DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,679
Acha kudanganya watu wewew Mwenge hauna lolote siku hizi umefulia, hauna mvuto kama sisiemu!
Ngonini au ngonan ebu tupe alternative?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha kudanganya watu wewew Mwenge hauna lolote siku hizi umefulia, hauna mvuto kama sisiemu!
Kama ni amri yangu ningeufuta mara moja.
Wazo muafaka. Mwenge ni mojawapo ya national symbols kama ilivyo kwa bendera ya taifa na wimbo wa taifa. National symbols zo zote zile huwa zinalisaidia dola kutawala, kudhibiti, kupumbaza na hata kukandamiza watawaliwa. As long as tuna dola, ni lazima hizo symbols ziwepo. Baadhi ya symbols zina maudhi na hasara na nyingine zipo tu hazipunguzi wala kumwongezea hasara mwananchi wa kawaida. Mwenge ni mojawapo ya symbols zenye maudhi na hasara na kero kama ulivyoainisha vizuri. Tunachoweza kufanya ni iwapo "wenyenchi" watakubali kuwepo na mchakato huru wa kubadilisha katiba, hapana budi tukubaliane juu ya symbols za taifa zisizowaletea kero wananchi ndio zibaki kutambuliwa. Mwenge ukatwe kabisa na kuwekwa kwenye makumbusho ya taifa!!
mwenge ufutwe utupiliwe mbali
hata kama Mwenge ungekuwa na uwezo wa kumulika kama wanavyotaka tuamini, sisi wenyewe timefumba macho... hayo maovu tutayaonaje?kama kuna mambo ambayo tunapaswa kuyakataa ni kuamini ya kuwa mwenge wa uhuru unao uwezo wa kuyamulika maovu kwenye jamii na kuyakemea...
kama kuna mambo ambayo tunapaswa kuyakataa ni kuamini ya kuwa mwenge wa uhuru unao uwezo wa kuyamulika maovu kwenye jamii na kuyakemea.........kama sisi tulioutengeneza huo mwenge kazi hizo zimetushinda yawaje.....................kiumbe kisicho na uwezo wa kuongea au kutembea au kuona kiweze kufanya hiyo miujiza..................kila mahali mwenge uendako unahitaji kubebwa na wale ambao wamekiri kero zetu zimewashinda na wapo kwenye nafasi zao serikalini kula tu.......................au niseme kutumikia matumbo yao pekee yake................ambayo ndiyo wanayoyaabudu?
ndiyo maana kila mwenge uendako raia wengi huendelea na shughuli zao za kutafuta lishe........na kuwaachia wapumbavu ndani ya serikali kuendelea kujidanganya ya kuwa mwenge ambao ni mfu kuwa ndiyo suluhishi ya matatizo yetu................................magari yenye nambari za sth, pt, dfp....n.k........na su za hapa na pale huwa yanaukimbiza mwenge..............huku polisi wakionyesha ya kuwa hii "takataka" ndiyo kipaumbele chetu kwa kuzuia magari barabarani yasiendelee na shughuli za ujenzi wa taifa..........kupisha sanamu ipite.......huku wabunge wakilitukuza Bunge ambalo linawapatia ulaji uliokithiri kuwa saawia na Muumba yaani nalo Bunge ni TUKUFU kama Mwenyezi Mungu.............................hatuna kiongozi ndani ya serikali ambaye anaweza kusimama kidete na kukemea ufujaji wa mali za umma ambao tuliigia kutoka kwa wachina.................wao siku hizi sioni wakiukimbiza mwenge ila wanafukuzia dola za mmarekani na mali ghafi kutoka kwa wazubaifu kama sisi.......................
Nijuavyo mwenge ni kiini macho chakutufanya tusahau kero zetu na akina nani ndiyo wamezisababisha na ya kuwa kamwe mwenge hauwezi kuwa mkombozi wa mtanzania ila nijuacho tuendelee kuwaacha wafu wazike wafu wenzao kupitia hii aibu ya kitaifa...................