwa
 
Kwani amezindua mwenge wa uhuru wa kule kwao ZNZ, au ni ule mwenge wa uhuru wa Tanganyika? ikizingatiwa Tanzania haikuwahi kuwa koloni hapo kabla!
 
Hizo Bilioni 400 tupe mchanganuo wake...maana kwa kudandia matukio hamjambo.

Tafadhali tupe mchanganuo wake kama unaufaham....
 
ni vizuri kuuona mwenge hauna faida,maana kuna mengi yanayotendeka unaweza ukaona hayana faida hata uingereza wanaona gharama kuitunza familia ya kifalme japo nayo inautajiri wake
 
Mwenge ni kiashiria tosha kwamba nchi inaendeshwa kishirikina. Hauna faida yoyote zaidi ya ccm kuutumia kama sehemu ya kuwapumbuza wananchi hasa wa vijijini. Siku hizi huo mwenge umekosa mvuto mpaka unatumika ubabe kuhakikisha eti watumishi wa umma wanakesha kwenye mwenge tena kwa lazima.
 
Ni nembo ya taifa Kama nembo nyingine,

Asiyejua maana haambiwi maana
 
Unaweza kudhibisha " hiyo bajeti ya bilioni 400 kuwa ni sahihi.!
 
Hauna faida yoyote bali kuwaonea wafanyakazi wa Serikali hasa walimu ambao nchi nzima wanakatwa pesa zao chungu nzima tena bila ridhaa yao eti kwa mafuta ya mengi. Ni wizi mtupu wa mabilioni ya pesa za walipa kodi na kwa kujua kumejaa wizi kwenye pesa hizo hawataki CAG azikague.
Walimu acha wakatwe tu maana wamezubaha sana
 
hawatasema ila nahisi hii kitu inaendana na imani za kishirikina..kila mwaka hela kibao zinapotea..hata bwana yule aliesema anabana matumizi bado kaufyata.. wangefanya basi mara moja kwa miaka mitano..toka niko primary school miaka ya tisini hadi leo kila mwaka unazunguka tu..kuna kitu lazma
 
Pesa za kuwalipa watumishi hawana ila za kukimbiza hiyo tochi wanazo. Bajeti ya mwaka iliyopita haijafanya kazi wamefichama kwenye zimwi walilofinyanga liitwalo uhakiki.
Siku nikimkuta mwanaccm Analiwa na simba namkatia simba kachumbari ili ashibe sawasawa.Yanamalenga mwemwe. Hivi uchaguzi ni lini?.
 
Mwenge hauna tija yoyote kwa karne hii ya viwanda. Ni kupotezeana muda na gharama pasipo Sababu
 
Kuna baadhi ya viongozi wanaabudu moto lakini huuita mwenge, ndio maana unawakuta hawana hofu na Mungu kwa ufisadi wanaoufanya.😡
 
Habari wadau!

Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.

Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.

Nini faida yake?
Mkuu hapo hakuna faida..ni uzandiki tuu wa miafrika. Ni aibu kungangania vitu visivyokuwa na maana na kuacha kufanya vitu vya maana. Mwenge ni kati vitu vya kipuuzi ambavyo serikali hii ya ccm inavitumia kuwaibia watanzania, ni miradi ya wanaccm. Bahati mbaya hata wananchi wenyewe hawafahamu hilo. Can you imagine ni kiasi gani cha fedha zinatumika kugharimia huo upuuzi. Je hizo fedha na rasilimali zisingetumiaka katika miradi ya maendeleo, mfano ni hospitali ngapi zingepata dawa na wananchi wangapi wangetibiwa..the list is endless.....

Upuuzi wa masoud kipanya!!!!
 
Back
Top Bottom